Hatimaye 'mtemi' Jecha Salim Jecha ang'atuka

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,698
Reaction score
2,262
Jecha Salum.jpg

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha amemaliza muda wake wa majukumu ya tume hiyo kwa kipindi cha miaka mitano kilichoanzia Aprili 30,2 013 hadi Aprili 29, 2018 ambapo yeye na wajumbe wa tume hiyo wamekabidhi ripoti yao ya kazi.

Akitoa taarifa yake kwa Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Jecha amesema kuwa tume inaamini kwamba, mafanikio yaliyopatikana wakati wa utekelezaji wa majukumu yake hasa ya kiuchaguzi yalitokana na ushirikiano wa wadau mbalimbali na wananchi kwa jumla.

"Ndani ya miaka mitano tume imeweza kuendesha jumla ya chaguzi ndogo nne, zikiwemo chaguzi ndogo tatu za Udiwani na chaguzi moja ya uwakilishi pamoja na kusimamia uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25,2015 na ule wa marudio yake Machi 20, 2016. Tume imefanya mapitio ya majimbo ya uchaguzi na kubadilisha mipaka ya majimbo ya uchaguzi, majina ya majimbo na kuongeza idadi ya majimbo kutoka 50 hadi 54", ameeleza Jecha.

Pamoja na hayo, Jecha ameendelea kwa kusema "Tume imeweza kufanya uandikishaji wa wapiga kura kwa awamu mbili na kuliendeleza daftari la kudumu la wapiga kura sambamba na kuendesha programu mbalimbali za elimu ya wapiga kura kupitia vyombo vya habari, mikutano ya wadau, uchapishaji wa vipeperushi, majarida na makala mbalimbali".

Aidha, Mwenyekiti huyo amemueleza Dkt. Shein kuwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imechaguliwa kuwa kiongozi wa Uchaguzi Mkuu wa nchini Congo utakaofanyika mwezi Disemba mwaka huu.

Kwa upande wake, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein ameipongeza Tume hiyo kwa kutekeleza vyema majukumu yake ndani ya miaka mitano kwa kuendesha chaguzi zote .

"Tume hii inastahiki pongezi kwa kuifanikisha vyema kazi waliyopewa ikiwa ni pamoja na kuendesha chaguzi zote ukiwemo uchaguzi Mkuu, chaguzi ndogo na ule uchaguzi wa marudio ambazo zote hizo zilifanywa kwa ufanisi mkubwa", amesema Dkt. Shein.

Wajumbe wa tume hiyo ambao wamemaliza muda wao ni Mwenyekiti mwenyewe Jecha Salim Jecha, Jaji Abdul-hakim Ameir Issa, Balozi Omar Ramadhan Mapuri, Nassor Khamis Mohammed, Ayoub Bakari Hamad, Haji Ramadhan Haji na Salmin Senga Salmin ambao wote hao waliapishwa rasmi Mei,4, 2013.

Chanzo: EATV

Je utamkumbuka huyu jamaa kwa lipi maishani mwako?

Soma: Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu
 
Jk haloo mzee mkapa mzee salama nipe ripoti za uchaguzi jk huko zenji mambo mazito bwm sawa nipe nusu saa mkapa huyo zenji ndani ya zec mzee jecha vipi huku kukoje? jecha hali siyo kabisa mkapa pumbavu kabisa ina maana hujui cha kufanya futa uchaguzi haraka jecha sawa mkapa jk na wewe ni lofa kabisa huko mwanza kuna mtoto kagoma kusaini ngoja na huko niende nchi hii haikupatikana kwa makaratasi
 
Kwani katiba hairuhusu huyu Mzee wetu kupewa kiindi chengine? Kama inakubalika itapendeza kama atapewa kipindi kingine cha kuongoza hiyo tume ya uchaguzi.
 
Aende tu kwakweli! Watu hawatomsahau kwa kuwadhulumu wazanzibar, ni kama yule farao mbaya!
 
Kwani katiba hairuhusu huyu Mzee wetu kupewa kiindi chengine? Kama inakubalika itapendeza kama atapewa kipindi kingine cha kuongoza hiyo tume ya uchaguzi.
Sijui mkuu. Naamini ikimpendeza mh Rais Dr Shein atamtafutia kanafasi kengine
 
Kifo nakikubali sana.
Huwa hakiangalii cheo
Kikimzonga mtu anakuwa mpole
Anakuwa mzito hajiwezi tena
Ndipo matendo ya mtu hutangulia mbele.
Note: Jamani tufanye yote ila tukumbuke kifo.
Natania tu
 
Kibaraka huyu!

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha amemaliza muda wake wa majukumu ya tume hiyo kwa kipindi cha miaka mitano kilichoanzia Aprili 30,2 013 hadi Aprili 29, 2018 ambapo yeye na wajumbe wa tume hiyo wamekabidhi ripoti yao ya kazi.

Akitoa taarifa yake kwa Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Jecha amesema kuwa tume inaamini kwamba, mafanikio yaliyopatikana wakati wa utekelezaji wa majukumu yake hasa ya kiuchaguzi yalitokana na ushirikiano wa wadau mbalimbali na wananchi kwa jumla.

"Ndani ya miaka mitano tume imeweza kuendesha jumla ya chaguzi ndogo nne, zikiwemo chaguzi ndogo tatu za Udiwani na chaguzi moja ya uwakilishi pamoja na kusimamia uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25,2015 na ule wa marudio yake Machi 20, 2016. Tume imefanya mapitio ya majimbo ya uchaguzi na kubadilisha mipaka ya majimbo ya uchaguzi, majina ya majimbo na kuongeza idadi ya majimbo kutoka 50 hadi 54", ameeleza Jecha.

Pamoja na hayo, Jecha ameendelea kwa kusema "Tume imeweza kufanya uandikishaji wa wapiga kura kwa awamu mbili na kuliendeleza daftari la kudumu la wapiga kura sambamba na kuendesha programu mbalimbali za elimu ya wapiga kura kupitia vyombo vya habari, mikutano ya wadau, uchapishaji wa vipeperushi, majarida na makala mbalimbali".

Aidha, Mwenyekiti huyo amemueleza Dkt. Shein kuwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imechaguliwa kuwa kiongozi wa Uchaguzi Mkuu wa nchini Congo utakaofanyika mwezi Disemba mwaka huu.

Kwa upande wake, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein ameipongeza Tume hiyo kwa kutekeleza vyema majukumu yake ndani ya miaka mitano kwa kuendesha chaguzi zote .

"Tume hii inastahiki pongezi kwa kuifanikisha vyema kazi waliyopewa ikiwa ni pamoja na kuendesha chaguzi zote ukiwemo uchaguzi Mkuu, chaguzi ndogo na ule uchaguzi wa marudio ambazo zote hizo zilifanywa kwa ufanisi mkubwa", amesema Dkt. Shein.

Wajumbe wa tume hiyo ambao wamemaliza muda wao ni Mwenyekiti mwenyewe Jecha Salim Jecha, Jaji Abdul-hakim Ameir Issa, Balozi Omar Ramadhan Mapuri, Nassor Khamis Mohammed, Ayoub Bakari Hamad, Haji Ramadhan Haji na Salmin Senga Salmin ambao wote hao waliapishwa rasmi Mei,4, 2013.

Chanzo: EATV

Je utamkumbuka huyu jamaa kwa lipi maishani mwako?

Soma: Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu
 
Dhuluma aliyoifanya 2015 lazima malipo yake ayapate hapa hapa duniani!
 
Back
Top Bottom