Hatimaye Mo Dewji anamalizia mwaka kwa azimio la kutowavumilia wanaomtolea lugha za matusi kwenye mitandao ya kijamii kwa mwaka 2021

Bongo ukiwa na pesa unakuwa na maadui wengi Sana hasa sisi akina kapuku .Maana tuna hasira ya maisha ,Mo katutoa kwenye hatua moja kwenda nyingine .Mapungufu hayakosekani ,mkitaka mtu perfect hamuwezi mpata kamwe.Tuendelee kuvumiliana na kudai hayo Mapungufu katika namna nzur na sio kejeli.
 
kwa nini billionea mzima anapoteza muda na nguvu zake kwenye mitandao kuchambana kama kina mwajuma ndala ndefu?
Kuchambana ?
MO kamtukana nani ?

Kuandika katika mtandao kila mtu ana uhuru wake.
Hakuna sheria yoyote inayesema Billionea asiwe anaandika maoni yake kwenye mtandao.
Hapa kinachosemwa ni kumtukana mtu bila sababu na ni kosa la kimtandao.

Kama unaona anastahili kutukanwa basi mtukane.
 
....Mikwara Mbuzi tu hiyo! Alipe Bilioni anazodaiwa ununuzi feki was timu yetu a one kama Luna MTU atakuwa na shughuli naye!

Hivi sisi Watanzania ama Waafrika tumerogwa?
MTU anatoka chumbani kwake na kutangaza kununua litimu letu likubwa, halipi hela anayotakiwa kulipa lakini anakabidhiwa litimu loote na kulifanya apendavyo!
Tuna akilii, matope?
Yaan wakisikia hv wanaweza kukumeza. Yaan nimekuja kugunduaga hawa kanjibahi shida sana
 
....Baasi! Hapo hapo! Ndio zinamtia Kiwewe! Wenye timu yao wanapohoji, atasema in matusi? Ni Kashfa???
Nimemsoma Mo huwa anapenda sana sympathy. Anapenda sana kuplay victim akiulizwa hayo maswali ya msingi. Anapanic vibaya mno. Myu hajaweka hela kama mkataba usemavyo. Anafanya ajisikiavyo halaf akihojiwa ndo mpaka na press. Sipendi hii tabia.
 
Tatizo ni zile bilioni 20 anazodaiwa na Simba SC!
Hivi ni kwann akiilizwaga kuhusu hizi hela anakuaga mkali kama pilipili? Yaan maruhani na mizimu yote inaamka. Na anaanzisha drammar hapohapo. Sasa ile ishu yake na kigwa mambo ya pikipiki yanagusiana nn na mpira. Yaan Mo is very weak. Tuache kusema sijui maskin tuna wivu na blah blah. Maswali ya msingi yanapohojiwa yajibiwe kwa hoja. Si kuanza kutafuta visingizio. Honestly sijawahi ona hayo matusi zaidi ya utani na kuulizwa iko wapi biriwoni 20 ya simbaa
 
Kuchambana ?
MO kamtukana nani ?

Kuandika katika mtandao kila mtu ana uhuru wake.
Hakuna sheria yoyote inayesema Billionea asiwe anaandika maoni yake kwenye mtandao.
Hapa kinachosemwa ni kumtukana mtu bila sababu na ni kosa la kimtandao.

Kama unaona anastahili kutukanwa basi mtukane.
vijana wa mudi mna jazba sana.
unamjua nani ambaye ameshawahi kumtukana huyo mudi?
 
Aiseh..!
Mi sikuwa nafaham hilo jina.

Uliangalia kichekesho cha Joti nini.
Maana alimpa majina kama matatu hivi ya kumtania
Muhammed, Mwamedi, na Mudy.
Mohamed wote ni Mudi.
cha msingi bilionea wenu asipoteze muda wake kusoma comments za watu wanaotumia majina feki mitandaoni hawana cha kupoteza wale.
 
Aiseh..!
Mi sikuwa nafaham hilo jina.

Uliangalia kichekesho cha Joti nini.
Maana alimpa majina kama matatu hivi ya kumtania
Muhammed, Mwamedi, na Mudy.
mkuu nisamehe, niliamini unajua Mudi ni nani ila unajitoa ufahamu. Mohamed huku uswazi huwa yamefupishwa hivyo kabisa na ni kawaida wala si matusi wala dhihaka. Mbona wapo wengi sana mtaani wanaitwa hivyo?
 
Mohamed wote ni Mudi.
cha msingi bilionea wenu asipoteze muda wake kusoma comments za watu wanaotumia majina feki mitandaoni hawana cha kupoteza wale.
Ishu ni kwamba hataki kutukanwa na Katoa tahadhari.
Sasa kama mtu anaona amejificha ktk fake ID na anaona yuko salama na anataka kumtukana basi kitakacho mkuta aridhike nacho.
Asije akalalamika kuwa ameonewa.
 
Back
Top Bottom