Hatimae utabiri wa mwaka 1995 umetimia, muda ni rafiki wa kweli

Hatimae utabiri wa mwaka 1995 umetimia, muda ni rafiki wa kweli

Subira the princess

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2018
Posts
4,465
Reaction score
4,613
Wasalaam.

Mwaka 1995 Baba wa taifa hayati mwl J.K. Nyerere akiwahutubia wajumbe wa CCM alisema, nanukuu "CCM inapomtangaza mgombea urais katika uchaguzi wa rais, ni kwamba wanamtamka rais ajae wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini huyo anataka urais asiutake kwa siri bali aje aseme mbele ya wajumbe ili wampime".

Akasema, ni lazima mtu huyo apate baraka za wajumbe wa CCM na sio kujipitisha chini chini ili yule rais mtarajiwa akapate kusikiliza maoni ya wananchi sambamba na maoni ya vyama vya siasa, CUF na Chadema na NCCR Mageuzi pamoja na vyama vingine.

Pia akasema, mgombea huyo urais wa CCM asiwe mkabila wala mkaburu.

Leo ni 2025 na maneno haya ya mwl bado yanaishi na yataishi vizazi na vizazi. Ni mwongozi na onyo kwa CCM, wajumbe wa CCM na viongozi wa vyama vya upinzani kujitafakari wakati wa uchaguzi wa rais.

Kuna watu ndani ya CCM bado wanaziishi na kuziamini hizi falsafa za Baba wa taifa mfano hayati rais Magufuli, mh Polepole, Luaga Mpina, Pastor, na jamii ya watu kama kina Tundu Lissu japo Mh Polepole kaenda mbali zaidi na uvumilivu umekoma kaamua kuiishi kauli mbiu ya tanu "NITASEMA UKWELI DAIMA FITNA KWANGU MWIKO."

Sikiliza hii video huenda tukakumbuka uzalendo ni nini, hasa sisi wanaccm.
 
Back
Top Bottom