Hatimae wanaanga waondoka Duniani kuelekea Mwezini

Mkuu kama mpaka kwa Dunia hii ya Innovation bado tutaachwa basi hatustahili kuishi kwenye huu ulimwengu

Watatuacha ila sio saana kama enzi za mawe
Innovation is life huu msemo uko na unafanya kazi Kwa wenzetu, Sisi tunasubiria Yesu aje atuchukue atupeleke mbinguni.

Hata zama za mawe watu wanasema Afrika ilikuwa na nguvu kubwa sana, ukiuliza nguvu zenu zilienda wapi wanaanza kumlaumu mzungu,
Sasa kama una nguvu na unashindwa kuzilinda nguvu zako hizo ni nguvu au udhaifu
 
Totally wrong, ni mmoja kati ya wanaanga waliokaa anga za mbali kwa muda mrefu zaidi so ana uzoefu wa kutosha na hiyo kazi.

Wabongo tunawazaga mizagamuano tu ndio maana hata project zenu hazifanikiwi.

Unakuta kampuni flani inatuma watu kadhaa mkafanye utafiti labda sehemu flan ya Tanzania na mnagawanywa kwa group la watu wawili wawili na kwenye kundi kuwe na manzi mmoja, huyo manzi atagombewa aende na kila mtu na hata kuna jitu linaweza onga hela ili apangiwe na yeye.

Hapo hakuna mizagamuano mzee, ni full kazi

Hivi watu mnajuanaje jinsia zenu humu jukwaani? Kwa kuangalia avatar au mwandiko?

ISijekuwa unaemwita mama ni babako mdogo
Unatumia muda wako kumuelewesha mtu aliyechagua kuwa mpumbavu!
 
Hivi tuna waafrika wenye brain pawa za namna hii? Au za kuibia umma tu na hata kuiba kwenyewe ni kijinga tu kwa kulindwa na masystem yao!

Nasoma na kurudia hiyo process nakosa kujua uwezo wa akili ya hawa binadamu na kufikiria waafrika tunavyouana kama mbuzi wa kuchoma, tutafikia huu uwezo mwaka gani? Yesu akirudi? Probably kule firdaus tutakapopewa bikra 72 tukilala nazo kwa zamu? I don't know.

My dirty thinking though...
Unajua bibilia inatuita KONDOO?
 
Artemis II: Safari hatari na ya kihistoria, binadamu wanarejea Mwezini baada ya miaka 50.

Kwa mara ya kwanza katika zaidi ya miaka 50, binadamu anarudi Mwezini, akisafiri zaidi kutoka Duniani kuliko mtu mwingine yeyote aliyewahi kuwa hapo awali.

Wanaanga wanne watafanya safari ya zaidi ya maili nusu milioni kuzunguka sayari na kurudi nyumbani katika misheni iliyojaa mshangao, lakini pia hatari.

Misheni ya Nasa ya Artemis II, ambayo imepangwa kuzinduliwa mara tu Aprili 1, itatuletea mandhari nzuri ya Mwezi na uelewa mpya wa mazingira ya mwezi.

Pia itafungua njia ya kutua na, hatimaye, kituo cha Mwezi, hatua yetu ya kwanza katika kujifunza jinsi ya kuishi katika ulimwengu mwingine.

Lakini safari hiyo inakuja na hatari kubwa, wafanyakazi wataruka katika chombo cha angani ambacho hakijawahi kutumiwa na wanadamu hapo awali.

Na kutakuwa na changamoto za binafsi: wanaanga watatumia siku 10 wakiwa wamebanwa pamoja katika chombo cha angani chenye ukubwa wa basi.

Ni roketi yenye nguvu zaidi kuwahi kuundwa na shirika la anga la Marekani na itaanzia kutoka Kituo cha Anga cha Kennedy huko Cape Canaveral, Florida.

Ikiwa na urefu wa mita 98 (futi 322) SLS imewahi kuruka mara moja tu hapo awali, ikirushwa mwaka wa 2022 kwa ajili ya Artemis I bila wanaanga kuingia ndani.

Ina roketi mbili kubwa za usaidizi na injini nne zinazotoa nguvu ya kuruka kutoka ardhini.

Kiini cha chungwa kimsingi ni tangi kubwa la mafuta, lenye zaidi ya lita milioni tatu za hidrojeni oevu na oksijeni oevu.

Kazi ya SLS ni kubeba chombo cha anga cha Orion, ambacho kiko juu ya roketi huku wanaanga wakiwa ndani, hadi angani.

Ikiwa kitu kitakwenda vibaya wakati wa hatua za mwanzo za kuruka, Mfumo wa Usalama wa chombo cha anga , ulio juu kabisa ya roketi, utawapeleka wanaanga hadi mahali salama.

Wanaanga wote wanasema walikaa chini na familia zao kuzungumzia hatari zinazoweza kuwakabili.

Rubani wa misheni anasema, "Sote tuna mtu, mwanaanga, ambaye atakuwa na wanafamilia wetu wanapotazama kuanza kwa safari, ambayo inaweza kuwa wakati mzuri na wa kutisha kwa wakati mmoja."

Wanaanga
Glover ni mmoja wa wanaanga wanne, Wamarekani watatu na Mcanada mmoja , ambao wamekuwa wakifanya mazoezi ya Artemis II kwa zaidi ya miaka miwili.

Wana uzoefu wa miongo kadhaa, ingawa mmoja hajawahi kwenda angani hapo awali.

Unapowaona pamoja, ni wazi jinsi wanavyojuana, na wanavyopendana. Kamanda Reid Wiseman amesema wanne hao wametumia muda mwingi pamoja, sasa wanaelewana kikamilifu.

"Unafikia hatua ambapo huna haja ya kuwasiliana tena, unasikiliza tu kila kitu kinachotokea, na sisi sote wanne hatuhitaji kuzungumza, tunajua tu."

Maisha ndani ya chombo cha anga cha Orion
Wanaanga watatumia misheni yao ya siku 10 wakiwa ndani ya chombo, ambacho kina upana wa takribani mita 5 na urefu wa mita 3.

Ili kuzoea kuishi katika nafasi ndogo kama hiyo, wafanyakazi wamekuwa wakitumia muda mwingi iwezekanavyo wakiwa pamoja. Kumekuwa na hata baadhi ya watu wanaolala Artemis.

Moduli ya wafanyakazi inafanana na ile iliyotumika kwa misheni za Apollo miaka 50 iliyopita, lakini mambo ya ndani ni tofauti sana.

Ndani ya nafasi hii ndogo ya kuishi, hao wanne watafanya kazi, watafanya mazoezi, watakula na kulala.

Kuna tenki, kwa ajili ya maji ya kunywa na kurudisha maji mwilini kwenye chakula.

Misheni ya kwenda Mwezini na kurudi itachukua siku 10 hivi ni kwa sababu inategemea wakati halisi wa uzinduzi, na nafasi zinazohusiana za Dunia na Mwezi.

Kwa siku ya kwanza ya misheni, wanaanga watazunguka Dunia. Watakuwa juu yake kama kilomita 70,000) . Ili kuweka hilo katika mtazamo, Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu kiko kama kilomita 400 (maili 250) juu ya sayari yetu.

Watalazimika kuzoea mazingira yasiyo na uzito, na kwa mgeni wa angani Jeremy Hansen itakuwa mazingira magumu kujifunza.

"Nadhani itakuwa marekebisho kidogo kwetu tutakapofika huko juu ... Nitakuwa nikijifunza jinsi ya kuelea na kuruka na kukutana na vitu. Na labda nitahitaji msaada kidogo," alisema Jeremy Hansen, mtaalamu wa misheni.

Wanaanga pia watakuwa wakiangalia mifumo muhimu ya usaidizi wa maisha ya chombo cha angani na hii inajumuisha choo cha ndani.

Wanaanga pia watapata nafasi ya kuipeleka Orion kwa jaribio lake la kwanza.

Baada ya takriban saa tatu tangu kuruka, sehemu ya juu ya roketi hutengana, na wahudumu huendesha chombo cha angani kwa mikono wakikaribia na kuondoka tena ili kufanya mazoezi ya kukidhibiti na kukiunganisha katika misheni za baadaye.

Kwa siku ya kwanza ya misheni, wanaanga watazunguka Dunia
Sasa timu ya Artemis inapaswa kufanya uamuzi mkubwa.

Ingawa wanaanga wako karibu na Dunia, kurudi ni rahisi sana ikiwa kuna masuala yoyote ambayo hayawezi kutatuliwa.

Kituo cha udhibiti wa misheni lazima kiwe na uhakika kabisa kwamba kila kitu kiko salama kabla ya kuruhusu mchakato muhimu wa kuwasha injini unaosukuma chombo cha angani kuelekea Mwezini.

Huu ni wakati ambapo chombo cha angani kinatumia injini yake kuu kujinasua kutoka kwenye nguvu ya uvutano ya Dunia na kuelekea Mwezini.

Mara tu watakapokuwa njiani, kurudi nyumbani haItakuwa rahisi au haraka, wanaanga sasa wamejitolea kwa safari yao ndefu kuzunguka Mwezi na kurudi.

Wakati huu, wafanyakazi wataendelea kutathmini mifumo ya vyombo vya anga, lakini wanaanga wenyewe pia watatathminiwa na kufuatiliwa.

Ni fursa ya kuwatumia wafanyakazi kama ndege wa Guinea, majaribio yaliyo kwenye chombo yataonesha jinsi miili yao inavyoathiriwa mbali sana angani.

Mionzi ni jambo muhimu, kwani Jua linaweza kutoa chembe zenye uharibifu na zenye nguvu nyingi.

Wanaanga watabeba kifaa kinachoitwa dosimeter ili kuona ni mionzi mingapi wanayopata.

Wafanyakazi wanahitaji kujua jinsi ya kuingia haraka ikiwa dhoruba ya jua litawafikia.

Kipindi kingine cha mazoezi cha kusaidia kujiandaa kwa yasiyotarajiwa kitawahusisha wanaanga kufanya mazoezi ya kuvaa mavazi yao ya anga ya rangi ya machungwa ili kujitayarisha kwa dharura.

Safari hatari ya kurudi
Kurudi kutachukua siku nyingine nne. Lakini sehemu hii ya mwisho ya misheni ni mojawapo ya hatari zaidi.

Katika hatua ya mwisho, kapsuli ya wahudumu hutengana na sehemu nyingine ya chombo, kisha inajizungusha ili ngao yake ya joto ikabiliane na joto kali, na baadaye inaingia tena katika anga ya Dunia kwa kasi kubwa huku ikiwalinda wanaanga dhidi ya joto kali sana.

Chombo cha angani kinapopita salama, parachuti kadhaa hutolewa ili kukipunguza mwendo.

Wanaanga watatua taratibu baharini katika Bahari ya Pasifiki karibu na pwani ya California, ambapo timu ya uokoaji itakuwa ikisubiri.

Kapsuli inaweza kutua ikiwa wima, ikiwa imegeuka juu chini au ikiwa imejilalia upande, na mifuko ya hewa ya rangi ya machungwa itajaa ili kusaidia kukirekebisha kiwe wima ili wahudumu waweze kutoka salama.

Credit: Bbc

Veri denjaraz 😳😳😳
 
Isije kuwa studio setup kama ile ya apollo.
Mkuu hii kitu kila hatua ilikuwa live na wananchi wameshuhudia kila pande ya Dunia na hata baadhi waliokuwa karibu na eneo la kurushia roketi.

Kiukweli wenzetu wapo mbali sana, then kilichonishangaza hakukuwa na raisi wala mbunge au waziri wakati roketi inaondoka. Huku roketi inarushwa na raisi yupo zake huko na waandishi wa habari anazungumzia vita ya Iran.

Wenzetu taaluma wameacha wafanya wanataaluma wenyewe, ingekuwa huku kwetu shughuli zote zingesimama na rais angekuwa mgeni rasmi na angeenda na msululu wa viongozi wa serikali na kidini na wangelipana posho kwa kazi ambayo hawaielewi wala kuijua.

Kwakweli wazungu wapo far sana.
 
Mkuu,
Sijadanganya watu bali nimesema historia itabakia hivyo
Ni kweli ila watu wamejua ukweli kua yule boya hakuenda mwezini..it was all propaganda ambapo walifanya hivyo sababu walishaona Kuna nchi Fulani wewe unaijua walikua wanakaribia kufanikisha Hilo, na kama unavyojua Hawa maibilisi worshipers hua wanataka kua wa kwanza kwa kila jambo sababu za pride, kujionesha umwamba, kujionesha supa pawa , siasa n.k..
 
Hivi tuna waafrika wenye brain pawa za namna hii? Au za kuibia umma tu na kuuana Kama wanyama pori na hata kuiba kwenyewe ni kijinga tu kwa kulindwa na masystem yao!

Nasoma na kurudia hiyo process nakosa kujua uwezo wa akili ya hawa binadamu na kufikiria waafrika tunavyouana kama mbuzi wa kuchoma, tutafikia huu uwezo mwaka gani? Yesu akirudi? Probably kule firdaus tutakapopewa bikra 72 tukilala nazo kwa zamu? I don't know.

My dirty thinking though...

Mkuu, japo hitimisho lako limekaa kiwaki ila una hoja..

Sio wewe tu uliyefikiria na kusoma mara mbili mbili, mimi pia nimejikuta kwenye tafakari nzito juu ya uwezo wa akili za hawa jamaa. Ukisoma mchakato wote wa namna chombo kinavyofanya kazi unagudungua akili iliyotumika ni ya juu sio kidogo.

Nilikuwa najiuliza hizo siku kumi za kusafiri chombo hakitaishiwa mafuta? Nakutana na mambo ya Hydrogen oevu na Oxygen oevu lita milioni kadhaa..

Haya mambo tutakuja kufanya baadae sana kwa sasa acha tuendelee kuuwana kama mbuzi tu.
 
Kwahio tunakubaliana kua Hawa watu hawakwenda mwezini kipindi kile ilikua danganya toto walienda sehem flan jangwani wakapiga picha na kutengeneza video za uongo, mana huwez niambia kua eti baada ya miaka 50 Ndio wanarudi tena. ..watu walioenda mwezini ni warusi na wachina tu.
Wachina na Warusi walienda mwezini mwaka gani?
 
Ni kweli ila watu wamejua ukweli kua yule boya hakuenda mwezini..it was all propaganda ambapo walifanya hivyo sababu walishaona Kuna nchi Fulani wewe unaijua walikua wanakaribia kufanikisha Hilo, na kama unavyojua Hawa maibilisi worshipers hua wanataka kua wa kwanza kwa kila jambo sababu za pride, kujionesha umwamba, kujionesha supa pawa , siasa n.k..
Neil Armstrong na Buzz Aldrin walishawahi kwenda mwezini na watu walishuhudia kama ilivyokuwa jana. Hata tukio la jana kuna watu wanasema ni uongo.
 
Hivi tuna waafrika wenye brain pawa za namna hii? Au za kuibia umma tu na kuuana Kama wanyama pori na hata kuiba kwenyewe ni kijinga tu kwa kulindwa na masystem yao!

Nasoma na kurudia hiyo process nakosa kujua uwezo wa akili ya hawa binadamu na kufikiria waafrika tunavyouana kama mbuzi wa kuchoma, tutafikia huu uwezo mwaka gani? Yesu akirudi? Probably kule firdaus tutakapopewa bikra 72 tukilala nazo kwa zamu? I don't know.

My dirty thinking though...
wapi ulisoma kuna bikra 72 firdaws , ?? lete reference mkuu
 
Back
Top Bottom