Elections 2010 Hatimaye DED wa Hai district atoswa, alikataa kuidhinisha 100m kumwondoa Mbowe

Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,762
825
yuele mkurugenzi wa wilaya ya hai bwana mtega sasa yamemfika baada ya kutemwa rasmi wiki hii kwa maelekzo ya makamba na celina kombani!

amehamishiwa makao makuu tamisemi bila shaka kumkomoa. mnamo wiki mbili zilizopita mbowe alizindua kampeni zake kwenye mji wa bomangome. shughulizote zikasimama akapokelewa kama mfalme.

kesho yake labda kwa kiwewe cha kushindwa, mkuu wa mkoa anayekaimu said kalembo alifunga safari toka tanga kuja moshi, wakafanya kikao yeye , mbunge fuya kimbita, mkuu wa wilaya ya hai somebody msigala, nk, ikaamuliwa ded atoe 100m toka kwennye halmashauri eti kusawazisha mambo

ded alipopewa maagizo hayo alitaka aelekezew mahali pa kutoa hilo fungu, na kwa maandishi. ndipo alipoonekana hafai.

nafasi yake imechukuliwa na afisa mipango wa wilaya ya same mr. humbe ambaye anakuja hai kuhakikisha mbowe anashindwa

kuwemi machp
 
Hili li nchi linaitwa Tanganyika hata shetani akikaribishwa, atalikimbia. Mateso na manyanyaso kila kona, si ofisini, si hospitali, kisa kuna kitu kinaitwa CCM aaaaaaaaaaaaggggggggggghhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kichwa cha habari hakijakaa sawa pengine kingesomeka: DED Atoswa kwa kukaidi kumtosa Mbowe Hai, ni mawazo tu
 
Kichwa cha habari hakijakaa sawa pengine kingesomeka: DED Atoswa kwa kukaidi kumtosa Mbowe Hai, ni mawazo tu

sawa njilembera, unaweza ku-edit? watu wengine siyo fani zetu. ukiweza ku-edit itakuwa vema
 
Jamani watanzania shime tuamke na kuuondoa utawala huu wa kiimla, wakati hospitali hazina dawa na wanafunzi wanakaa chini wengine wanataka kutoa milioni 100 za wananchi masikini ziwashindishe uchaguzi.... Huyo Kimbita kwa nini asitoe zake??? Yeye si ndio anayetaka ubunge??? Wana Hai mkataeni huyo mnafiki, hii ni nchi ya watanzania na sio Cartel ya mafisadi wakatuendesha kama wanavyotaka. Wazee kama Kalembo wameishafikia wakati wa kustaafu lakini wanang'ang'ania kubakia madarakani kwa ajili ya njaa tu ndo mana wanajikuta wakimtumikia shetani ili wabakie madarakani. Ni aibu kubwa kuwa hili taifa halina muelekeo...
 
Dc wa Hai ni Dr Norman Msigala.

Aliwahi kuniambia yeye ni mlokole, nashangaa kama ameshiriki kwenye vituko vya rushwa.

Mungu wamulike genge la CCM.
 
Dc wa Hai ni Dr Norman Msigala.

Aliwahi kuniambia yeye ni mlokole, nashangaa kama ameshiriki kwenye vituko vya rushwa.

Mungu wamulike genge la CCM.

Mkuu usishangae,kule Makete wakati wa kura za maoni alipata tuhuma za rushwa (watoto wa sekondari Iwawa walipewa kadi za CCM ili wampigie kura) haikuwa rizki.
 
yuele mkurugenzi wa wilaya ya hai bwana mtega sasa yamemfika baada ya kutemwa rasmi wiki hii kwa maelekzo ya makamba na celina kombani!

amehamishiwa makao makuu tamisemi bila shaka kumkomoa. mnamo wiki mbili zilizopita mbowe alizindua kampeni zake kwenye mji wa bomangome. shughulizote zikasimama akapokelewa kama mfalme.

kesho yake labda kwa kiwewe cha kushindwa, mkuu wa mkoa anayekaimu said kalembo alifunga safari toka tanga kuja moshi, wakafanya kikao yeye , mbunge fuya kimbita, mkuu wa wilaya ya hai somebody msigala, nk, ikaamuliwa ded atoe 100m toka kwennye halmashauri eti kusawazisha mambo

ded alipopewa maagizo hayo alitaka aelekezew mahali pa kutoa hilo fungu, na kwa maandishi. ndipo alipoonekana hafai.

nafasi yake imechukuliwa na afisa mipango wa wilaya ya same mr. humbe ambaye anakuja hai kuhakikisha mbowe anashindwa

kuwemi machp
Dah, kwa wale mliopiga theory kidogo kuna kitu kinaitwa 'Rise and Fall' sasa mimi naamini ili tukae level lazima tudundane kidogo!! ili tuanze tena upya nadhani tutaheshimiana.........
 
Hivi watu wanaoishabikia CCM wana akili kweeli? Sasa ded aaliyetaka justification anafukuzwa, analetwa ambaye atasema YES SSIR!!!!!!! nchi hii imekwisha. Bye
 
Let thiz year be an historic for receivin New Hope..ts time. Dr. Slaa z READY for presidency! Mungu Ibariki Tanganyika
 
Dah, kwa wale mliopiga theory kidogo kuna kitu kinaitwa 'Rise and Fall' sasa mimi naamini ili tukae level lazima tudundane kidogo!! ili tuanze tena upya nadhani tutaheshimiana.........
together sana mkuu. tuzipange km Kenya ili tuheshimiane na katiba mpya iwepo.
 
Mtendaji yeyote atakae kuwa mpumbavu na kukubali kuidhinisha pesa za umma bila mpango kwa maelezo ya hawa mbwa mwitu kina Makamba itakula kwake hapo baadae. Kwani wakati utakapofika wa kuburuzwa mahakamani kwa wizi haya majangili ya ccm hayakawii kujivua na kumwachia kesi mhusika kwa maelezo kwamba chama hakifisadi ila mtu binafsi. ded ana akili sana binafsi namsifu, kwani anajua ni nini kiliwatokea waliotumiwa kupitishia pesa za wizi ktk account ya EPA. Kuna waliobaki kama kina Kimei wa CRDB kwani pesa kubwa sana ya genge hili la wanyanganyi imekuwa kwa mda mrefu ikipitishiwa kwenye benki hii. Hata ya Kagoda ilipitia hapa hapa crdb. EEH MUUMBA JALIA MKOMBOZI SLAA KUCHUKUA USUKANI WA TAIFA HILI LINALOLAZIMISHWA KUSHUKA SHIMONI LIKIWA HAI NA MAFISADI CCM.
 
yuele mkurugenzi wa wilaya ya hai bwana mtega sasa yamemfika baada ya kutemwa rasmi wiki hii kwa maelekzo ya makamba na celina kombani!

amehamishiwa makao makuu tamisemi bila shaka kumkomoa. mnamo wiki mbili zilizopita mbowe alizindua kampeni zake kwenye mji wa bomangome. shughulizote zikasimama akapokelewa kama mfalme.

kesho yake labda kwa kiwewe cha kushindwa, mkuu wa mkoa anayekaimu said kalembo alifunga safari toka tanga kuja moshi, wakafanya kikao yeye , mbunge fuya kimbita, mkuu wa wilaya ya hai somebody msigala, nk, ikaamuliwa ded atoe 100m toka kwennye halmashauri eti kusawazisha mambo

ded alipopewa maagizo hayo alitaka aelekezew mahali pa kutoa hilo fungu, na kwa maandishi. ndipo alipoonekana hafai.

nafasi yake imechukuliwa na afisa mipango wa wilaya ya same mr. humbe ambaye anakuja hai kuhakikisha mbowe anashindwa

kuwemi machp

Maandalizi ya wizi wa kura hayo.
 
Mtendaji yeyote atakae kuwa mpumbavu na kukubali kuidhinisha pesa za umma bila mpango kwa maelezo ya hawa mbwa mwitu kina Makamba itakula kwake hapo baadae. Kwani wakati utakapofika wa kuburuzwa mahakamani kwa wizi haya majangili ya ccm hayakawii kujivua na kumwachia kesi mhusika kwa maelezo kwamba chama hakifisadi ila mtu binafsi. ded ana akili sana binafsi namsifu, kwani anajua ni nini kiliwatokea waliotumiwa kupitishia pesa za wizi ktk account ya EPA. Kuna waliobaki kama kina Kimei wa CRDB kwani pesa kubwa sana ya genge hili la wanyanganyi imekuwa kwa mda mrefu ikipitishiwa kwenye benki hii. Hata ya Kagoda ilipitia hapa hapa crdb. EEH MUUMBA JALIA MKOMBOZI SLAA KUCHUKUA USUKANI WA TAIFA HILI LINALOLAZIMISHWA KUSHUKA SHIMONI LIKIWA HAI NA MAFISADI CCM.
Kwa taarifa yako wale wote ambao hawajafukuzwa wameshaidhinisha hiyo kitu huko wilayani kwao.
Pesa ya bajeti ya nchi inaingia kukampeinia chama kilichokusanya zaidi ya bilioni 50 za kampeni kibindoni.
Halafu CAG baadae anakuja kutuambia hizi hati chafu ni kutokana na kutopata risiti za matumizi halali wakati hata hiyo miradi haijaguswa asilani.

Tuijengee heshima serikali kwa ajili ya wananchi hivyo basi tuipigie kura CHADEMA kiwe chama mbadala wa CCM.
Ni CHADEMA pekee ambayo inapata upinzani hata kutoka kwa wapinzani wengine. kinaogopwa kwa msimamo wake thabiti na utashi wa kuutumikia umma wa watanzania kwa uadilifu.

Mwacheni kikwete akapumzike salama kijijini kwake wakati nchi tunaikabidhi kwenye mikono salama
 
Hili li nchi linaitwa Tanganyika hata shetani akikaribishwa, atalikimbia. Mateso na manyanyaso kila kona, si ofisini, si hospitali, kisa kuna kitu kinaitwa CCM aaaaaaaaaaaaggggggggggghhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!
Kuanzia leo zimebaki siku 31 TU kuliondoa DUDE liitwalo CCM. Shime watanzania hii ndio fursa pekee
 
Kama DED Hai kakataa katakata kutoa Fedha 100m sasa kwanini wengine wametoa?Nadhani hata wa Jimbo la SIHA watakuwa wameshatoa.
 
Uchaguzi wamuondoamkurugenzi wa Hai Wednesday, 29 September 2010 18:55 0diggsdigg

Daniel Mjema, Moshi
MKURUGENZI mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Nicholaus Mtega ameondolewa ghafla katika wadhifa huo na kuhamishiwa makao makuu ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) mjini Dodoma.

Uhamisho wa Mtega, ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, unaonekana kuwachanganya watumishi wengi wa halmashauri hiyo, hasa kutokana na uvumi kuwa uhamisho wake una msukumo wa kisiasa.
Uhamisho wa mkurugenzi ni wa tatu kufanywa kwa watumishi wa serikali katika mazingira yanayohusishwa na uchaguzi mkuu baada ya mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Raphael Mbunda kupata uhamisho siku chache baada ya kutupilia mbali pingamizi la CCM dhidi ya mgombea wa Chadema wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema.

Pia kamanda wa Takukuru wa Kilimanjaro, Alexander Budigira alishushwa cheo katika mazingira ya kutatanisha siku chache baada ya maofisa wake kumkamata mkuu wa wilaya ya Kasulu, Betty Machangu kwa tuhuma za kuhusika katika vitendo vya rushwa wakati wa mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM.

Habari zilizopatikana jana zinaeleza kuwa Mtega pia ameondolewa ghafla kwenye cheo chake wakati masuala ya uchaguzi yakizidi kupamba moto. Nafasi yake imechukuliwa na Melkizedeck Humba ambaye alikuwa afisa mipango wa Wilaya ya Same na jana aliripoti ofisini na kukabidhiwa ofisi.
Waziri wa Tamisemi, Celina Kombani hakupatikana kutoa ufafanuzi wa sababu ya kuhamishwa ghafla kwa mkurugenzi huyo wakati huu ambao wakurugenzi wa halmashauri ni nyenzo muhimu kwenye uchaguzi mkuu, lakini Mtega mwenyewe alikiri kuwa amehamishwa baada ya kubanwa sana.
"Hizo sababu unazonieleza kwamba zimechangia uhamisho wangu, mimi sizijui ndio kwanza nazisikia kwako lakini nataka nikuambie barua yangu imesema tu imeamuliwa uhamishiwe Dodoma basi," alisema Mtega.
Mtega alisema sababu zilizoelezwa katika barua yake hazionyeshi kama uhamisho huo ni wa adhabu bali ni wa kawaida na kwamba kama unavyoteuliwa hakuuliza sababu za uteuzi wake hata hilo hana sababu ya kuulizia.
Lakini vyanzo mbalimbali vimeidokeza Mwananchi kuwa tangu Mtega alitupilie mbali pingamizi la CCM dhidi ya mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema, Freeman Mbowe amekuwa akionekana kama msaliti kwa chama hicho tawala.

Pingamizi hilo ambalo kama lingekubaliwa lingeweza kuifanya CCM ipate ushindi mwepesi, liliwasilishwa na mgombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho, Fuya Kimbita.

Kimbita alimwekea Mbowe pingamizi hilo akidai amekwepa kulipa kodi zinazofikia Sh40 milioni kwenye hoteli yake ya kitalii ya Protea Aishi anayoimiliki, pingamizi ambalo lilitupwa baada ya Mbowe kuwasilisha utetezi wake.
Mbali na suala hilo, inadaiwa kuwa kigogo mmoja wa serikali wa ngazi ya wilaya (jina tunalo) amekuwa akimchukulia Mtega kama mfuasi wa vyama vya upinzani kwa kuwa amekuwa akikataa maombi mengi ya kuisaidia CCM.
"Nakwambia uhamisho wake una mkono wa huyo kigogo... ndiye amejenga hoja kuwa kwa vile Mtega anakataa kusaidia kuipa CCM mafuta ya kampeni, lazima ni (mfuasi wa) Chadema na huyo kigogo amekuwa akitamka hayo waziwazi," alidokeza mpashaji wetu wa habari hiyo.
Fitina nyingine anayodaiwa kuzushwa na kigogo huyo pamoja na baadhi ya viongozi wa CCM ni kwamba msimamizi huyo alihudhuria mkutano wa kampeni wa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa wakati alipozuru wilaya hiyo.
"Wanadai eti alihudhuria mkutano wa Dk Slaa, lakini akakacha ule wa mgombea urais wa CCM (Jakaya Kikwete)... sisi watumishi tumeshtushwa sana na tuhuma hii ya uongo na ya kutungwa dhidi ya Mtega," alidai mtumishi mmoja.
Watumishi hao ambao waliomba majina yao yahifadhiwe, walidai kuwa siku Kikwete alipofika Uwanja wa Bomang'ombe wilayani humo, Mtega alikuwepo uwanjani akiwa kwenye gari la halmashauri na watumishi wengine.

Lakini, duru nyingine zilidai kutosainiwa kwa mkataba kati ya halmashauri na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini wa kuipandisha hadhi Hospitali ya Machame kuwa teule nako kumechangia.
Vyanzo hivyo vimeidokeza Mwananchi kuwa Kikwete alitoa agizo hilo mwaka 2007, lakini mkataba huo haukusainiwa baada ya KKKT kushindwa kutimiza masharti muhimu, ikiwamo idadi ya watumishi waliokuwa wanatakiwa.

Inadaiwa KKKT walichukulia agizo hilo la halmashauri la kutaka vigezo hivyo muhimu vya kisheria vitimizwe kwanza kabla ya kusainiwa kwa mkataba kama ni usumbufu na kuandika barua nzito ya kulalamika kwenda Ikulu.
Habari hizo zinadai kuwa CCM wanachukulia kutosainiwa kwa mkataba huo kuwa huenda kukainyima kura hasa baada ya askofu wa dayosisi hiyo, Dk Martin Shao kulalamika hadharani kuhusu kutekelezwa kwa agizo hilo la rais.
Source Mwananchi
 
Back
Top Bottom