Hatimaye Hamad Rashid, Shoka Hamis na wenzao wawili wafukuzwa CUF!

Points nzuri mnoo.ziko wazi na zinaeleweka na kukubalika na watu wote ambao wanaelewa maana ya uongozi.Regards
 
siasa ni unafik kama huwezi unafik basi kaa chonjo , hawa jamaa wanaelewana vizuri , Seif Sharif is the King na Hamad Rashid is the Prince .
 
kama ni kweli hii inaashiria machafuko mapya zanzibar kati ya watakaokuwa wafuasi wa Hamad na wale wa cuf
Kwani fedha anayopata mjengoni anakula na Wazanzibari? Mdomo huponza kichwa na hilo ndilo liliopo kwa Hamadi Rashid.
 
Sawa hawa ni wanachama wa CUF Zanzibar - Je, huko bara umekutazama?... Yaani sasa hivi kila mwanaCUF kahamia CCM kwa taarifa yako CUF bara kwisheny...Tatizo lenu mnasahau kwamba kuna Wazanzibara pia yale yale ya Nyerere!...
Utasikia utambi ukiwashwa Tanga na Kusini hivi karibuni.

Juu ya udhaifu mnaodai kwa MS lakini alichozungumza ni hali ya Zanzibar. Kama umependa kazi yake aliyofanya huko basi ni kumuomba tu awaandikie kwa yanayojiri upande wa pili.
 
Nadhani chadema ikimruhusu ajiunge hili swala la kusingiziwa udini na ukanda itakuwa imepungua

Huwezi kupinga udini kwa kujaza waislamu au wakristo kwenye chama, hou ni unafiki! Mwenye mapenzi na chama ajiunge kwa hiari yake mwenyewe kama Prof. Safari. Sio kulambwa miguu.....
 
Je hoja za ndugu hr zina mashiko? Nafikiri hilo ndilo la msingi, mengine hayo ni propaganda tu!
 
ni kweli. Naisikia sauti ya Duni Haji ndani ya hayo maandiko. Ila Hamad songesha tu
 
nnn-564x272.jpg


Historia ya Zanzibar ni ndefu sana katika dunia. Tunaweza kusema pia tarikh ya Zanzibar imechukua muda mrefu kuenea katika ulimwengu. Wanahistoria mbalimbali na hata wa wagunduzi wa kimataifa wameandika mambo mengi na vitabu vingi tofauti tokea mwaka 1980 lakini vyote ukivitizama, ukivusoma na ukiunganisha maudhui yake vinakupa ishara ya kuviona visiwa vya Zanzibar ni katka visiwa vichache vilivyo duniani vilivyo na umaarufu, usataarabu na uwelewa wa mambo kwa watu wake.

Historia hiyo hiyo haikuwacha kuwazungumza wakaaji, wenyeji au wazaliwa wa visiwa hivi kwa mapana na marefu kiasi ambacho imeonyeshwa kwenye maandiko mengi kama wenyeji wa visiwa hivi ni watu walio makini, mahodari, wazalendo na wafuatiliaji na wapambanaji.

Kwa mtiririko huu ndio tunapoona mampambano yameanza mbali tokea hata kabla ya Mreno, kuja kwa Mreno, kung'olewa kwa Mreno, na mapambano mbalimbali hii yote ikionyesha ushujaa wa watu wa visiwa hivi kutetea haki zao. Zama hizo zilipokwisha zama za kisiasa ziliingia kuanzia miaka ya 1957. Siasa ziliingia katika miaka hiyo na zikashamiri katika visiwa vya Unguja na Pemba. Kwa kuwa siasa ilishamiri basin a fitna na khiana nazo zilichukua nafasi yake nazo zikawa sehemu ya harakati hizo za siasa. Matokeo yake yakawa ni mapambano ya ndani yaliyochukua sura ya chuki na kupambana wenyewe kwa wenyewe hadi kupelekea kupotea kwa maisha ya watu wengi na wengi wao wakiwa hawana hatia.

Haya yote yametendeka kwa kuwa tu baadhi ya wahusika walisimamia zaidi ubinafsi wao kuliko maslahi ya wengi. Mduara huu uliozunguka visiwa hivi uliviathiri na kuvipotezea watu wengi maisha yao. Wenine wengi wakahama nchi yao wanayoipenda na kusambaa katika kila pembe ya ulimwengu kwenda kuhuisha uhai wao na hata kufikia kusahau kwao kwenye asili yao, kulikofukiwa vitovu vyao na vya wazee wao. Hawana lawama kwani si makosa yao bali ni makosa ya ubinafsi na khiana za wenye tama.

Nimeanza na utangulizi huu kwa lengo la kukumbusha ili tunapoamua kujadili mambo, matokeo au watu mbali mbali kwa nafasi zao za utumishi wa kinchi au wa kisiasa tunapaswa turudi nyuma kwenye historia yetu ili kwanza kujiangalia na halafu twende mbele kwa kufanya maamuzi yenye busara. Vinginevyo pasi na uangalifu wa kupima kwa mezani iliyo sawa tutakuja kujikuta tunashabikia mambo na kuyamini mambo hayo kinyume na uhalisia wake.

Hali hii ni kama hivi sasa miongoni mwetu tunavyoliona na kulitazama hili sakata la kufukuzwa Hamad Rashid katika chama cha CUF kwa mtazamo ulio mwepesi na kuvutwa na upepo wa hadaa za mwanasiasa aliyejiandaa kutizama ubinafsi wake kuliko dhamira ya kweli ya mapambano iliyotegemewa kuonyeshwa na kusimamiwa na nafsi yake.

Hamad Rashid Mohammed kwa wakati ule, alikuwa ni miongoni mwa vipenzi vya rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius K. Nyerere hata kufikia kwa mwalimu Nyerere kumpa nafasi nyeti ya kuwa naibu waziri wa fedha wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Bila shaka alipata nafasi hii baada ya kukubalika na idara ya usalama wa taifa.

Hata hivyo Hamad Rashid alijiunga na mapambano ya kudai haki za Zanzibar katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania akiwa ndani ya CCM pamoja na Maalim Sei.. Jambo hili llipeleea kufukuzwa katika system ya chama cha CCM yeye, Maalim Seif na wenzao wengine wakipewa muda mdogo kujitetea na hapohapo hukumu kufuata.

Alijiunga na vugu vugu la kudai heshima na haki ya Zanzibar ndani ya muungano kabla ya kuundwa kwa vyama vingi vya siasa katika miaka ya 1980. Alishiriki katika kuasisi chama cha CUF mwaka 1992 na vugu vugu lake kubwa lililopelekea watu kuteswa, kufukuzwa makazini, kufungwa na kuuliwa.

Katika uchaguzi wa mwanzo wa vyama vingi 1995 ambao chama cha CUF kilikuwa kikitarajiwa sana kutwaa serikali ya Zanzibar, Hamad Rashid aligombea uwakilishi kwa matarajio ya kuwa waziri wa serikali ya Zanzibar. CUF imekuwa ikinyimwa ushindi wake Zanzibar kwa ubabe unaofanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kuwa ilifahamika chama cha CUF lengo lake ni kurudishwa kwa dola ya Zanzibar. Baada ya kuuona muelekeo wa siasa za Zanzibar wa kuporwa ushindi kila baada ya uchaguzi kwa nafasi ya urais aliamua kugombea ubunge katika uchaguzi wa pili uliofuatia wa mwaka 2000. Aliendelea kuwa mbunge hadi muda huu anafukuzwa katika CUF.

Mwaka 2009, Maalim Seif na Rais mstaafu Amani Karume walileta maridhiano ya wazanzibari yaliyopelekea kwa mara ya mwanzo kufanyiwa marekebisho ya katiba ya Zanzibar yaliyotamka kuwa Zanzibar ni nchi na kuweka msimamo wa kuyaondoa mafuta katika orodha ya mambo ya muungano. Baada ya kumalizika uchaguzi mkuu wa 2010 serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar iliundwa. Hamad Rashid alitegemea kupata nafasi ya uwaziri katika serikali ya umoja wa kitaifa kwa kuteuliwa kuwa mwakilishi. Bahati mbaya Hamad Rashid hakuteuliwa kuwa waziri na hivyo suala hili halikumfurahisha.

Serikali ya Jamhuri ya muungano ilimteua Hamad Rashid kuliwakilisha bunge la Tanzania katika bunge linaloziwaklisha nchi za jumuiya ya madola, commonwealth Parliamentary Assembly (CPA) akiwa ni mbunge wa bunge hilo na makamo mwenyekiti wa kamati ya fedha ya bunge hilo. Nafasi hiii alikuwa ameishika kwa muda mrefu mbunge wa CCM, Bwana Mporonyoki. Nafasi hii ni nyeti na kakatifu hapewi mtu isipokuwa anaeaminiwa na CCM. Jambo hili lilimnyima Hamad Rashid muda wa kuwepo bungeni na kulitumikia bunge ipasavyo.

Hivi tujiulize msingi wa mapambano ya Hamad Rashid ndani ya CUF ameutoa wapi ghafla? Kwa nini basi iwe ni ndani ya kindi hichi ambacho chama kinajipanga na mchakato wa katiba mpya ambao ndio msingi mkuu wa kuundwa kwa CUF? Jee hivi kweli agenda yake ya mapambano ni kwamba Maalim Seif anakiuwa chama? Kwamba matawi ya CUF hayafunguliwi? Kwamba Maalim Seif hafanyi ziara Tanzania bara? Kwamba Maalim Seif hakushiriki kampeeni za CUF bara?

Hivi karibuni Hamad Rashid ameuthibitishia umma wa watanzania msimamo wake mpya juu ya mustakbala wa muungano kinyume na msimamo wake ule aliofukuziwa katika CCM na akashiriki kuunda CUF. Msimamo ambao ndio msingi wa mapambano ya wadai haki wa Zanzibar pale alipoulizwa na kutakiwa na mwandishi wa Star TV atoe msimamo wake thabit juu ya muungano tulionao anauonaje, na ana maoni gani juu ya marekebisho ya katiba. Jawabu yake ilikuwa ni kwamba anaamini umoja ni nguvu utengano ni udaifu.

Na yeye mara zote amekua akisimama katika umoja. Wa bara wanaishi Zanzibar na wa Zanzibar wanaishi bara, hivyo ni jambo la kuendelezwa. Kero anayoiona yeye katika muungano ni kwamba mpaka leo hakuna tume ya pamoja ya fedha, jambo ambalo lingeweza kuondoa kero ndogo ndogo zilizopo.

Hivi ni kweli Hamad Rashid alifukuzwa katika CCM kwa kuwa kulikosekana tume ya pamoja ya fedha? Hivi kweli Hamad Rashid alikubali kuachishwa kuwa naibu wazri wa fedha wa Jamhuri ya muungano kwa kukosekana tume ya pamoj ya fedha?. Hivi ni kweli tatizo na kero za Zanzibar katika muungano ni kukosekana kwa tume ya pamoja ya fedha? Hii ndio ile khiana tulioizungumzia kule mwanzo. Hamad Rashid amethibitika sasa hasimami tena katika ile misingi mikuu ya wazanzibari ya kudai haki, hadhi na heshma ya Zanzibar katika muungano. Tokea alipoanza kuvitawala vyombo vya habari kwa kuibua kwake madai dhidi ya CUF hajawahi kusikika kutumia nafasi hiyo kukosoa mfumo wa muungano au kuzizungumzia shida za wazanzibari katika muungano huu.

Hivi karibuni Maalim Seif aliitisha Mkutano wa Hadhara kibanda maiti Unguja wenye lengo la kuwafahamisha wazanzibari juu ya mambo muhimu ya kuzingatiwa wakati wa mchakato wa katiba mpya ikiwemo nafasi, heshma na hadhi ya Zanzibar katika katiba mpya. Hamad Rashid amejitokeza na kutoa machapisho kuhoji uhalali wa Maalim Seif kutoa maelekezo hayo, hasa katika kipengele cha Zanzibar kuwa na benki kuu yake na sarafu yake. Pia pale Maalim Seif aliposema kama ni serikali mbili basi kila mmoja na yake. Lengo lake ni kujaribu kuonyesha kwamba Maalim Seif ni hatari (threat) ndani ya Serikali ya Zanzibar.

Hii ndio ile khiana tulioisema mwanzoni. Kuzusha mgogoro huu ni khiana yake katika kufikia lengo lake. Sayyidna Ali (AS) anasema, "asiyeweza kuficha siri yake hawezi kuficha ya wengine, watu wanafiki hujipamba kwa uongo. Achukiza sana mtu mwenye nyuso mbili". Lakini sasa mma umeshafahamu, khiana haina tena nafasi.

Forward forever! Backword never!

Nendeni umoja wa mataifa mkaombe uhuru wenu jamani, mbona mnatusumbua!?
 
kwa kweli sasa mengi tutayajua na kujifunza ambayo yaliokuwa yamejificha.

bwana Hamad ameamua kumwaga mbona baada ya wenziwe kumwaga ugari, ila nnadhani ameshachelewa.


kuhusu suala la kuanzisha chama na kukubalika kwa Tz sidhani pia. maana mkuu huyu ni mzuri wa kugonganisha fikra za wabara na wazanzibari. maana akiwa zanzibar hujifanya yeye ni mtetezi mwema wa wazanzibari, na hawa hasa ndio waliowafanya wazanzibari wawahisi ndugu zao wabara kuwa sio ndugu zao ila ni wakoloni. fitna hii Hamad na Mwenziwe Seif hawawezi kuikwepa.

jengine akiwa bara hujifanya yy yuko tofauti na akina Seif ati yy ni mzanzibari anaependa muungano na hana kasumba za kibaguzi, ati yy anaamini kuwa sote ni watanzania.


na anapokuwapo Pemba huyu bwana huwasema sana waunguja na kujaribu kuwajenga ndugu zetu wa pemba kuwachukia ndugu zao waunguja na hili ndilo ambalo karibu viongozi wengi wa CUF wanalifanya.


kwa ba Hamad siri utazozitoa na ujiseme na mm ni miongoni mwa watenda fitna hizo
 
Sawa hawa ni wanachama wa CUF Zanzibar - Je, huko bara umekutazama?... Yaani sasa hivi kila mwanaCUF kahamia CCM kwa taarifa yako CUF bara kwisheny...Tatizo lenu mnasahau kwamba kuna Wazanzibara pia yale yale ya Nyerere!...
Utasikia utambi ukiwashwa Tanga na Kusini hivi karibuni.

Nimepata simu kutoka kwa ammi yangu wa Pujini pemba.

Amesema leo baada swala ya ijumaa watuwa WAWI watapata halua kushangilia kwa Hamad Kufukuzwa CUF. naomba mlifuatilie hilo.

Na nazidi kujiuliza. Hivi hamad hana Kwao. Kwanini asirudi kwa wapiga kura wake wa Wawi kuwasabahi kama alivyofanya kafulila?

haya yetu macho. labda anataka kugombe jimbo la temeke, Dar.

Pole sana.

 
Kwa hakika , Siku zote ndege mjanja hunasa katika tundu bovu.

Hakika Hamad Rashid ameshindwa kusoma alama za nyakati kwa kutumia vyombo vya habari vya huko tanzania katika kujijengea umaarufu pasi na kujua kuwa kila kitu kina tartibu na kaanun zake.

Tunajuwa fika kuwa hata nyumbani kwako kama kuna mtu ana mushkirah wowote basi kuna taratibu za kuwasilisha malalamiko yake na sio kutoka nje na kuanza kupiga mayowe. Hivyo hata vyama vyote vina taratibu zao za kumaliza migogoro yao kwa kupitia vikao vyao vya ndani na taratibu nyingine lakin si kukimbilia vyombo vya habari.

Hakika vyombo vya habari vya Tz vimemmaliza kabisaa Hamad. Kwani vyenyewe havimsaidiii bali vinafanya biashara ya kuuza habari zake huku vikimmaliza kisiasa pasi na mwenyewe kujua.

Siku zote taarifa za vikao utolewa na msemaji wa Chama na sio kila mtu ana nafasi hiyo. Jana niliongea na ammi yangu ambaye yupo Pujini ameweka wazi kabisa kwa kosa lake hamad hata kwao wawi hawamtaki na ndio maana hana mpango wa kwenda wawi kwa wapiga kura wake kama alivyofanya kafulila.

Hakika vyombo vya habari vimemmaliza kabisa kisiasa Hamad Rashid. Na kwa mujibu wa historia wote waliofukuzwa CUF hakuna aliyekuja juu.
Mfano. Bi naila majid Jidawi, Mapalala, Salum Msabaha, Rwekatare n.k. watazameni hao kisiasa wakoje hivi sasa na hshma yao kwa jamii ikoje?

Pole sana Hamad RASHID.
 
Umejaribu kutaka kueleza kitu ila umeshindwa kueleza nini ulitaka watu wajue kwa maelezo yako umeshindwa kuonyesha nani mkosa kati ya seif na hamad rashid
 
Kwani Dogo hilo?


Hilo si dogo na ukubwa halina; cha msingi wanachokitafuta akina Hamadi ni kuirudisha CUF kiwe chama cha siasa kama mbinu waliyoitumia sio sahihi labda ungejaribu, kuja hoja ya nini kifanyike; Maalim amekuwa mamluki wa demokrasia atewezaje kesho kudai haki sawa kwa wote ilhali ndani ya nyumba yake haki haitendeki? CUF kimegeuka kama genge la wahuni kwa lengo la kujichotea ruzuku, huku Maalim akijifanya ndiye mungu wa Pemba, alichokifanya Hamadi kama ni sahihi au si sahihi hili limeshamuonyesha Maalim ni mtu wa namna gani; wana CUF wenyewe ndio watakaoamua.

Chama
Gongo la Mboto DSM.
 
Back
Top Bottom