Hatimaye ngoma sasa ni Lowassa vs Magufuli

Hatimaye ngoma sasa ni Lowassa vs Magufuli

watz ni watu very predictable.we already know who is nxt tanzanian president.in kenya its anyones to win,who thot uhuru was going to lead mnths b4 elections?btw will there b a presidential debate in tz like we saw in kenya?
 
Huyo Lowassa si ni hivi majuzi tu aliapa kutoachana na CCM? Ni vipi tena? Yaani huu urais atautafuta kwa udi na uvumba, hata kama ni kwa kulisaliti chama kilichomjenga kisiasa na kuungana na kile ambacho kimekuwa kikimtuhumu yeye kwa ufisadi!

Huyu Lowassa hana jipya kabisa ya kuwapa watanzania, manake nafkiri sera zake hazitatofautiana kabisa na zile za CCM, chama ambacho alikuwa akihudumia hadi hivi majuzi.

Tanzania, hili linasikitisha sana ya kwamba hamna alternative nyingine kabisa. Either ni Magufuli au Magufuli ndiye atakaye kuwa rais.

Hivii sio we we uliesema hapo juu kua Sera za lowasa hazitifautiani na ccm😕 SA Magufuli ni wa chama gani?
 
Hivii sio we we uliesema hapo juu kua Sera za lowasa hazitifautiani na ccm😕 SA Magufuli ni wa chama gani?

Nilimanisha Edward Lowassa anapoteza mda wake tu kukimbilia chama kingine, manake CCMu ina wafuasi wengi zaidi Tanzania.
Hata hivyo, hata akifaulu katika jaribio lake la kupata uongozi, zile zile sera za zamani za CCMu alizozoea ndizo huenda akaziendeleza.
 
Contest of a century really? I think the CCM has the wider edge by far over the oppotision parties.... feel that the CCM is still the most widely supported party in the country.

They're probably already loosing their sleep, now that ED has turned his back on them! (unless it's just for the show, I still can't imagine him VS CCM, you can never trust this pipo)
 
MAGUFULI(ccm) vs LOWASA (ccm) = CCM hawa jamaa wanacheza double game ipo siku tutajua hili.

Na mimi nafikiria hivi, ili kuvutia watu is he really going to speak against CCm?!
 
Contest of a century really? I think the CCM has the wider edge by far over the oppotision parties.
I predict an easy lead for them come October.

If the opposition parties chose to form an alliance to face CCM, I guess they wouldnt even manage to notch up more than the 40% of the votes cast. The CCM will scoop the bigger portion.

I feel that the CCM is still the most widely supported party in the country.

Feel however/whatever/whichever... Lowassa is your President..
 
H

Hakuna anayeweza kuchukua nchi kwa lelemama? Hata JK alikatwa mara ya kwanza na baadae akaomba tena! Sasa kuna shida gani nae Edo akigombea urais? au uroho wa madaraka ni kwa edo tu? Mbona husemi Ndugai hadi kauwa huko !!

Kikwete was patient alisubiri elections zilizofuata. Lowassa ana uchu wa madaraka, nilikuwa namsapoti lkn kwa hili hapana kanitisha na desperation aliyonayo. Chadema nao hawajielewi wanavurugana wenyewe kwa wenyewe, kwa mara ya kwanza nasapoti anachokisema slaa. Hakubaliani na wenzie ila hana ujanja wako greedy km lowassa mwenyewe. October tutamaliza hii kesi. But lowassa and chadema? Hamjitambui
 
Hahahaa anamkubari mtu
La, hasha. Mimi siegemei upande wowote katika siasa zenyu. falcon mombasa
na Ston Merchant, samahani sana, mimi nimedadisi tu haya mambo jinsi ninavyoyaona; simpigii upatu yeyote kwenye kinyang'anyiro hiki. Uamuzi ni wenyu nyinyi wenyewe watanzania.
Wote hawa wana nia njema kwa Tanzania.
 
Last edited by a moderator:
Lowassa atapita tu ukweli upo kwa jinsi anaokubalika ndani na inje ya inchi
 
watz ni watu very predictable.we already know who is nxt tanzanian president.in kenya its anyones to win,who thot uhuru was going to lead mnths b4 elections?btw will there b a presidential debate in tz like we saw in kenya?
It doesnt matter really. As long as their elections will be issues based rather than tribal or clash of personalities angled....this is one area where we Kenyans should observe and learn from our neighbors down south.
 
Contest of a century really? I think the CCM has the wider edge by far over the oppotision parties.
I predict an easy lead for them come October.

If the opposition parties chose to form an alliance to face CCM, I guess they wouldnt even manage to notch up more than the 40% of the votes cast. The CCM will scoop the bigger portion.

I feel that the CCM is still the most widely supported party in the country.
this time opposition can pull up a surprise as looked more organized than CCM and CCM party cadres seemed to have that greatest fear of their political life and very confused! You wait from next week you will understand what i mean some issues are so sensitive to disclose overhere!
 
La, hasha. Mimi siegemei upande wowote katika siasa zenyu. falcon mombasa na Ston Merchant, samahani sana, mimi nimedadisi tu haya mambo jinsi ninavyoyaona; simpigii upatu yeyote kwenye kinyang'anyiro hiki. Uamuzi ni wenyu nyinyi wenyewe watanzania.Wote hawa wana nia njema kwa Tanzania.
Bora yako kuliko MK254 anafuata upepo unakokwenda leo mara magufuli kesho lowasa ujuaji tu
 
Last edited by a moderator:
Sio kushoboka hata kidogo. Kwani si dhahiri hata kwako ya kwamba CCMu ina uungwaji mkono zaidi Tanzania kuliko hivyo vyama vingine?

dogo nani kakwambia CCM ndio inaungwa mkono zaidi tanzania? hiyo ilikuwa zamani sasa na wewe usiwe kama mzee kukaa kufikiria rais bado ni arap moi kumbe rais ni UHURU ,CCM unayozungumzia ni CCM ya enzi zenu huko miaka ya 80's hadi 2000. sasa hivi mkoa mzima wa kigoma CCM wanaviti viwili tu,jiji la mwanza pia CCM wanaviti viwili,ARUSHA,KILIMANJARO,MANYARA na mkoa wa MARA huko CCM hawana chao,jiji la MBEYA msafara wa kikwete umepigwa mawe mara mbili,mikoa ya LINDI na MTWARA huku ni chama cha CUF ,kwanza wakazi wa maeneo haya mara kadhaa wamechoma ofisi na nyumba za watumishi wa serikali kwakuwa wamedhulumiwa gesi,UNGUJA na PEMBA huku ni CUF mpango mzima. mwambie MK254 akutafsirie mrahaba huu.
 
Last edited by a moderator:
Bora yako kuliko MK254 anafuata upepo unakokwenda leo mara magufuli kesho lowasa ujuaji tu

MOTOCHINI Nimekuambia mara nyingi kwamba una ulimbukeni sana kwenye masuala ya siasa. Fahamu mimi na Mkenya mwezangu Iconoclastes tupo tu kama wadadisi na wachambuzi, na wala hatuegemei upande wowote.

Magufuli anafahamika kama mtendaji, pamoja na kwamba alikua kwenye mazingira magumu ndani ya CCM, alifaulu kupenya na kutenda. Na kufikia hadi sasa, hana doa mbali na tetesi kwamba aliuza nyumba fulani. Hivyo ina maana uongozi wake utakua wenye ujasiri na busara. Kuna kipindi alibomoa nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya barabara, hadi akabomoa na za wakwe zake bila kusita. Ni mtu mwenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu bila uwoga.

Lowassa naye, pia anafahamika kama mtendaji, ila yeye alishindwa kubanana na unyang'au ndani ya CCM na akaamua kushuka. Pamoja na kwamba ametajwa kwenye ufisadi wa Richmond, hamna yeyote aliyejitokeza na kumhusisha moja kwa moja. Mwakyembe alitishia kufanya hivyo, lakini akasita baadaye.
Kwa sasa Lowassa ana mashibiki wengi na kuna uwezekano mkubwa kwa yeye kuibuka mshindi kama UKAWA watamkabidhi wadhifa wa kuwania.

Lakini pia patakua na ushindani wa hali ya juu maana Magufuli naye anakubalika sana. Halafu naona Wasukuma wamechangamka na wengi wapo tayari kujitokeza kwa mamilioni kumpigia kura. Japo Tanzania huwa mnadai kutokua na ukabila, lakini mwenyewe najionea na bila kuambiwa. Hata Wamaasai nao wameibuka kwa ajili ya Lowassa wao na hapakaliki.

Mimi binafsi ingelikua napiga kura Tanzania, basi chaguo langu angekua yule mtu wenu wa Kigoma, Zitto Kabwe. Huyo jamaa huwa nampenda sana na kawaida anadhihirisha kuwa na uchungu na nchi. Amepigana na ufisadi sana, halafu anaonekana kuelewa suluhu za matatizo ya Tanzania. Anaogopwa sana na wafisadi. Siku moja nilikua na kikao na wakuu wa idara muhimu sana Bongo, tukiwa kwenye maongezi, kinara wetu akaanza kuhoji mikakati na utendaji wetu na kutuomba tuwe makini sana ili mapungufu yoyote yasimfikie Zitto Kabwe, maana hatakawia kulipua bungeni. Tangu hiyo siku nilianza kumfuatilia kwa karibu bwa Zitto na nimegundua ni mtu muhimu sana kwenye hiyo nchi yenu, ila kwa nyie wafuata mkumbo, hamtaliona hilo.
 
MK254 lowasa anachukua fomu ya urais leo saa tano.leo ngoja nikufumbue macho kidogo "mafisadi wote Tanzania wanatokea kanda ya ziwa " wabongo hawawezi kubisha hili.pia hili li magufuli mimi nilisema toka siku ya kwanza halifai hili lijitu tena nalichukia na nipo tayari kuitwa m'baguzi ni kweli mimi ni mbaguzi lakini hata kabla ya uchaguzi tayari watanzania wameanza kugeuka na kumuwekea magufuli mashaka.magufuli kamaliza bunge bila kujibu ripoti ya CAG ya bilion 263 mali ya watanzania yeye kaila na familia yake.pia anakashfa ya kujengea mahawala hotel (kebby's hotel) hii ipo bamaga karibu na trafic lights ,mkabala na TBC ,kama unaenda mwenge iko upande wa kushoto mita chache baada ya kupita mataa
 
Last edited by a moderator:
MK254 wewe husomeki, leo umekana na kujifanya upo upande wa mbaari kabisa ok lakini, sio leo wewe kufuata upepo unavyo kwenda, Nipende kuwashukuru bwana nimewasili nyumbani TZ salama leo sikuamini maana kenya sasaivi unaish kama upo IRAQ
 
Last edited by a moderator:
MK254 wewe husomeki, leo umekana na kujifanya upo upande wa mbaari kabisa ok lakini, sio leo wewe kufuata upepo unavyo kwenda, Nipende kuwashukuru bwana nimewasili nyumbani TZ salama leo sikuamini maana kenya sasaivi unaish kama upo IRAQ

MOTOCHINI Naomba uwaulize watu kadhaa wakuelimishe kidogo kuhusu nini maana ya "mchambuzi wa siasa", kuanzia hapo ndio utakua tayari kunielewa.

Hongera kwa kurudi kwenu salama, ila kama kawaida ya Watanzania, huwa hamuoni njema popote, mpo watu wa full majungu kwenda mbele. Wewe umekaribishwa Kenya, umekula, kujamba na kunya kwenye vyoo vyetu na unapogeuza na kurudi kwenu, kwa unafiki unaona uongee kuhusu mabaya tu. Aliyewaroga na kuwalaani Watanzania kafia zake mbali na zamani.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom