Hatimaye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ahamishwa

Hatimaye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ahamishwa

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,059
Reaction score
64,209
attachment.php

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty amehamishwa. Bado haijajulikana sababu ya kuhamishwa kwake.

Hivi karibuni kumeibuka taarifa katika vyombo mbali mbali vya habari kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeuza Ufukwe wa Oysterbay (Coco Beach) kwa Kampuni ya Q-Consult, ambayo baadae ilikuja ikanyang'anywa kwamba imechelewa kuendeleza sehemu hiyo.
Sasa nasikia wamepewa matajiri wengine.

Ufukwe wa Oysterbay unaanzia katika eneo la Police Officers Mess hadi Barabara ya Kenyatta, upande wa Mashariki wa Barabara ya Toure. ambapo ndani ya ufukwe huo kuna eneo maarufu linaloitwa Coco Beach.

Kwa muda mrefu sana, ufukwe huo umekuwa ukitumiwa na wananchi wengi wa Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kujipumzisha, kuogelea na wakati mwingine kufanyia mazoezi ya viungo ikiwamo mazoezi ya kutembea.

Hii hali ya Kuuzwa kwa Coco beach imezua sintofahamu nchini.

Stay tuned..

===========

Update:


DSC09883.jpg
 

Attachments

  • 12345576_891975167577166_1688588680665240964_n.jpg
    12345576_891975167577166_1688588680665240964_n.jpg
    9 KB · Views: 15,909
Na kuna mwingine ni kijan tu bado ila nimepata taarifa nyeti sana
kuwa eti kastaafu umeya wa Kinondoni. Mie nikabaki kinywa wazi,
meya kijana kama yule ana staafu wakati katoka kuwa meya bora afrika..
 
Na kuna mwingine ni kijan tu bado ila nimepata taarifa nyeti sana
kuwa eti kastaafu umeya wa Kinondoni. Mie nikabaki kinywa wazi,
meya kijana kama yule ana staafu wakati katoka kuwa meya bora afrika..

Kastaafu? Meya aliyepita hana uwezekano wa kurudia nafasi yake kwani UKAWA ndo wenye madiwani wengi katika Manispaa ya Kinondoni. BTW, kwani meya wa zamani alishinda kiti chake cha udiwani?
 
Magufuli alisema ukiharibu hakuna kuhamishwa.... ni KUFUKUZWA TU...

NAKATA nione hilo 😨👉🚶🚶🚶
 
Penye Ukweli uongo hujitenga. Yusuph Manji alikabidhi kwa Mh. Rais Magufuli mikataba yote aliyoingia na Manispaa ya Kinondoni kwenye Uendelezaji wa Ufukwe wa Coco sasa ukweli umeanza kudhihiri hapakuwa na kipengele cha Kuuzwa Fukwe wala kuzuia Watu wa "Manzese" kuogelea, waliompotosha Mh. Rais walikosea
 
Jana saa tatu usiku kulikuwa na kipindi kipindi maalum itv, tanzania invest bank walikuwa wanazungumzia mradi huo wa coco beach

Ovaaaa
 
magufuli umeanza kutuangusha....hamisha haisadii kitu.inatakiwa ukamate,pekeka mahakani,funga.
 
Hamna kitu hapo.Serikali ya awamu ya tano ilikuwa effective kwa siku 32 tu za mwanzo..baada ya halmashauri kuu ya CCM serikali imebadilika na wapinzani sasa tunaanza kuipinga mwanzoni tuliikubali lakini sasa mmhhh
 
Magufuli alisema yeye haamishi atafukuza, sasa huu mwanzo anaotuonesha naelekea kumjumuisha katika wasemaji na sio watendaji.
 
Jana saa tatu usiku kulikuwa na kipindi kipindi maalum itv, tanzania invest bank walikuwa wanazungumzia mradi huo wa coco beach

Ovaaaa

Kinondoni kushirikiana na Benki ya TIB ndio wameandaa michoro inayoonyesha namna ufukwe huo utakavyokuwa baada ya kutengenezwa.
 
Penye Ukweli uongo hujitenga. Yusuph Manji alikabidhi kwa Mh. Rais Magufuli mikataba yote aliyoingia na Manispaa ya Kinondoni kwenye Uendelezaji wa Ufukwe wa Coco sasa ukweli umeanza kudhihiri hapakuwa na kipengele cha Kuuzwa Fukwe wala kuzuia Watu wa "Manzese" kuogelea, waliompotosha Mh. Rais walikosea

Kwa hiyo anataka kuendeleza fukwe kama sadaka au? Tusifanyane watoto hiyo project inagharimu kiasi gani na hiyo hela atairudishaje?
 
Magufuli alisema ukiharibu hakuna kuhamishwa.... ni KUFUKUZWA TU...

NAKATA nione hilo 

Ndo na mimi nashangaa hapa, naye sasa kaanza kuhamisha hamisha tu badala ya kumchukulia hatua za kinidhamu?! au kuhamisha nako ni hatua ya kinidhamu mi ndo sijui tu
 
Kwa hiyo anataka kuendeleza fukwe kama sadaka au? Tusifanyane watoto hiyo project inagharimu kiasi gani na hiyo hela atairudishaje?

Badala ya kuuliza kwa Adabu ueleweshwe unaanza kejeli ya eti tusifanyane watoto? Tembelea Kijiji Beach au South beach kigamboni ujue wanarudishaje Fedha zao bila ya kuzuia watu ku access Beach!!!
 
Badala ya kuuliza kwa Adabu ueleweshwe unaanza kejeli ya eti tusifanyane watoto? Tembelea Kijiji Beach au South beach kigamboni ujue wanarudishaje Fedha zao bila ya kuzuia watu ku access Beach!!!

Hakuna cha kueleweshwa hapo... Coco beach ibaki kama ilivyo, huu ujanja ujanja hatuuhitaji kwa sasa... Kijiji beach na south beach sihitaji kutembelea ndio nyumbani na ni tofauti kabisa na coco beach
 
Penye Ukweli uongo hujitenga. Yusuph Manji alikabidhi kwa Mh. Rais Magufuli mikataba yote aliyoingia na Manispaa ya Kinondoni kwenye Uendelezaji wa Ufukwe wa Coco sasa ukweli umeanza kudhihiri hapakuwa na kipengele cha Kuuzwa Fukwe wala kuzuia Watu wa "Manzese" kuogelea, waliompotosha Mh. Rais walikosea

Ndugu fafanua.

Huyo Manji ataendeleza kivipi ilhali awaruhusu watu wa Manzese kwa Mfuga mbwa kuingia na kupunga upepo????


Miaka ya awali tulikuwa na uwezo wa kutembea bahari kwa bahari toka Mbezi Beach na kufika Msasani Cine Club. Lakini leo huwezi kwani watu binafsi wamejibinasisha zile eneo zote.

Tembelea Fukwe za Kigamboni utakuta watu wamejibinasisha maeneo na ukitaka kuingia unalipa kiingilio cha Tsh. 1,000/= hadi 2,000/=

je, tueleze manji alikuwa anataka kuendeleza kivipi??? Hatumuelewi bado!!!
 
Back
Top Bottom