Hatimaye Dk. Juma Mwaka ajisalimisha Polisi

Hatimaye Dk. Juma Mwaka ajisalimisha Polisi

Afya ya binadamu sio ya kuchezea ,Mwaka aende shule miaka 5 akasome kama ana credit asilete mzaha
 
wakamataji wote wamekunywa kikombe cha babu kwa kuamini watapona maradhi yao...sasa hivi anaanda kikombe kingine anawavutia pumzi tuu...
 
Mwaka amesaidia wengi sana mimi shuhuda, ajabu sijaona hata mmoja alielalamika kadhurika na tiba za mwaka, chuki ya kipato chake. Mbona babu wa loliondo hakamatwi au kuna ushahidi gani anatibu ukimwi? Kichaa cha serikali ni kushuhulika na mambo ambayo yanweza kujitatua na kuacha mabo ambayo ni lazima wayatatue. Kama dawa za mwaka zingekuwa fake asingepata wagonjwa jamani mbona hesabu rahisi tu?!. Embu washuhulike na mambo ya msingi., ikiwepo kugawa mashamba kwa vijana na si kuwahimiza walime wakati wengi hatuna mashamba, tulime lami?!
Mkuu watu wengi hawana ujuzi wa kutambua kuwa wanatapeliwa, na matapeli wengi wana akili sana husoma sikolojia ya watu anaowalenga.

Kuna matapeli wanaotumia dini, mabenki, hospitali nk. hata shule za kitapeli zipo, ndio maana kuna regulatory boards za ku monitor huduma hizo.

Mwaka yeye anatumia magonjwa ya akinamama ambayo ni mengi kutapeli. Haiingii akilini mtu hana kizazi completly ukamuwekea kizazi ni Mungu tu anayeweza hiyo kazi.

Eti mtu anatibu kansa wazungu wenyewe wameshachemsha zaidi ya kukatwa kiungo. Sasa Mwaka anadanganya kina dada masikini wasio na uelewa badala ya kuwashauri mgonjwa kuwahi kwenye vipimo vya kisasa yeye anampa dozi aweke kwenye dumu la simtank lt 500 atumie mwaka mzima, matokeo yake anajikuta kansa imekuwa sugu na kuishia kukatwa matiti yake.

Mtu pekee wa kuwasaidia kinadada kama hao ni kupitia wizara ya Afya tu.
 
Jambazi ni jambazi tu hata kama halijakuibia wewe.
Ni kweli sipingani na wewe. Ila tukubaliane kuwa kuna majambazi basi wanapewa vibali na serikali vya kufanya ujambazi! Kwa sababu huyu jambazi alisajiliwa na mamlaka zinazotambulika serikalini. Sioni kosa lake, na zaidi ya hapo sehemu kubwa ya jamii ikakubali ujambazi wake. Au kuna uwezekano amevuka mipaka ya kufanya huo ujambazi wake kwa utaratibu wa kibali alichopewa ndio maana wanamkamata!?
 
Mkuu watu wengi hawana ujuzi wa kutambua kuwa wanatapeliwa, na matapeli wengi wana akili sana husoma sikolojia ya watu anaowalenga.

Kuna matapeli wanaotumia dini, mabenki, hospitali nk. hata shule za kitapeli zipo, ndio maana kuna regulatory boards za ku monitor huduma hizo.

Mwaka yeye anatumia magonjwa ya akinamama ambayo ni mengi kutapeli. Haiingii akilini mtu hana kizazi completly ukamuwekea kizazi ni Mungu tu anayeweza hiyo kazi.

Eti mtu anatibu kansa wazungu wenyewe wameshachemsha zaidi ya kukatwa kiungo. Sasa Mwaka anadanganya kina dada masikini wasio na uelewa badala ya kuwashauri mgonjwa kuwahi kwenye vipimo vya kisasa yeye anampa dozi aweke kwenye dumu la simtank lt 500 atumie mwaka mzima, matokeo yake anajikuta kansa imekuwa sugu na kuishia kukatwa matiti yake.

Mtu pekee wa kuwasaidia kinadada kama hao ni kupitia wizara ya Afya tu.
pole sana kwa kuamini kuwa wazungu ndio wako sahihi, samahani lakini ila pole sana.
 
Nahisi kuna mashinikizo fulani katika mahakama zetu.
Labda ungefafanua hayo "mashinikizo fulani katika mahakama" kama siyo hisia tu!

Viongozi wa kisiasa, wanaodai kutokuwepo demokrasia nchini, ni budi kwanza waheshimu taasisi za kidemokrasia (mahakama na bunge)zilizopo, wanachama na wananchi waliowapa nafasi za kuongoza.

Kuhamasisha mikutano ya hadhara na maandamano ni kiashirio kwamba wakipewa madaraka ya Dola, hawataheshimu kamwe taasisi za kidemokrasia.

Kufanya hivyo ni sawa na Tabibu Mwaka ambaye anakiuka masharti yaliyowekwa ya kufanya shughuli zake za utabibu, na amri halali za Mamlaka zilizo juu yake. Lakini kuna watu wanamtetea.

Nchi ikiongozwa bila taratibu, kanuni na sheria, haitatawalika. Ndiyo maana kuna mahakama pale ambako haki haikutendeka.

WAKATI NDO HUU WA KUUENGA NCHI KWA PAMOJA - UMOJA NI NGUVU
 
Jeshi la polisi limefanikiwa kumtia nguvuni tabibu Juma Mwaka, maarufu Kama Dokta Mwaka, baada ya kumsaka Kwa siku kadhaa bila mafanikio.

Polisi yasema mmiliki wa Foreplan Clinic tabibu Juma Mwaka amejisalimisha Kituo Kikuu cha Polisi Dar leo, atakiwa kurudi kesho kwa mahojiano.

Jeshi la polisi linatekeleza agizo la Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Hamisi Kigwangalla kuwa tabibu huyo mashuhuri akamatwe Kwa kukiuka agizo la Serikali la kuacha kutoa huduma za tiba asili na tiba mbadala baada ya kufutiwa kibali na Baraza la tiba asili na tiba mbadala, ambao walimkuta na hatia ya kukiuka masharti ya sheria ya tiba asili na tiba mbadala ya Mwaka 2002, sheria namba 23, ulaghai wa kujiita dokta na kujifanya amesomea tiba ya kisasa kumbe la, kukutwa na shehena ya dawa za kisasa zaidi ya boksi 200 bila vibali vya mamlaka ya chakula na dawa, TFDA na kukutwa na shehena ya dawa za tiba asili na tiba mbadala kinyume cha sheria, haswa baada ya kufutiwa usajili wa kutoa huduma hizo.

Tabibu Mwaka alikuwa Polisi Kwa mahojiano katika kituo cha kati.
Nimekumbuka kilichotokea kwa Dr.Masao bingwa wa Magonjwa ya moyo na hospital yake aliyofungua wenye chuki binafsi wakamfrustrate to death!
Hii nchi kuna wanadamu wabaya sana!
 
pole sana kwa kuamini kuwa wazungu ndio wako sahihi, samahani lakini ila pole sana.
Pole na wewe kwa kuamini Mwaka atakurudishia kizazi.

Vitu vyetu vingi tunavyotumia haviko scientific proved sawa na dawa za Mwaka hazina research yeyote, ukimuuza alizigungundua vipi sana sana atakuambia alioteshwa.
 
Vitu vyetu vingi tunavyotumia haviko scientific proved sawa na dawa za Mwaka hazina research yeyote, ukimuuza alizigungundua vipi sana sana atakuambia alioteshwa.
Kama kaoteshwa na zinatibu kuna shida gani? Hizo ambazo ziko scientific na hazitibu zina faida gani? Mbona hata ugali mtu alioteshwa tu akaupika na haujawahi kumdhuru mtu? Acheni kuamini sna uzungu hata wao pia wanaoteshwa ndio wanaingia maabara.
 
Babu wa Loliondo alisomea wapi mkuu? Mbona serikali yote ilihamia huko kunywa kikombe?
Kwani babu wa Loliondo alikuwa anatumia Ultrasound kutibu?

Mwaka amefungiwa kwa kutumia vifaa vya hospitali ambavyo anatakiwa mtaalam kuvitumia.

Mfano unapotakiwa kupigwa X-ray kuna vyakula unaambiwa usitumie au usile kabisa siku hiyo yeye huo ujuzi kusomea wapi.
 
Ni wote wanafungiwa? Sijasikia akina Ndodi na Rahabu
 
Kama kaoteshwa na zinatibu kuna shida gani? Hizo ambazo ziko scientific na hazitibu zina faida gani? Mbona hata ugali mtu alioteshwa tu akaupika na haujawahi kumdhuru mtu? Acheni kuamini sna uzungu hata wao pia wanaoteshwa ndio wanaingia maabara.
Achana na mambo ya ujima tuko kwenye electronic era mkuu.
 
Achana na mambo ya ujima tuko kwenye electronic era.
Hizo electronic era zingesaidia watu wasingefurika kwa mwaka, atapiga sana hela, atatibu sana bila hata ya kuwa na hospital. huko mahospital maleria tu imewashndia, itakuwa haya makubwa atibuyo mwaka?! Kalagabaho kumuacha babu wa loliondo alietangaza kuponya ukimwi na hawakupona kuhangaika na mwaka anaetangaza kuponesha na watu wakapona. Kupanga ni kuchagua, na hapa kigwa kachagua galasa kupambana na mwaka.
 
Mungu pekee ndiye anajua nchi hii inaelekea wapi!!
Mungu ni mkuu sana hatotuacha tutumbukie shimoni..

Tukeshe tukiomba before things get out of hand.!!!

Sentensi ya kwanza Na ya pili zinakinzana labda kama wewe ndio huyo Mungu otherwise ya pili inaonesha hata wewe unajua inakoenda.
 
Hizo electronic era zingesaidia watu wasingefurika kwa mwaka, atapiga sana hela, atatibu sana bila hata ya kuwa na hospital. huko mahospital maleria tu imewashndia, itakuwa haya makubwa atibuyo mwaka?! Kalagabaho kumuacha babu wa loliondo alietangaza kuponya ukimwi na hawakupona kuhangaika na mwaka anaetangaza kuponesha na watu wakapona. Kupanga ni kuchagua, na hapa kigwa kachagua galasa kupambana na mwaka.
Tujadili tu lakini serikali imeshatimiza wajibu wake kafungiwa, kama anajipenda a comply na kanuni na taratibu za utabibu. Mengine tunafurahisha baraza.

Serikali hawezi ku-take risk kuruhusu dawa itumike eti kwa vile jirani yako alipoitumia alipona.

Unaweza kutuambia ni wangapi wamedhuriwa na dawa zake ambazo haziko proved na chombo chochote?

Kama mnampenda sana mshauri arudi shule miaka mitano siyo mingi, lakini siyo kwenda short course ya miezi mitatu India halafu aje kutudanganya eti anatibu magonjwa yote, never, atawapata type yenu.
 
Back
Top Bottom