Hatimae nimeamua kuoa

Magnificient

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
1,177
Reaction score
734
Natumai ndugu zangu nyote wa MMU ni wazima, nami namshukuru MUNGU.

Baada ya kuwa na mpenzi wangu kwa muda kila mtu akiishi kwao kwa wazazi wake (takribani miezi 6 sasa) tumeridhia kuwa tunaendana na sasa tunaweza tukaoana na kuishi pamoja. Hapa nina amani kiasi na utulivu wa moyo sasa, isipokuwa tu sijajua muundo wa barua ya posa; anayejua tafadhali anisaidie mapemaaa tusije tukaandika barua ya kiofisi au ya kirafiki kama hizi tulizozoea kuombea kazi.

Pia nakaribisha maoni na ushauri juu ya mchakato mzima wa kuchumbia na kuoa, nikiwa na imani kuwa hapa MMU ndipo penyewe, kila kitu ni live bila chenga.

Natarajia kupeleka barua tarehe 10.05.2014, ingawa mshenga sijaconfirm kati ya rafiki yangu au kaka yangu kama hakuna tatizo.

Au hadi nimpate mzee? Kila kitu kinakaribishwa. Nawatakieni siku njema!
 
1. Unaoa kabila gani?
Kila kabila lina taratibu zake za namna ya kuwasilisha barua ya posa na posa yenyewe. Yapo makabila ambayo binti hupeleka nyumbani barua ikiwa na posa, yapo ambayo mshenga hupeleka barua yenye posa na wazazi huongea na binti n.k

2. Barua ya posa huwa na format ya kawaida isipokuwa ipo kama ya kiofisi ikiwa na heading, wahusika watakiwao kuipokea(wakwe) na lengo kuu la barua n.k.

3. Mshenga si lazima wawe hao wawili uliowataja, jaribu kutafuta mtu anayeijua vizuri familia yao au ukoo au kabila lao maana atakusaidia sana kwenye kupanga mahari.
 
Familia ya Bw & Bi [Jina la Baba wa binti]
Kinondoni, Dar es Salaam.

Wazazi wapendwa,

YAH: KUMPOSA BINTI YENU.

Rejea taarifa tajwa hapo juu.

Mimi Magnificient wa Tegeta Dar es Salaam ninayo heshima kubwa kuleta kwenu maombi ya kumposa binti yenu [Jina la Binti] kufuatana na utaratibu wa familia.

Naambatanisha barua hii na kishika uchumba/posa ya [Taja kiasi cha pesa uliyoweka].

Wenu mwanenu mtarajiwa,

Magnificient.
 
Kila la heri mdau katika kuliendea hilo jambo.
 
Ombi langu:- thread kama hizi ziwe nyingi nyingi japo ata tatu kwa siku ili wale masingula angalia tupate moyo.
Kila la heri kaka
Kwendraaaaa kama hujapata moyo na upo nae mnakula raha za dunia ndo thread itakupa moyo
ha ha ha umeongea kwa huruma, pole
 

CC:#mkoroshokigori na babu Dr. #Mzizimkavu
 
Kwendraaaaa kama hujapata moyo na upo nae mnakula raha za dunia ndo thread itakupa moyo
ha ha ha umeongea kwa huruma, pole

Nikiona thread kama hizi na mm nakua na mawazo hayo. Leta basi na wewe nzuri nzuri
 

Umenikumbusha wallahi.....natamani kama niposwe tena hihihihihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…