Hatimaye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ahamishwa

Hatimaye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ahamishwa

Hivi Makonda hakuliona hili jipu au alibariki, angoje zamu yake ya kutumbuliwa.
 
Injinia Mussa Natty msimamizi wa uchaguzi aliyesimama kidete kupambana na uchakachuaji na alisimamia haki katika wilaya ya kinondoni katika uchaguzi uliopita. Kitendo cha kuahirisha Jana kikao cha madiwani mpaka suala tata LA viti maalumu lipate ufumbuzi limewakasilisha wengi.
 
Kinondoni kushirikiana na Benki ya TIB ndio wameandaa michoro inayoonyesha namna ufukwe huo utakavyokuwa baada ya kutengenezwa.
Ok! Sasa kinondoni na tib watafanya huo mradi ..ndiyo Manji mwenyewe atafanya
Mpk sasa haeleweki nani ndy ana right hapo
 
yaani wadau me nawaambia hivi alilmashauri nyingi nchini zimeoza hasahasa za majiji kuanzia wakurugenzi mpaka watu wanao jihita wakuu wa idara wana wasumbua sana wafanya kazi sasa magufuli kama ameamua aka safishe almashauri zote akianzia na Mwanza(jijini) watu wanao jihita wakuu wa idara wote hawa fai kabisa washajijengea usugu ubabe dhidi ya wanyakazi wa kawaida pamoja na kuwa na watu wake wanao watumia kuvuja hela za serikal kwa matakwa yao hawa watu wahamishwe au wapigwe chini wote hawafai kabisa hawa watu na almashauri nyingi ndipo pesa nyingi zinakopotelea tunaomba muheshimiwa atuokoe kwa hilo hawa watu wanao jihita wakuu wa idara hawafai kabisa
 
mkichunguza vizuri kwenye mchoro hinayo onyeshwa kwenye tv mtagundua sehemu ya watu wa kawaida ni kama korongo vile,
 
Penye Ukweli uongo hujitenga. Yusuph Manji alikabidhi kwa Mh. Rais Magufuli mikataba yote aliyoingia na Manispaa ya Kinondoni kwenye Uendelezaji wa Ufukwe wa Coco sasa ukweli umeanza kudhihiri hapakuwa na kipengele cha Kuuzwa Fukwe wala kuzuia Watu wa "Manzese" kuogelea, waliompotosha Mh. Rais walikosea

Lakini huo usamaria wa manji kuwatengeneźea walala hoi coco beach umetoka wapi? Hivi unaamini kweli manji anaweza kutumia mabilion ya fedha zake bila kuwa na uhakika zitarudije? Mimi siamini.
 
Penye Ukweli uongo hujitenga. Yusuph Manji alikabidhi kwa Mh. Rais Magufuli mikataba yote aliyoingia na Manispaa ya Kinondoni kwenye Uendelezaji wa Ufukwe wa Coco sasa ukweli umeanza kudhihiri hapakuwa na kipengele cha Kuuzwa Fukwe wala kuzuia Watu wa "Manzese" kuogelea, waliompotosha Mh. Rais walikosea
ndiyo madhara ya kumeza kilakitu
 
attachment.php

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty amehamishwa. Bado haijajulikana sababu ya kuhamishwa kwake.

Hivi karibuni kumeibuka taarifa katika vyombo mbali mbali vya habari kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeuza Ufukwe wa Oysterbay (Coco Beach) kwa Kampuni ya Q-Consult, ambayo baadae ilikuja ikanyang'anywa kwamba imechelewa kuendeleza sehemu hiyo.
Sasa nasikia wamepewa matajiri wengine.

Ufukwe wa Oysterbay unaanzia katika eneo la Police Officers Mess hadi Barabara ya Kenyatta, upande wa Mashariki wa Barabara ya Toure. ambapo ndani ya ufukwe huo kuna eneo maarufu linaloitwa Coco Beach.

Kwa muda mrefu sana, ufukwe huo umekuwa ukitumiwa na wananchi wengi wa Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kujipumzisha, kuogelea na wakati mwingine kufanyia mazoezi ya viungo ikiwamo mazoezi ya kutembea.

Hii hali ya Kuuzwa kwa Coco beach imezua sintofahamu nchini.

Stay tuned..

Ni uhamisho wa kawaida tu, wakurugenzi wengi wamehamishwa vituo vyao ili kuboresha utendaji, haihusiani na coco beach
 
Kastaafu? Meya aliyepita hana uwezekano wa kurudia nafasi yake kwani UKAWA ndo wenye madiwani wengi katika Manispaa ya Kinondoni. BTW, kwani meya wa zamani alishinda kiti chake cha udiwani?

Ukiwa na madiwani wengi ni lazima Meya atoke kundi lako?
 
Kwa hiyo anataka kuendeleza fukwe kama sadaka au? Tusifanyane watoto hiyo project inagharimu kiasi gani na hiyo hela atairudishaje?

Ufukweni hamwendi na bidhaa zenu, mtanunua za kwake!
 
Mchakato wa manji na kinondoni ulianza 2009.... sidhani kama Musa aliisha kuwa Mkurugenzi.... ni vizuri kuto weka hisia na kuleta mada bila kuwa na uhakika.... maana jana ilikiwa ufanyike uchaguzi wa meya kinondoni.... ilishindikana maana ukawa walidai kuna wabunge wa viti maalum ccm toka zenj walikuwemo kupiga kura na musa alionekana akisema ameomba mwongozo kwa wakubwa ili kujua kama huo utaratibu ni sawa na kuahirisha uchaguzi.... yawezekana imewaudhi wakubwa.... ni vema kuwa na uhakika kabla ya kumjadili mtu... jiweke mwenyewe kwenye nafasi yake na fikiria kama kinacho semwa kitakuwa si kweli.... kama ni kweli basi ni vema ila naona mleta mada hana uhakika...
 
Ukiwa na madiwani wengi ni lazima Meya atoke kundi lako?

Meya asipotoka kundi lenye madiwani wengi katika halmashauri husika, LAZIMA ujiulize sana. Huenda hao madiwani ni mamluki ama wamepandikizwa (uchaguzi ulioahirishwa jana refers)!
 
attachment.php

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty amehamishwa. Bado haijajulikana sababu ya kuhamishwa kwake.

Hivi karibuni kumeibuka taarifa katika vyombo mbali mbali vya habari kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeuza Ufukwe wa Oysterbay (Coco Beach) kwa Kampuni ya Q-Consult, ambayo baadae ilikuja ikanyang'anywa kwamba imechelewa kuendeleza sehemu hiyo.
Sasa nasikia wamepewa matajiri wengine.

Ufukwe wa Oysterbay unaanzia katika eneo la Police Officers Mess hadi Barabara ya Kenyatta, upande wa Mashariki wa Barabara ya Toure. ambapo ndani ya ufukwe huo kuna eneo maarufu linaloitwa Coco Beach.

Kwa muda mrefu sana, ufukwe huo umekuwa ukitumiwa na wananchi wengi wa Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kujipumzisha, kuogelea na wakati mwingine kufanyia mazoezi ya viungo ikiwamo mazoezi ya kutembea.

Hii hali ya Kuuzwa kwa Coco beach imezua sintofahamu nchini.

Stay tuned..

..ninyi mliomtukana na kumlaumu sana Manji someni kwa makini uzi huu hapo nilipowawekea rangi nyekundu kisha mjiulize Manji kakosa nini? ? kama Manji ataachana na ufukwe kama ambavyo wengi mmekuwa mkitaka afanye, nini maoni yenu juu ya adhma na manispaa ya kinondoni kuwapa matajiri wengine ufukwe huo ? ?tumia busara siyo kuropoka tu

Kama huyu mkurugenzi amehamishwa tu bila kutumbuliwa je hakuwa jipu au serikali inabifu endelevu na manji?
 
Nimesoma sehemu kua kapelekwa BABATI
 
Kwa hiyo anataka kuendeleza fukwe kama sadaka au? Tusifanyane watoto hiyo project inagharimu kiasi gani na hiyo hela atairudishaje?

Mkuu unajua kuna watu wanafikiri wana akili kubwa kumbe hazijali hata kwenye kizibo cha soda! Mtu ataendeleza ufukwe tu kama sadaka? Huyo jamaa ni mother of corruption in Tanzania na kazi yake ni kuhonga fedha ndefu ili apewe raslimali za nchi hii kwa bei ya chee! Halafu anakingiwa kifua na huyu mzee wa Msoga aliyemaliza ungwe na mtoto wake.
 
Back
Top Bottom