Mimi nashangaa uwezo wa wachangiaji wengine humu ndani, hivi ukisoma taarifa yeyote huwezi kujishughurisha kufanya upekuzi ujue undani wa jambo ndio uchangie? Hii ndio forum ya watu waelewa kweli: Wanaopinga msimamo wa Rusia juu ya majimbo ya kusini mashariki mwa rusia hajui historia na sera za nchi mbambali duniani zinazohusiana na Mali za taifa. Rusia ina mali zake Ukrain, ambapo ni raia wenye asili ya Rusia walioishi maeneo ya Ukrain kabla na baada ya USSR kuvunjika..ukitaka kujua vyema google ramani ya enero la kiutawala la USSR kabla na baada ya kuvunjika. maeneo ya kusini mashariki mwa Ukrain wapo warusi (Pro-Rusian) ambapo Rusia kwa sera zake hao ni Rusia National Interest, hakuna atakayepinga Rusia kulinda kilicho chake popote pale Duniani, hizo ni sera za mataifa mbalimbali, marekani analijua hili na ndiyo maana kwa ujumla katika kuujadili mgogoro wa Ukrain Rusia ni muhimu sana kwani sehemu kubwa ya nchi hiyo inakaliwa na pro-rusian. Rusia katika mgogoro wa Ukrain wapo sahihi kabisa, kushutumu na kutokuunga mkono namna uongozi uliochaguliwa kwa demokrasia ulivyoondolewa madarakani na kuwapa vibaraka wa Marekani, pili hawawezi kukaa kimya na hali wana wananchi wao sehemu ya ukrain,. Utetezi wa Rusia kwa watu wa kusini mashariki ya Ukrain hauna tofauti na msimamo wa Marekani kutetea raia wake mahali popote duniani. swali la msingi Je, Tanzania inatekeleza vipi talatibu za kutetea na kulinda raia wake? katika misingi ya sera za mambo ya nje na utekelezaji wake.