Hatimaye Kigogo wa NIC aachia Ngazi

NgomaNzito

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
559
26
Hatimaye yule kigogo wa shirika kubwa la Bima hapa nchini Mama Margreth Ikongo ameachia ngazi na kuhamishiwa wizara ya fedha kitengo cha masuala ya Bima.
Kama mnakumbuka gazeti la Mwanahalisi la wiki hii lilitoa taarifa hii likisema ni taratibu zinaendelea kufanyika na kigogo huyo kutupwa nje ikiwa inasemekana ndiye aliyelisababishia Shirika hilo kubwa hapa nchini kuwa katika hali mbaya kifedha na matumizi mabaya na kutolipwa kwa wateja madai yao ya muda mrefu.

My take yule jamaa wa Any time Cancelation ankaribia kuhamishiwa huko??

Tunatega sikio nzi wetu akirukaruka
 
Si bure jambo ninalolijua ni kwamba huyu Magreth Mwambapa Mwakabungu a.k.a Mrs.Ikongo in mtu wa UWT na ndiyo maana amhamishiwa Hazina kuweka kituo kungojea kupewa wadhifa wa kisiasa,Hili linaeleweka na hakuna kipingamizi.Kuwepo kwake NIC hakukuwa kwa tija hata kidogo,Kwani ukiachia mbali upeo wake mdogo wa uongozi aliokuwa nao tulitarajia muda mrefu sana angeondolewa ili kulinusuru shirika.Kinyume chake amezidi kuwepo zaidi ya miaka kumi (10).Kumbukeni sakata la Ubungo Plaza na Kharf &Co. huyu alikuwa ni fisadi katika mradi huu hata mpaka leo hii bado ni kitendawili kizito kwamba mali zote za NIC yakiwepo majumba ,magari na aseti lukuki havieleweki viko wapi .Hilo lilifumbiwa macho katika awamu iliyopita na akaendelea kupeta pasipo kuangaliwa wala kuchukuliwa hatua dhidi ya ubadhirifu mkubwa alioufanya.Ni mlolongo wa muda mrefu wa kulindana tu huku uchumi wa nnchi na watu wake ukizidi kusinyaaa kila kukicha katika sekta zote.
Haingii akilini kwa mtu aliyeshindwa mahali kumpa tena nafasi hata kama siyo ya uongozi lakini ya dhamana yoyote ya umma.Wahusika wachunguze hili la NIC kuna ufisadi wa kupindukia ndani ya shirika hili.Magreth apelekwe mbele ya vyombo vya sheria kujibu tuhuma hizo na siyo kumtengenezea njia nyingine ya kuwaumiza wananchi.ACHENI HIZO.
 
Who the hell is she,sababu anafanya kazi UWT ndiyo asifukuzwe wala kuwajibiak.

F*&%^ UWT,It shame..you have touch my nerve.

Hao UWT ni kina nani?kama mama huyo ni mwizi leteni ushahidi tu na tuntahakiksiaha anweza mbele ya pilato..

Go and tell that mama ,if she is your mama,ameliingiza shirika katika khali mbali na yeye ni muhujumu UCHUMI.

amesababisha watu wengi kukosa kazi na badp unamtetea ni mtu wa UWT?UWT ndiyo asiguswe?kingunge naye ni UWT?Lowassa Pia??

Shame shame,screw up and Go to hell mama Ikongo!

GO to hell UWT.Taasisis isyo na integrity ...am still pissed off unlsess UWT stands for Umoja wa Wezi Tanzania
 
Ameachishwa au amehamishiwa , si bado yumo humo humo ni usanii tu ,amaeharibu atupwe nje kabisa atafute jembe akalime hakuna tofauti na Mkwere anaehamisha kila siku sijui gharama za uhamishaji analipa nani ?
 
Usanii juu ya usanii wanajuana na wanalindana haoo wote hakuna jipya....serikali inatafuta njia ya kuutua mzigo wa nic
 
Kha Jamani,

Sikatai shirika lilikuwa na matatizo kama yalivyo mashirika yote ya uma lakini mzigo huo asitwishwe ndugu yangu huyu peke yake ki hivyo! Shirika limeanza kutafunwa tangu enzi za Mkuu wa kwanza yule marehemu leo iweje mumshupalie huyu Mama wa watu! Haya basi tuyaache hayo ......mnasema replacement wake eti atakuwa mzee wa Any Time Cancellation.....are we serious? what is with this country with recycling of the wrong type of garbage? Kha mwee! Tunachoka........tunapata kiungulia sana!

Ndeanasia
 
Taarifa zilizopatikana hivi punde Ndugu Mwandu wa Insurance Supervisory Dept. kachaguliwa kuwa New NIC MD yule tuliyekuwa tunamtegemea Mataka abaki ATCL
 
Hatimaye yule kigogo wa shirika kubwa la Bima hapa nchini Mama Margreth Ikongo ameachia ngazi na kuhamishiwa wizara ya fedha kitengo cha masuala ya Bima.
Kama mnakumbuka gazeti la Mwanahalisi la wiki hii lilitoa taarifa hii likisema ni taratibu zinaendelea kufanyika na kigogo huyo kutupwa nje ikiwa inasemekana ndiye aliyelisababishia Shirika hilo kubwa hapa nchini kuwa katika hali mbaya kifedha na matumizi mabaya na kutolipwa kwa wateja madai yao ya muda mrefu.

My take yule jamaa wa Any time Cancelation ankaribia kuhamishiwa huko??

Tunatega sikio nzi wetu akirukaruka

Mkuu siyo kweli kwamba huyu mama ndiye aliyelimaliza shirika la BIMA. Shirika lilikufa tangu akiwepo hayati mwaikambo, akaja TEMU akachimba kaburi na huyu mama alichofanya ni kupiga misumari kwenye jeneza. Hivyo kufa kwa shirika hili ni kama process ya kutengeneza kitu kiwandani kuamzania hatua ya kwanza hati kupata end product.

Hivyo shirika nalo lilikuwa katika hiyo process ya kufa tangu lilipoanza hadi sasa.
Nawasilisha hoja,
 
Tatizo ni kwamba wanapeana wao vyeo hilo shirika wakimuachia kichaa mmoja mpya kabisa kutoka nje ya recycling system yao linapona kabisa kwani tatizo lake ni dogo sana kureorganise shuguli zake upya na kuanza upya kabisa, lakini hiyo haiwezekani kwani atachukuliwa Mataka na kupewa wakati ameshafirisi ATC
 
Shirika lilikufa tangu akiwepo hayati mwaikambo, akaja TEMU akachimba kaburi na huyu mama alichofanya ni kupiga misumari kwenye jeneza. Hivyo kufa kwa shirika hili ni kama process ya kutengeneza kitu kiwandani kuamzania hatua ya kwanza hati kupata end product.
Mkuu hapa sikubaliani na wewe kabisa kwani sifa kubwa ya Mwaikambo ilikuwa kuiweka BIMA ktk hali nzuri kisha akahamishiwa TIB wakati wa amwinyi ambayo pia ilikuwa hoi bin taaban..
Mhasibu wa NIC wakati ule alikuwa ndugu yangu (sasa marehemu Mungu amlaze mahala pema peponi) nafahamu fika kwamba hadi ameacha kazi pale aliifanya kama shirika la baba yake (waswahili wanasema).
Hivyo, hizi habari za kwamba Bima ilikwisha toka wakati wa Nyerere sii kweli kabisa na sidhani kama kuna shirika lilotoa ajira kwa vijana wetu waliomaliza chuo Kikuu na vyuoni kama Bima..
Huwezi kabisa kulinganisha bima hii na ile ya mwalimu hata kama tulikuwa ktk mfumo mbovu wa Kijamaa. leo hii shirika kama NIC lilitakiwa kuwa kiungo kikuwbwa cha maendeleo ya nchi yetu ktk Ubepari lakini tumeshindwa kutokana na viongozi ambao kwanza hawafahamu Ubepari unafanya kazi vipi!..
 
Kha Jamani,

Sikatai shirika lilikuwa na matatizo kama yalivyo mashirika yote ya uma lakini mzigo huo asitwishwe ndugu yangu huyu peke yake ki hivyo! Shirika limeanza kutafunwa tangu enzi za Mkuu wa kwanza yule marehemu leo iweje mumshupalie huyu Mama wa watu! Haya basi tuyaache hayo ......mnasema replacement wake eti atakuwa mzee wa Any Time Cancellation.....are we serious? what is with this country with recycling of the wrong type of garbage? Kha mwee! Tunachoka........tunapata kiungulia sana!

Ndeanasia

Hebu tueleze utafunaji wa huyo Marehemu please...........
 
Back
Top Bottom