Hatimaye Nimepata Heka 5 Msolwa

Mavu
Hivi kitaalamu ukilima heka moja mahindi kwa kufuata kanuni zote mbegu nzuri. Heka itatoa gunia ngap??
Mavuno yanatokana na 1) Aina ya mbegu, 2)Matumizi ya mbolea kwa usahihi, 3)usafi wa shamba 4)Hali ya hewa/Upatikanaji wa maji bila ya kusahau 5) Nafasi kati ya mche ne mche pamoja na mstari
 
Mkuu udongo wa ukanda huo tikiti pia linakubali..!kipindi cha mvua lakini..!ushauri tengeneza miundombinu ya kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya umwagiliaji coz ukanda huko mvua ni nyingi..!watu wanalima vuli na masika wanapata..
 
Mnavyoongea mi huwa siwaelewi. Unamaanisha acre ambayo kiswahili ni ekari ama hectare (kiswahili ni hekari)?
Btw hekari 1 = ekari 2.47 za ardhi.
Ukilima ardhi nzuri, taratibu zote ukazifuata na mbegu bora unavuna hata gunia 70 za mahindi kwa ekari.
Lakini wengi wanaishia gunia kati ya 20-30 sababu ardhi imechoka na acidic content ni kubwa.
Na wengine anapata 5 tu. Ni uwekezaji
Sorry nilikuwa nje ya mtandao kwa muda, nilimaanisha ekari yaani ile ya 70*70 yenye mita za mraba 4900

Okay.. Sasa nimekusoma hivi gunia 70 Kwa akari moja!!??? Aisee ikiwa hivyo itakuwa raha Sana. Sasa tuoteshe mbegu gani kwa mashimo yawe na umbali kiasigani??
 
Hongera sana kiongozi, mimi ninakijishamba maeneo ya mboga (Msoga kwa mbele)
nakushauri kwa nature ya uoto wa pwani, ukifyeka tu hakikisha unang'oa visiki, kwasababu ukifyeka pekee vichaka havikawii kuchipua hivyo pori litajirudia upya
Wenyenyi wananishauri eti nilime misimu miwili ili visiki vioze ndio moving'oe kwa bei rahsi na kwa uraisi zaidi
 
Mkuu udongo wa ukanda huo tikiti pia linakubali..!kipindi cha mvua lakini..!ushauri tengeneza miundombinu ya kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya umwagiliaji coz ukanda huko mvua ni nyingi..!watu wanalima vuli na masika wanapata..
Upo sawa kaka naambiwa na wenyeji kuwa mvua ni nyingi na wao wanalima twice a year
 
Wenyenyi wananishauri eti nilime misimu miwili ili visiki vioze ndio moving'oe kwa bei rahsi na kwa uraisi zaidi
Hapana kiongozi sikushauri, visiki vinachipua kwa speed na kufunika mazao, itakupasa kufyekea maotea mara kwa mara, gharama itarudi palepale, mimi nimekula hasara ya ekari sita, nilizilima zote, mbili nikazipanda na nikazitelekeza, nikaona bora ning'oe tuu, kwani upande huo kung'oa sh ngapi/ekari?
 
Wakati unafikiria cha kulima pia fikiria utakiuza wapi usije kulia bure.

Kingine hao wenyeji usiwaone wajinga kulima mahindi na maharage, ukiingia shambani utaelewa sababu pale ambapo utakapo vuna halafu bei sio nzuri na zao ulilolima halihifadhiki mfano tikiti na hayo mapapai unayotaka
 
Good job ila .make sure unazindika shamba kwanza vijiji hivyo ni nuksi kwa uchawi LA sivyo hapo utakua huambulii kitu kabisa
 
Hapana kiongozi sikushauri, visiki vinachipua kwa speed na kufunika mazao, itakupasa kufyekea maotea mara kwa mara, gharama itarudi palepale, mimi nimekula hasara ya ekari sita, nilizilima zote, mbili nikazipanda na nikazitelekeza, nikaona bora ning'oe tuu, kwani upande huo kung'oa sh ngapi/ekari?
Wanasema wana ng'oa kwa laki mbili.. Ila kufyeka kwa heka ni 45,000/=
 
Hiyo almond ni bidhaa moja expensive sana
Brother kwa hapa Tanzania inalimwa wapi zaidi!! Natamani niwatembelee wakulima husika wa Almond nikajifunze nianze nayo kwenye mashamba yangu yenye rutuba.. Maana ile ni non-parishable so nahitaji kujua tu ABC Zake na masoko..
 
Back
Top Bottom