Hatimaye Isindigo imeisha rasmi ITV ilikuwa the best soap opera

Nilikuwa napenda nisikilize akiongea,anajua ku twist lugha yule mzee,na vi methali vyake vya kisomi,yule alikuwa mzaramo wa kizungu aisee,ntawezaje kupata clips za isidingo episodes zilizopita?
YouTube zipo mkuu lakini zile za zamani sana huwa zinafutwa
 
Halafu sasa hivi nadhani kilichobaki ni historia zao kila mmoja anaelezea yake nadhani chereli de ville anafuata Lincoln toka utotoni masomoni, jeshini, mpka uzeeni
 
Kati ya maeneo yote ya hii tamthiliya hakuna sehemu iliyo nikera kama ya Nikiwe (Pisi Kali) na Mtoto wa Tajiri Lincoln kushawishiwa na kumegwa kisela na yule mpuuzi Pastor Gabriel!!

Pia George Zamdela naye alikuwa ni Mafia sana. Ilihitaji utulivu sana kuielewa Isidingo The Need! Kinyume na hapo, unaona kama watu wanapiga piga tu stori.
Papaa G (george zamdela)alikuwa ni common mafia,ila mzee Baker hayes alikuwa ana act kama real economical hitman,nilimkubali sana yule mzee,lincoln alijaribu vyema kuvaa viatu vyake aisee
 
Umenikumbusha utotoni nimerudi tena YOU TUBE kuiangalia. Ndiye yule mwanamke niliyemkusudia, tamthilia ya kijapani. Nimeikumbuka na Journey to the west.

Sijui ni Capital TV au ni nini ile? Kila jumapili ilikuwa inaonyesha movie za kihindi 2003 au na 2004. Kuna series ya kihindi inaitwa Ganga Maiya kila siku ya Jumapili.

Kuna Days of Our Lives
Kuna The Bold and the Beautiful.
Kuna tamthilia waliionyesha ITV inaitwa Acapulco bay!

Kipindi hicho naangalia katuni vibaya! Cha kusikitisha mpaka sasa sijaacha kuangalia katuni.
Days of our lives nilipendaga sana kwa kweli, hadi leo wakati mwingine natazama YouTube
 
Hawa ndio character zao walizicheza vyema .
Sibiya - huyu alitakiwa kuziba character ya matiala ,japo alikuwa toka zamani lakini hakupewa airtime sana kama kina shorty na lucky .!
Naweza sema baada ya Gabriel kufa huyu ndio aliibeba sana soup kwa visa ,vituko anavyoibua kila siku.. Akiwa na mwenzake makgholomesa .na Gatanga ..!

Lincoln - amecheza character kubwa sana tangu zamani baada ya kina barker kuondoka na papa g akabaki yeye.
Business mogul, mafia,baba wa familia ,na mengine mengi.amepigwa risasi lakini akafumbua macho hatujui amekufa au lah na aliyempiga risasi ni mdada hajaoneshwa sura nadhani Lincoln anamjua.

Sechaba- huyu pia amecheza character kubwa sana ,ameteseka sana kutoka kufanya kazi mgodini kwa Lincoln kisha kupigwa na wazungu wale racist kuzikwa mzima mzima kuachana na mkewe relato mpka kuwa mayor kisha kupinduliwa tena na kurudi tena ,yahitaji moyo.

Kaghotalo - huyu mama ana huruma sana dakika chache tu anakupea ,alishaumizwa sana kwenye ndoa kwahiyo akaamua agawe tu kwa vijana kina ntando refa .aliwahi kuwa mke wa bwana Tyson .ni mayor msaidizi na biashara zake kama hoteli saloon nk.ana jeuri kweli kweli.

Pia tukapige kura jamni sibiya na cebisa wameingia kwenye tuzo za couple bora soup ziko 6 tuwape kura
 
Ila Sunset Beach ilikuwa kiboko. Ila iliishia njiani.
Kipindi hicho ilipigiwa kelele Hadi bungeni kwamba inamaudhui yasiyofaa kwa jamii,wanavaa vichupi SI unajua Mambo ya beach..

Leo hii tamthililia nyingi Zina maudhui ya kishoga,kutembea na vichupi sio ishu Tena,watu watembea uchi kabisa
 
Eeeeh.....nakumbuka Kuna tamthilia ya kijapani ITV...iliitwa Oshin....
Nimeikumbuka Sana...

Isidingo. Nliangalia Sana...ila nikaja achana nayo
oshin anatoka nyumbani kwenda kijijini...............
dah childhood memories☺️☺️☺️☺️
 
Isidingo iliisha muda mrefu toka mwaka jana mwezi wa tatu ilikuwa inapatika live youtube ila itv walikuwa nyuma sana
 
Kwa kweli kama mdau wa isidingo long time nimeumia sana wametuacha kwenye kitendawili kikubwa sana kwamba alikufa ama lah ,aliempiga yule ni mdada gani?
Hata hivyo nawapongeza ITV sanaa wamesema Jana wataleta soupy nyingine ya UZALO ITV wako juu sanaaa

Isidingo tutakukumbuka sana waigizaji wenu wenye chura za kushuka
Uzalo kwa miaka zaidi ya minne sasa ndio popular South African soap opera na ndio inaongoza kwa kuangaliwa.

Kama ITV wataanza kuionesha hiyo basi kwa hakika itawavutia watu wengi sana
 
IMG-20210306-WA0032.jpg
 
Umenikumbusha utotoni nimerudi tena YOU TUBE kuiangalia. Ndiye yule mwanamke niliyemkusudia, tamthilia ya kijapani. Nimeikumbuka na Journey to the west.

Sijui ni Capital TV au ni nini ile? Kila jumapili ilikuwa inaonyesha movie za kihindi 2003 au na 2004. Kuna series ya kihindi inaitwa Ganga Maiya kila siku ya Jumapili.

Kuna Days of Our Lives
Kuna The Bold and the Beautiful.
Kuna tamthilia waliionyesha ITV inaitwa Acapulco bay!

Kipindi hicho naangalia katuni vibaya! Cha kusikitisha mpaka sasa sijaacha kuangalia katuni.
Da kama mm mkuu nimeshakua mtu mzima Sana ila nasikitika kuwa bado napenda kuangalia katuni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom