Hatimaye Lady Jay Dee Afanikiwa Kupanda Mlima Kilimanjaro

Hatimaye Lady Jay Dee Afanikiwa Kupanda Mlima Kilimanjaro

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,154
Reaction score
13,267
E86A2244.JPG
Huyu ndiye mumewe Lady Jaydee aliyemuongoza hadi kileleni mwa Mlima Kilimanjaro


MS
ANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura maarufu kwa jina la Lady Jay Dee, jana alifanikiwa kukamilisha ziara yake ya sikusita ya kupanda mlima Kilimanjaro, ikiwa na lengo la kutangaza mlima huo na kujionea upekee wa kivutio hicho.

Katika ziara hiyo iliyodhaminiwa na shirika la hifadhi za taifa nchini (TANAPA), msanii huyo aliyeambatana na mumewe ambaye ndiye anesimamia kazi zake, Gadna Habash, waliwasili kwenye lango kuu la Marangu saa 12 jioni na kupokelewa na mhifadhi mkuu wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro (KINAPA), Erastus Lufungulo.

Msafara wa Jay Dee ulianza safari ya kupanda mlima Kilimanjaro Januari 8 na kufanikiwa kufika katika kilele chake chenye urefu wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mara baada ya kushuka mlimani, Jay Dee, alisema ziara hiyo imetoa mafunzo makubwakwao na wakatoa wito kwa wasanii, waandishi wa habari na watangazaji nchini, kutembelea vivutio hivyo ili kufahamu yale wanayozungumza kuhusu hifadhi hizo.

"Ziara hii imenipa mwanga kama msanii, nimejifunza mengi na niwakumbushe tu wasanii wenzangu kuchukulia zoezi la kupanda la
kupanda mlima Kilimanjaro kama moja ya majukumu na wajibu wao kama wananchi wa taifa hili," alisema Jide.

Kwa upande wake mhifadhi wa KINAPA Lufungulo ametoa rai kwa wadau wote hasa wananchi wa kawaida kushiriki kupanda mlima huo, kwa lengo la kukuza utalii wa ndani

 
E86A2236.JPG
akikabidhiwa Golden Certificate kwa KUFIKA KILELENI
 
Jamani kupanda Raha sana, kama kuna anayehitaji na mimi nimfikishe kileleni ani pm, maana nilifika tangu mwaka 2008...nitakueleza mbinu rahisi za kufika, lakini lazima utomase sana
 
Aaaaaaaaaaahhhhhhhhh, MKUU VIPI TENA? AMA KWELI uHAMASISHAJI WA UTALII WA NDANI UNAHITAJIKA SANA...........
Lady jay dee ni mwanamke, mumewe ni mwanaume. Unaposema kafikishwa kileleni unamaanisha nini mkuu? unamaanisha kilele gani?
 
Afikishwa kileleni ........................, jamani!!!!
 
Unajua tatizo mmezoe sana mada za Mbuzi Mzee, unajua you must lead a horse to water, drinking is another business but your part is done................
Duuh.. Kichwa cha habari kilinistua nikafungua uzi fasta.. Kumbe ah..
 
Mnshangaa nini enyi kizazi cha JF? Huwezi kupanda mlima bila muongozaji (Tour Guide) yeye ndiye anakusaidia/kuongoza kufika KILELENI Uhuru hata kama mumewe angeshindwa..............
Afikishwa kileleni ........................, jamani!!!!
 
  • Thanks
Reactions: awp
Tunashukuru kwa KUFIKISHWA KILELENI JIDE.
Wenzio wanapanda lakini hawafiki KILELENI ni miujiza ya mungu na mumewe kukufikisha kileleni.
Ni mfano wa kuigwa kwa wadada wa jf mnaotaka kupandishiana ili mfike KILELENI.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom