Hatimae Naona Kama 1+1 = 2 Inaleta Maana


C

chige

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Messages
8,375
Likes
16,069
Points
280
C

chige

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2016
8,375 16,069 280
Nimesikiliza interview ya Ommy Dimpoz... watu wanadai wamemwelewa lakini mimi SIJAMUELEWA!

Katika kuonesha kwamba tatizo ni Diamond, Ommy Dimpoz anatoa simulizi ya Diamond "kumbania" collabo na Iyanya pamoja na Davido! Tukianza na suala la Davido; Ommy Dimpoz anamnukuu Sallam akisema ".. basi poa lakini safari hii lazima ulipe... tulikusaidia kwa J Martin lakini sasa lazima ulipe!" (Sikiliza kuanzia Dakika 15:30-15:38).


Hapa huhitaji kuwa na digrii kufahamu kwamba kumbe collabo ya Ommy Dimpoz na J Martins jamaa (Dimpoz) alifanya bure!

God forbid, mwanaume UNASAIDIWA collabo... serious?! Hivi kweli J Martins anaweza kufanya collabo FOR FREE? If not; nani alimlipia Ommy Dimpoz hiyo collabo?! Wakati ule tayari Ommy Dimpoz alishakuwa msanii mkubwa tu hapa Tanzania ambae asingeshindwa kumlipa J Martins... halafu anapata FREE INTERNATIONAL COLLABO tena kutoka kwa M-Nigeria aliyeapa kutafuta pesa kwa udi na ubani!!!!

Mungu kiokoe kizazi chako... kama naanza kumuelewa Diamond aliposema "tunakufichia mengi!" Kauli ambayo awali niliipuuza!

Anyway, collabo ya Davido na Ommy Dimpoz haikufanyika kwavile Diamond alibania! Watu wanapotosha kwamba eti Diamond alipanda dau! Ukisiliza hiyo video, baada ya Davido kuja kwenye Fiesta; Diamond akawasiliana na Sallam na kuomba collabo na Davido ndipo Sallam akasema $5000 na Diamond akasema poa (sikiliza Dakika 16:00-16:07)!!

Kwahiyo sio kwamba Diamond alipanda dau bali baada ya yeye kuomba collabo, Sallam ndo akataja hiyo $5000.

Anyway, nadhani watu wamesahau tu! April mwaka huu kulikuwa na uzi humu JF ambao ulihusu mahojiano na Sallam na point of interest hapa ni pale Diamond alipofanya kazi na Davido! Mwandishi wa Champion anamuuliza Sallam walivyokutana na Diamond kisha Sallam anajibu

Kwa kuwa nilikuwa tayari nina ‘connections’ zangu, mwaka 2013 nilipata tenda ya Clouds FM kuwaleta kina Iyanya, Jay Martins na Davido kwenye Fiesta nikiwa wakala, nikapewa hela yangu tukamalizana.

Baadaye Diamond akanipigia simu akasema anataka kufanya kazi na Davido, nikampa masharti yangu akayakubali, nikazungumza na menejimenti ya Davido, tukaelewana, kesho yake ikaenda kufanywa remix ya Number One.
Sasa hivi kulikuwa na kosa gani hapo?! Ina maana kwavile Dimpoz alisha-book collabo na Davido ndo basi haikutakiwa msanii mwingine kufanya collabo na Davido? Ni mambo ya wapi hayo? Mbona Ommy Dimpoz huyo huyo alifanya collabo na J Martins ambae alishakuwa amefanya collabo na AY/Mwana FA? Mbona C Pwaa alifanya kazi na Ms. Triniti na AY alivyonogewa na yeye akafanya nae kazi huyo huyo Ms. Triniti? Mbona AKA kafanya kazi na Diamond wakati Diamond huyo huyo alishafanya kazi na wasanii wengine wa South Africa?

Kama ni jambo la kawaida, nini kilimfanya Ommy Dimpoz asifanye kazi na Davido? Hivi Diamond wa miaka ile alikuwa na uwezo wa kumwambia Davido asifanye kazi na Dimpoz? Ikiwa Connector (Sallam) alikuwa tayari kwa $3000 za Dimpoz wakati Diamond alimtaka atoe $5000... hivi hii haimaanishi kwamba Sallam alikuwa anam-favor Dimpoz kuliko Diamond?

Narudia; KWANINI HAKUFANYA NAE HATA BAADA YA KUWA AMEFANYA NA DIAMOND? Au ALISUSA? Au hata hiyo $3000 alitaka mtu amlipie kama ambavyo nina wasiwasi huenda alilipiwa kwa J Martins? By the way, hivi kweli Davido wa 2013/2014 ageweza kufanya collabo kwa $3000?! Hivi huu si ndo ulikuwa msimu ambao Davido alikuwa kwenye peak?!

Mashaka yanaedelea! Ukimsikiliza Dakika ya 11:50 - 12:15 Ommy Dimpoz anazungumzia suala la kutaka waende pamoja Marekani ili hatimae Diamond akamfanyie Ommy Dimpoz mpango wa collabo na wasanii wa Marekani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kuna watu wanadai hatimae wamemwelewa Ommy Dimpoz... kwamba, kumbe mshikaji hana noma kabisa! Wale waliomwelewa; naomba wanieleweshe na mimi manake binafsi sijamwelewa kabisa!!!

Hivi kweli Diamond huyu alikuwa na uwezo wa kumtafutia mtu collabo Marekani wakati ule?! Diamond huyu huyu mpenda collabo awe na uwezo wa kumtafutia mtu collabo Marekani wakati mwenyewe alikuwa hajawahi kufanya collabo hata na mtoto wa shule kutoka Marekani!! SERIOUS?!

Hivi si ni Diamond huyu huyu wakati ule alikuwa anamuomba JK awaunganishe na wasanii wa Marekani?! Hivi hata yeye mwenyewe collabo yake ya kwanza na Wasanii wa America; si kaipata juzi tu hapa kwa Ne-Yo and thanks MTV MAMA ambao waliwakutanisha... which means, ni collabo ambayo ilizaliwa hapa hapa Africa...!

Na kwa bahati mzuri, Ne-Yo tena akapata tour ya Coke Studio hapa hapa Afrika!!! Sasa hao wasanii aliokitaka Dimpoz awapandie ndege na Diamond hadi US ni wasanii wa aina gani?! Yaani mtu huna connection nae, huna mawasiliano nae; si ajabu wala sio Follower wake kwenye social networks... hata namba yake ya simu hauna; lakini ghafla tu, unapanda ndege kumuomba collabo... from nowhere!!!!

Hizi kauli zingine zinatufanya watu tuanze ku-connect dots ingawaje hatukutaka kufanya hivyo manake, sioni ni namna gani mtu unataka kupanda ndege kutoka Afrika Mashariki hadi Marekani eti ukatafutiwe collabo from nowhere!! Sijawahi kusikia kitu kama hicho!!! Hivi ni kweli alikuwa anataka akatafutiwe collabo na wasanii wa Marekani au alitaka akafanyishwe COLLABO na Diamond na ndio maana mwenzake akamtoroka?!

Sorry Ommy Dimpoz... kwavile ulijiandaa; umeweza kuwachezea akili wengine lakini binafsi naona kumbe kweli wewe ni tatizo sema ndo vile tena; KUNYA ANYE KUKU! Ingawaje kulikuwa na mitifuano ya chini kwa chini lakini ni wewe ndie uliileta kwenye media kwa mara ya kwanza majuzi uliposema kuna watu wananunua views!

Ni mjinga tu ndie atajifanya hafahamu kwamba ulimlenga nani?! Na kiukweli kabisa INAKERA... mtu una-struggle usiku na mchana hadi wapuuzi wengine wanafikia kusema "hapo alipofikia ni kwa sababu anamgegeda mama ake wa kumzaa....!" Halafu anatokea mpuuzi mwingine anasema "unafanya kazi kiujaujanja...!

" As if hazioni hustle unazopitia! Mtu unalipa mamilioni ya pesa kutengeneza video hadi unatengeneza royal viewers wanaokaa mkao wa kula kusubiria next video; halafu anatokea mjinga mmoja anasema "unanunua views...!" kisha unaenda radio na kujifanya innocent!!!

I am not that dumb...

Sababu kubwa ambayo ilinifanya kumshabikia Donald Trump ni kwavile hakuwa mnafiki... sipendi watu wanafiki! Na ndio maana katika hili namuunga mkono Diamond kwa 100% kwa sababu baada ya kuchoshwa na u-snitch; akaamua kutoa makavu live... ukitaka kumuona Mswahili na Mshari, sawa na ukimuona vinginevyo; POA TU!!!!
 
C

chige

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Messages
8,375
Likes
16,069
Points
280
C

chige

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2016
8,375 16,069 280
kwani kufanya collabo nani kasema lazima kulipana??? me najua ni makubaliano yao, wanaeza taka hela au wasitake...correct me if am wrong...
Nani kaudanganya... unless iwe Collabo sawa na ya Diamond & AKA, au Ommy Dimpoz & Kiba!!
 
C

chige

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Messages
8,375
Likes
16,069
Points
280
C

chige

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2016
8,375 16,069 280
kumbeee, au ile ya kiba na nuh
Kumbukumbu zangu zinaonesha kwamba ile ya Kiba na Nuhu ni Nuhu ft Ali Kiba na sio Nuhu & Ali Kiba! Kama ni Nuhu Ft Ali Kiba ina maana ngoma ni ya Nuhu na Kiba ameshirikishwa tu lakini kwa mfano Ommy Dimpoz & Ali Kiba ile ni ngoma yao kwa pamoja!!
 
scorpio me

scorpio me

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2016
Messages
5,176
Likes
5,981
Points
280
scorpio me

scorpio me

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2016
5,176 5,981 280
Kumbukumbu zangu zinaonesha kwamba ile ya Kiba na Nuhu ni Nuhu ft Ali Kiba na sio Nuhu & Ali Kiba! Kama ni Nuhu Ft Ali Kiba ina maana ngoma ni ya Nuhu na Kiba ameshirikishwa tu lakini kwa mfano Ommy Dimpoz & Ali Kiba ile ni ngoma yao kwa pamoja!!
duh
 
C

chige

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Messages
8,375
Likes
16,069
Points
280
C

chige

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2016
8,375 16,069 280
Povu linatokaaaaa..... asubuh asubuh waacheni wao kwa wao wale warabu wa pembe... bhn
Sasa na wewe kilichokusukuma kuja kuchangia ni nini?!
 
talnam

talnam

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2014
Messages
356
Likes
288
Points
80
talnam

talnam

JF-Expert Member
Joined Nov 13, 2014
356 288 80
Yaan halafu anasema mziki wa ujanja ujanja ile ni hashtag tu, eti hajamtaja mtu kuhusu views kama ni hivyo hata diamond hajamtaja mtu kuhusu kupumuliwa. Mi pia sikuwah kumsikia diamond akimuongelea vibaya kabla ya haya.
 
C

chige

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Messages
8,375
Likes
16,069
Points
280
C

chige

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2016
8,375 16,069 280
Yaan halafu anasema mziki wa ujanja ujanja ile ni hashtag tu, eti hajamtaja mtu kuhusu views kama ni hivyo hata diamond hajamtaja mtu kuhusu kupumuliwa. Mi pia sikuwah kumsikia diamond akimuongelea vibaya kabla ya haya.
TRUE KWA 100%!
 
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
38,495
Likes
51,235
Points
280
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
38,495 51,235 280
Nani kaudanganya... unless iwe Collabo sawa na ya Diamond & AKA, au Ommy Dimpoz & Kiba!!
Acha ushamba wewe.
Inategemea na makubaliano ya mtu.

Johmakini feat. Chidnma ni bure, Johmakini feat. AKA ni bure.
AY na Romeo ni bure, Yemi Alade na saut Sol bure.
Usikariri.

Wasanii wanatumia hii nafasi kutafuta fun base kwenye nchi zingine.

Naomba tu nikupe pole jana Ommy amewa-outsmart mmeonekana vituko mbele ya jamii.
 
zipompa

zipompa

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2014
Messages
5,012
Likes
9,361
Points
280
zipompa

zipompa

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2014
5,012 9,361 280
pale mchambuzi anapo ongozwa na mapenzi, mahaba juu ya mtu flani alafu upande wa 2 ana haisira, wivu, chuki kwa mwingine.

hakuna uchambuzi hapo mkuu ila utoto wa hali ya juu,naamini dimpozi ajasema mengi ndo maana una connect dot za ajabu
 

Forum statistics

Threads 1,274,218
Members 490,631
Posts 30,505,044