Hatimaye Muhimbili wameturuhusu kumzika mpendwa wetu!

Unasema mlikuta bill ya 29.9 milion. Na mimi nauliza hivi kwani mtu akitibiwa kwa mfuko wa bima (NHIF) ndugu wanaletewa tena bill mkononi? Ninavyoelewa hizo gharama huwa zinajumlishwa na hospitali husika na kwisha kupelekwa kwa mamla husika ya bima. Huenda kuna kitu nimeshindwa kuelewa.
Pili unadhani kuna mtu hapendi kuwa na bima? asilimia kubwa ya watanzania hawawezi kumudu gharama za kukata hizo bima.
Mkuu pale Muhimbili kabla ya kuchukua mwili unaambiwa uende kwa muhasibu ukaangalie deni lako.

Hivyo muhasibu anakupa bill yote ikiwepo na ile ambayo inalipwa na BIMA hivyo muhasibu atakuelekeza kipi mnatakacholipia na kipi kitalipwa na BIMA hivyo ndio maana unajua kuwa ni jinsi gani BIMA ilivyo na manufaa .

Bima sasa hivi ni nafuu sana kwani kwa TZS 192000/= inatosha kumlipia mtu mmoja hivyo mnajipanga kama familia mnachanga inakuwa helpful kwenu ikitokea ugonjw mkubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu siku 45 ICU ni balaa bora muhimbili, aga khan ni balaa zaidi. ICU sio mchezo aisee. Mzee wangu aga khan bima mlikuwa kwa wiki mnasigin bili ya 4-7M. Nhif walivyogombana na aga khan mzee hata hakuchukua round akafa maana kipindi kile akienda muhimbili au hindu mandal wanamlaza wodi za kawaida
Muhimbili kama hauna bima unaweza kudhani unatibiwa Appolo India,

Two weeks ago mama yangu mkubwa alifariki hapo muhimbili na alilazwa ICU for almost one month and a half , hivyo gharama zilipoletwa ili tulipie kwa ajili ya kuchukua mwili tulikuta bill ya 29.9M ila kwa vile wazazi wetu wote wale waliofikia utu uzima tulikubaliana kama familia tuwakatie bima ya afya.

Hivyo ikawa nafuu zaidi kwetu kwani deni asilimia kubwa lililipwa na NHIF sisi tulilipia gharama za mortuary na kule wodini tulilipa only 90k TZS .

Hivyo tujitahidi wakuu kuwa na bima za afya ili kuepuka usumbufu kama uliomkuta mtoa mada hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa Mada poleni sana lakini mpaka sasa nashindwa kuelewa milioni 40 za nini hasa kwa matibabu yepi hasa Walimwekea moyo,figo na mapafu mengine au?

HUU NI WIZI HAO WEZI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu tunategemea mtoto kama huyo awe na uzalendo kwa nchi yake.Inabidi tubadilike .
 
Nimepata huzini zaidi, nimejipata kwenye maumivu makubwa nikiwa kama baba na mTanzania mwenye maisha ya kawaida na mzazi kama mimi anapo pitia magumu haya.

NAOMBA TUOMBE.....
Tunakushukuru Mungu wetu kwa upendo wako kwetu,tangu tulipoamka hata sasa u pamoja nasi,
Umetulinda tulipotoka hata kurudi kwetu.
Tunakushukuru Mungu wetu na tunakurudishia heshima na utukufu.
Tunaomba toba kwa mambo yote tuliyotenda kinyume na mapenzi yako,tunaomba ututakase kwa Damu ya Yesu Kristo.
Ni usiku mwingine tena Baba tunaomba ulinzi wako,sawa na zaburi 127:1.kwani
Ulinzi wetu si chochote pasipo Wewe Mungu wetu.
Tuepushe na mipango yote ya adui yetu na wafuasi wake wote,
Tunanyamazisha kimya kila roho ya malipizi na watesi wetu,kwa jina la Yesu krito.....
Na wote tuseme.... Amen


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoto wa umri huo anajipikia baada ya kushinda njaa shule,wazazi wameachana na mama anafanya biashara ndogondogo Mbezi stand.Tatizo msingi wake uko hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo sio tatizo mkuu. Hayo ni maisha yetu ya kila siku.

Tatizo, ni kudaiwa milioni 40 kuuchukua mwili wa marehemu.

Soma mwanzo utaelewa.

Kuachana mke na mume, haya ya kila siku tumeyazoea, labda ungeanziasha uzi, utufundishe jinsi ya kuishi kwenye ndoa, lakini huu uzi una maudhui yake.
 
Hilo sio tatizo mkuu. Hayo ni maisha yetu ya kila siku.

Tatizo, ni kudaiwa milioni 40 kuuchukua mwili wa marehemu.

Soma mwanzo utaelewa.

Kuachana mke na mume, haya ya kila siku tumeyazoea, labda ungeanziasha uzi, utufundishe jinsi ya kuishi kwenye ndoa, lakini huu uzi una maudhui yake.
Kama wazazi wangeweka mzingira mazuri kwa mtoto hayo yasingetokea mkuu.Naangalia tulipo jikwaa siyo tulipoangukia mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wazazi wangeweka mzingira mazuri kwa mtoto hayo yasingetokea mkuu.Naangalia tulipo jikwaa siyo tulipoangukia mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ikiwa kwako uko vizuri, haimaanishi kila mtu yuko kama wewe. Tanzania ina masikini wengi na hata hao matajiri wachache sio wote wanaweza kumudu gharama za matibabu Tanzania hii.

Hiyo Bima yenyewe ni wizi mtupu unaofanyika, Wewe unaongelea maisha ya watu.

Maisha ya kila mtu hayawezi kufanana, na tabia za watu haziwezi kufanana.

Hukiyapatia shukuru, ni bahati kati ya wengi ambao yanawashinda.
 
Tulihangaika kwa madaktari tuliowajua watusaidie bila mafanikio mpaka baba aliomba kumuona Mkurugenzi wa Muhimbili bila mafanikio. Jana Jumatano aliambiwa alipe 2.5 million ili apewa mwili na pesa itakayobaki ailipe kwa awamu.
Salaam!

Wadau mtakumbuka wakati nikichangia uzi wa mdau mmoja juzi uliohusiana na Muhimbili hospital nilieleza kisa cha binti wa darasa la tatu kuungua moto na baada ya kufariki wazazi waliambiwa wanatakiwa kulipa milioni 40 zilizotokana na matibabu ndipo waweze kupewa mwili.

Binti huyu wa darasa la tatu aliyekuwa akisoma Shule ya Msingi Mshikamano iliyoko Mbezi Msakuzi kata ya Mbezi alikuwa akiishi na mama yake baada ya kutengana na baba. Mwezi June mwaka huu mida ya saa kumi na mbili jioni akiwa anapika nguo aliyovaa ilishika moto na kupelekea kuungua na muda huo mama yake anayefanya biashara ndogo ndogo stendi ya Mbezi Mwisho alikuwa hajarudi.

Binti alikimbia nje akipiga kelele ndipo majirani walipommwagia maji na baadae kumkimbiza zahanati ya mmezi, baada ya kufika zahanati ya Mbezi wauguzi walipomuona walisema ameungua sana hawawezi kumtibu apelekwe hospital ya Sinza Palestana lakini baada ya kufika nao walisema apelekwe Mwananyamala kwamba hawawezi kumtibu, cha kusikitisha Mwananyamala pia walisema apelekwe Muhimbili.

Tufahamu binti huyu aliungua saa 12 jioni fikiria foleni za kutoka Mbezi na mizunguko yote hiyo mpaka kufika Muhimbili mtoto hajapata matibabu zaidi ya maji na mchanga aliomwagiwa.

Kwa kipindi chote toka June mpaka sasa alikuwa amelazwa akiuguzwa na mama yake. Jumatatu ya wiki hii asubuhi binti yetu alifariki ndipo mama na baba yake walipoanza kufuatilia taratibu za kuuhifadhi mwili na mambo mengine.

HUZUNI YAZIDI
Baba alipewa bill milioni 40 ndio angepewa mwili, hapo ndipo alipochanganyikiwa. Kama nilivyoeleza hapo juu wazazi hawa walitengana kwa hiyo wakati mtoto anaumwa waliungana kumuuguza. Baada ya kuambiwa kiasi anachotakiwa kulipa alijaribu kuomba kupunguziwa bila mafanikio.

Tulihangaika kwa madaktari tuliowajua watusaidie bila mafanikio mpaka baba aliomba kumuona Mkurugenzi wa Muhimbili bila mafanikio. Jana Jumatano aliambiwa alipe 2.5 million ili apewa mwili na pesa itakayobaki ailipe kwa awamu.

Hivyo majirani tulichangishana na ndugu ikapatikana pesa ya kulipa na aandike barua na aache vitambulisho atakapomaliza deni ndio atapewa vitambulisho vyake, Hivi kweli mwananchi wa kawaida milion 40 anapata wapi? Kibaya zaidi mtoto amefariki halafu mnamtaka mzazi alipe pesa yote hiyo?

Muhimbili mmetuumiza sana kushikilia mwili wa binti yetu tangu Jumatatu kisa kulipa 40 milioni ni uhuni sana!
Ingawa tunashukuru kwenda kumpumzisha mpendwa wetu lakini mmetuhuzunisha sana kama nyie million 40 mnazo mtambuee watu wengine hawana.


Sent using Jamii Forums mobile app

Jr
 
Ikiwa kwako uko vizuri, haimaanishi kila mtu yuko kama wewe. Tanzania ina masikini wengi na hata hao matajiri wachache sio wote wanaweza kumudu gharama za matibabu Tanzania hii.

Hiyo Bima yenyewe ni wizi mtupu unaofanyika, Wewe unaongelea maisha ya watu.

Maisha ya kila mtu hayawezi kufanana, na tabia za watu haziwezi kufanana.

Hukiyapatia shukuru, ni bahati kati ya wengi ambao yanawashinda.
Sijaongelea bima wala kuwa na tabia nzuri.Kumbuka mtoto hakuumwa ugonjwa wowote bali ajali ya moto na mimi naongelea chanzo cha ajali ya moto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom