Hatima ya Uchaguzi wa Kenya kwa Siasa za Upinzani Tanzania

Musa Ndambo

Member
Jul 7, 2016
82
103
Uchaguzi wa Kenya unafanyika leo tarehe 9/8/2022

Uchaguzi wa huu una maslahi mapana si tu kwa wa-Kenya bali ukanda mzima wa E Africa, Tanzania tukiwa miongoni mwao

Wakati wa uchaguzi wa 2017 CDM walisamama na Uhuru, akashinda. Mgombea wa CCM, bwana Odinga akiangukia pua

Matokeo yake ndiyo yale tuliyoyaona kwa Shujaa wetu kuanzisha vita ya wazi dhidi ya Uhuru hali iliyopelekea kuchomwa kwa vifaranga nasisi kupigwa ban ya kuuza mahindi kwao

Hali ilifika pabaya sana, Alhamdulilah Mungu aliamua magomvi yetu, yamekwisha sasa!

Jambo kubwa alilofanya Kenyatta kurudisha fadhila kwa CDM ni kitendo cha kumpokea wakili msomi Tundu Lissu ba kumpa matibabu. Thank you Kenyatta

Siasa haina rafiki au adui wa kudumu, its 2022 things do change, Kenyatta aliyepiganiwa na CDM leo ni rafiki mkubwa wa CCM. Bad enough he’s endorsing Raila

Sishangai hadi hii leo siku ya uchaguzi CDM haijatoa msimamo wake wa mgombea wanauemuunga mkono

Je ni vipi matokeo ya uchaguzi wa leo yataathiri siasa ya Tanzania?

Raila Odinga akishinda katika uchaguzi wa leo ni ushindi kwa CCM kwasababu kuu mbili

◦ Walimuunga mkono mwaka 2017
◦ Raila atafanya kazi kwa matakwa ya Kenyatta (ambaye kawa rafiki wa Mhe Samia, CCM)

Pia Raila atakuwa ni Rais wa mhula mmoja na kumuachia kiti Bibi Martha Karua (mshirika wa Kenyatta) kama itakavyokuwa kwa Bwana Biden, USA.

JK kaitwa (na Kenyatta) kama miongoni mwa waangalizi wa Uchaguzi, this is not a coincidence. He’s there to help their man, RO.

Ruto akishinda tutegemee ataanza kufanya mambo kinyume na mtangulizi wake. So perhaps hata urafiki huu wa serikali ya Kenya na Tz huenda ukabadilika

Hii itakuwa ni karata nzuri kwa CDM kuitumia wakati huu wa kudai Katiba Mpya pamoja na Uchaguzi wa 2025 huenda Ruto akatoa msaada kwa CDM

Sifahamu vitu vingi ila nina hakika kama RO akishinda uchaguzi wa leo atahakikisha anafanya lolote awezalo kuisaidia CCM kurudi madarakani 2025

I stand to be corrected (not you, but time)

Asante
 
Bora ulivyosema hufahamu vitu vingi, maana unaleta vituko na mzaha kusema JK kapelekwa kwenye uchaguzi wa Kenya na Kenyatta.

Hii peke yake inatosha kuonesha huelewi hata ulichokiandika.

Rafiki wa ccm ni KANU na Wakenya walishaizika zamani tu, huzijui siasa za Kenya full stop.
 
CCM inapora Kura wakati Wakenya wanashinda kihalali huwezi kifananisha.
 
Bora ulivyosema hufahamu vitu vingi, maana unaleta vituko na mzaha kusema JK kapelekwa kwenye uchaguzi wa Kenya na Kenyatta.

Hii peke yake inatosha kuonesha huelewi hata ulichokiandika.

Rafiki wa ccm ni KANU na Wakenya walishaizika zamani tu, huzijui siasa za Kenya full stop.
Naona KANU wameizikilia mbali

Ova
 
Back
Top Bottom