MTINGIJOLI
JF-Expert Member
- Aug 19, 2014
- 1,460
- 1,476
Habarini Za Mchana Wana JF, Hongereni Kwa Majukumu Ya Siku, NIna Mpenzi Tangu Tumeachana imepita Miezi Kama mitano, Mbaya Hatukuachana Vizuri , Tuliachana kwa Maneno Ya Hapa na Pale (kashfa) kiasi Kilichopelekea Aniblock Kuanzia Kwenye Simu na Mitandao Yote ya Kijamii (Social Networks) So Sikua na Taarifa Zake zozote , Nadhani Hata Zangu hakua Nazo, Ingawa Sina Hakika.
Usiku wa Jana nimepumzika Zangu Sina Hili Wala Lile, Simu Inaingia, Kuangalia ni Namba Ngeni, Huwa Sina Utaratibu wa Kupokeaga Namba Ngeni ila Nikajikuta tu Nimepokea, Mara Sauti Ni Ya Kwake, Na Ana Kasauti Kake Unique Hivi, ( Kama Wema Flani Hivi) Akaanza Mara Upo Kimya Sana, Mama anakukumbuka Sana, Mara Kipindi Sipo Na Wewe Marafiki Zako Walikua Wananitongoza, Mwisho Akaniambia kuwa Alibadilisha Kila Kitu, Hadi Namba Za Simu, Na Ile Ndiyo Namba Yake Mpya Anaitumia.
Hadi Sasa ameniachia Maswali Mengi Yasio Na Majibu, Kwa Nini Jana? Nini Kimemfanya Anikumbuke? Kama Alinidelete Kote?
Naomba Kuwasilisha. Muwe Na Jioni Njema Na Na Weekend Njema