Hatimae Mwezi huu (Agosti, 2021) nahamia kwangu ili niwe huru kupiga muziki kwa sauti ya juu

Habari za muda huu wakuu,

Mara nyingi watu wengi hupenda kujenga ili kuepuka kadhia za kudaiwa kodi na wenye nyumba na masharti mengine kibao ila kwa upande wangu mimi hii haijawa sababu kubwa ya kunifanya nitamani kumiliki nyumba yangu hapa mjini,

Mimi kulichonifanya hadi kujenga ni kutamani uhuru wa kusikiliza mziki in maximum volume, yaani my addiction ni kupiga mziki kwa sauti ya juu,

Kwanza hii kitu haijatokea tu from no where, hapana hii tabia ina mizizi iliyoota kwangu longtime sana wakuu,
Picha linaanza kwanza katika mazingira ya ukuaji wangu home hakukuwa na radio wala TV yaani ilikuwa ikitokea nikaona mshkaji anamiliki Radio nilikuwa namtamani sana Kipindi hiko jirani yangu alikuwa na dundo kama mnavyojua kijijini miaka hiyo mtu akimiliki dundo huwa halipigwi mara kwa mara huwa linafunguliwa kwa week mara moja tena kwa matukio maalum mfano siku mifugo ikitoka malishoni ikiwa imeshiba huwa kesho yake mafuta yananunuliwa lita moja kisha dundo linafunguliwa kama kumtia moyo mchungaji ili na kesho ng'ombe walishwe vizuri, au ikitokea mkamaliza palizi, au mavuno hapo dundo hufunguliwa tena ukomo wa dundo huwa linaweza kukatikia katikati ya burudani baada ya genereta kuishiwa zutu, yaani ni shida tupu,

Sasa nilikuwa nikiskia tu mngurumo wa genereta hata kama nipo nakula msosi hapo hamu inakata natoka mbio naenda kunengua, tena genereta likikata hapo ndio furaha imekomea hapo narudi zangu home kinyonge sana,

Hadi nakumbuka siku moja nilisikia dundo limewashwa halafu wameweka lile goma la Bushoke Mme bwege nikaanza kunengua ndani ila baada ya muda nikagundua kama kuna usaliti wa kuino na mwili ndipo nikaamua kukaza mkanda kiunoni ili kukipa nafasi kiuno kuonesha ushirikiano na ile milindimo ya mapigo ya lile dundo,

Basi bana nikakaza ule mkanda hadi ile top point hamna tena uwezo wa kusogea nikakomea pale nikaanza kunengua, na ghafla kama kawaida tena dundo likakata katikati ya minenguo, Kudadeki sitasahau hii kitu maana ule mkanda ndio nilikuwa nimetoka kununua kwa ajili ya kuchomekea uniform,

Kwa middle wahenga wanaokumbuka vile vimkanda tulikuwa tunavuta kwa mbele halafu kwa juu vilikuwa na sumaku, hivyo ukitaka kukaza kuna sehemu ulikuwa unanyanyua kidogo unavuta kisha ukifika unapoona panakufaa unaachia kanabana tena kenyewe, na shart ukitaka kuvua lazima ukavute mbele kidogo kukataftia balance halafu ndio utoe,

Sasa hapa kibarua kilikuja kutoa mkanda maana tayari nilikuwa nimekaza hadi mwisho ili ninengue vilivyo, nyambafu haja nayo isipokuwa na heshima wala huruma ikatia timu katika ile pambana nikaona hapa hamna namna ikabidi nishushe mzigo kwanza ili nipate unafuu wa kupambana na mkanda kwanza

Hayo mengine yatafuata baada ya kuutoa, Basi bana baada ya kumaliza kukata gogo nikiwa na nguo wazo likaja kukata mkanda ila changamoto ulikuwa umeingia kwenye nyama katikati ya kiuno na tumbo, kukawa na ugumu kukata kwa upande wa tumboni kwa mbele upande wa nyuma kati ya mgongo na kiuno ndio kulikuwa na unafuu napo siwezi kukata mwenyewe maana ni upande wa nyuma, sasa nikisema niite msaada nakumbuka kuwa huko nyuma kumechafuka pia hakuna atakae weza kuja kukata na upande mwingine ni aibu pia, aseeh kwa kweli hili tukio sitakaa kulisahau ila yote kwa yote in Babalevo voice ilikuwa ni dundo, hatimae ilibidi tu nijitokeze kutoka mafichoni ili nipate msaada na msaada wenyewe kililetwa kisu wakakata ila kutokana na ule mbanano wa ngozi na mkanda nilipata majeraha ya kisu mwilini ila nilipona japokuwa hadi sasa alama bado ipo,

Sasa maisha yakaendelea hadi nikaona nikienda mjini ndio itakuwa rahisi kumiliki dundo nikaja mjini na kweli mungu sio athuman nikanunua dundo langu mwenyewe lakini bado sina amani kila nikifungulia kidogo makelele kwa majirani kuwa napiga kelele watoto wamelala kwa kweli sijawahi kufurahaia kutimiza ndoto yangu ya kumiliki dundo,

Mimi kujenga hakukuwa katika ndoto yangu ndoto yangu ilikuwa kumiliki mziki mkubwa na tv ila kwa kuwa nimeona bado sifurahii nimeamua kujenga kwangu, na ninatangaza rasmi kuwa kuanzia mwezi wa tisa nitakuwa naishi kwangu na nitakuwa nafungulia HOMTHIETHA yangu sauti ya mwisho kuanzia asubuhi hadi jioni, na nikiona kelele nitafunga soundproof.

Kwa kweli huwa sifurahii sauti ndogo ya mziki hata kidogo. Na nimepata wazo la kununua gari ili niwe nasikiliza mziki kila sehemu hata nikiwa katika Gari langu ila sijajua kama kwenye gari naweza kupata uhakika wa sound ya kutosha, nadhani nikishanunua nitakuja hapa kuomba uzoefu wa aina ya dundo kali linalofaa kwenye gari.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kufungulia mziki mkubwa kwebye gari ni hatari kwa maisha yako, otherwise uwe makini sana barabarani huko.
 
Unaweza kupanga nyumba na ukafungulia HOMTHIETHA yako max volume na Unaweza ukahamia kwako na ukashindwa kusikiliza huo mziki kwa kwa max volume vilevile

Mimi nakupa hongera kwa ujenzi
 
Back
Top Bottom