Leo Jumanne tar.28-08-2012 majira ya saa4 hivi za ASUBUHI chama chetu cha ADC kilichojizolea umaarufu mkubwa katika Nyanja za Siasa NCHINI Tanzania hata Kabla ya kuanza rasmi kazi za kisiasa, kimefanikiwa kupata usajili WA kudumu baada ya kukamilisha zoezi la UHAKIKI katika mikoa kumi (10).
Mikoa iliyohakikiwa na ofisi ya Msajili WA vyama vya Siasa CHINI ya MHE. john Tendwa ni pamoja na Tanga, Mwanza, Pemba, Mara, Unguja, Tabora, Dodoma, Lindi, Mtwara na Dar ES Salaam ambapo chama kilifanikiwa kuvuka idadi iliyo kuwa inahitajika na ofisi ya Msajili ya wanachama wadhamini 200 kwa kila Mkoa.
Tukio hili la kihistoria linaashiria mwanzo WA Harakati za chama cha ADC katika duru la Siasa NCHINI Tanzania, Kama ambavyo moja kati ya Madhumuni yake kuwa (1) Kushika dola kwa njia halali na za kidemokrasia.
GOD BLESS ALLIANCE FOR DEMOCRATIC CHANGE.
ADC - DIRA ya Mtanzania.