Hatimaye aliyemchinja yule kada wa CHADEMA Arumeru akamatwa!

Status
Not open for further replies.

Umenena sawa kabisa mkuu,

Huo wekundu wa maandishi waonesha jinsi gani CCM inavyofadhili siasa za UMWAGAJI DAMU!

Yawezekana SHIBUDA anahusika pia, sindo alikuwa anawapelelezea CCM maisha ya huyo m'kiti wa CDM?
 

Wanajua kuwa kauli walizotoa kina Nape kabla ya kuwa na facts zinaiweka CCM pabaya sana. Na CCM wasingependa kuona watu hawa wanakamatwa kama wanahusiana na chama chao ila hawana jinsi kama wanataka watu waendelee kuwa watulivu na kuamini vyombo vya dola kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake.

Ni ukweli kuwa DUBWANA kubwa huwa halifi bila kutupatupa miguu, na katika kutupatupa miguu ni lazima litajeruhi na hata kuua wale waliolizunguuka. Ni wakati sasa kwa CCM kukubali kuwa ili amani na utulivu viendelee waanze kufundisha makada wao wao mioyo ya kukubali kushindwa katika chaguzi, kwani ukishindwa leo utashinda kesho ndiyo maana ya demokrasia.
 
Dah....watu wana roho ngumu sana. Yaani mpaka kuchinjana kwa sababu ya siasa tu!

hapo sasa wakat wanasiasa wenyewe wanacheza rhumba pamoja na wanaitafuna keki ya taifa pamoja,,,,wanakwenda india kwa zamu muda mwingine pamoja,,,sisi tunabaki kubanana mwananyamala na muhimbili
 
Umeisoma vizuri hiyo taarifa wewe? Kwa kukusaidia tu ni kuwa huyo mpangaji "aliajiriwa" na mwenyekiti wa kijiji kufanya hayo mauaji kwa ujira wa sh. 2,000,000/-.



Na hajalipwa hela yake yote Bado sasa kalipwa Million Moja tu
 
Qwka picha zao nami niwajua bhana,japo si kamanda
Jamani huu ndio mpango wa CCM kwa sasa! Wanakodi wahuni kuwapiga wanaowapinga kwa hoja ili kuzuia wimbi la mabadiliko, Makamanda muwe macho saana. Nasema hivi kwa sababu ninawajua vizuri.
 
Dah! Yaani hadi mwili umesisimka. Kuna watu makatili sana, yaani mashine ya kukatia miti inatumika kukatia binadamu!?
Ahojiwe vizuri huyo jamaa, zana zote hizo tena za kutisha huwa anafanyia nini. Huenda ameshatoa roho za watu wengi sana.

hapo ndugu ndo utaona uzumbukuku wa CCM, wanawanyima watu elimu ili kuwarubuni na 2mil kuua wenzio......!
sasa hawa vijana wanakesha kny kumbi za VIDEO wanaiga muaji ya ACTION za kny moving wakidhani kule wanaua kweli, wao huku wanapractice reality....NI UMASKINI sababu ya NYINYIEM!
 
Waulizeni wasira,nape , mkapa na mwigulu walitaka hivyo..... Nashauri awekwa katika mashujaa wa wapigania mabadiliko
 
Nae achinjwe kama alivyomchinja mwenzie..



 
Mhe Kiongozi wetu mkuu Dr Slaa,

huo ushauri hapo chini kwenye wino wa Bluu uliokolea naomba ukauchukue na kuufanyia kazi mwenyewe.

Ni kweli tena ni haki tukatengeneza mabango ya
MASHUJAA WA MABADILIKO YA PILI Tanzania na kuyaweka sehemu ya wazi ili jamii yetu ipate kuwatambua na kuwapa heshima stahiki.


Waulizeni wasira,nape , mkapa na mwigulu walitaka hivyo..... Nashauri awekwa katika mashujaa wa wapigania mabadiliko
 
Haya mambo ukimfanyia mwenzio hapa duniani utalipwa hapahapa duniani, huyo jamaa kazoea kuua sasa Mungu kamdhalilisha alipokanyaga ni pabaya

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
naanza kuwa na wasiwasi, kama katika ngazi ya jimbo wamefanya hayo je ikitokea wakashindwa kitaifa itakuwaje!? Mungu apishe mbali
 
T.2015.CDM na Wana JF,
Kwanza Poleni wote walioguswa na Msiba huu,
Pili naipongeza Polisi kwa kazi nzuri ya kuwakamata na kumkamata mtuhumiwa, wasihiishie hapo wapate maelezo yake zaidi maana inaonekana kuna watu waliomtuma.
Tatu Maandiko yanasema auaye kwa Upanga.........
Nne iwe fundisho kwa wengine, 2m zinamfanya mtu akose Uungwana na UTU.
My Take: Inasikitisha kila siku Viongozi wetu wanahubiri Amani, Upendo, Utulivu na huku nyuma ya pazia kuna maswali yanayohitaji majibu. Ni matumaini yangu suala hili halitashughulikiwa kisiasa, sheria zifuate mkondo, timu nzima itajwe na adhabu kali kwa wahusika wote ifuatwe.
Nawakilisha




 
Huyo ndio mwenye Blue print ya mambo mengi atueleze kuhusu mpango wao.


 
Pongezi kwa jeshi letu la polisi kwa kufanya kazi yenu kwa umakini mkubwa na kumkamata mtuhumiwa.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…