Hatima ya OCD Zuberi Mwombeki wa Arusha

Hatima ya OCD Zuberi Mwombeki wa Arusha

Idimulwa

Platinum Member
Joined
May 27, 2011
Posts
5,105
Reaction score
2,689
Amekuwa kwenye misuguano ya mara kwa mara na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo tangu 2010, kikidai kuwa amekuwa akitumia wadhifa wake kukikandamiza katika harakati zake za kisiasa jijini Arusha huku OCD mwombeki akikanusha na kudai kuwa yeye anatekeleza wajibu wake kwa mjibu wa sheria za jeshi nlapolisi na nchi kwa ujumla wake.

Mgogoro wa mwisho ulikuwa ni ule wa kuwaita wafuasi wa CDM'PANYA' pale mahakama kuu Arusha kwenye kesi ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo G.Lema,hili ililalamikiwa sana na uongozi wa cdm pamoja na wafuasi wao na kuitaka serikali imwajibishe au ahamishwe Arusha,CDM walitishia hata kuitisha maandamano ya amani iwapo maombi yao hayatatekelezwa.Nakumbuka Jeshi La Polisi lilituma maofisa wake toka makao makuu akiwamo Changonja kwenda Arusha kuchunguza tuhuma mbalimbali dhidi ya OCD huyo na kuahidi kuchukua hatua.

Naomba mwenye taarifa ya nini ilikuwa hatima ya OCD Mwombeki baada ya uchunguzi kukamilika atumwagie hapa jamvini, maana ni muda kitambo umepita hasikiki kabisa huyu kamanda licha ya cdm kuendelea na harakati zao za kisiasa jijini Arusha,ikizingatiwa kuwa ndiye aliyechangia G.Lema aamue kukaa mahabusu kwa madai ya kuchoshwa na unyanyaswaji wa Jeshi La Polisi wilayani Arusha chini ya uongozi wake.
 
Unajua kuwa chagonja naye ni kada? Hivi unategemea jipya toka kwa hao jamaa?
 
Wakuu Crashwise,LiverpoolFC na wengineo mlioko ARUSHA tunaomba taarifa,kama huyo kamanda bado anaonekana A-Town au la!
 
Mkuu siyo Mwombeki, anaitwa Zuberi Mwombeji. Kwa kifupi huyu OCD alikuwa anatekeleza majukumu yake kwa maelekezo. Mfano mauaji ya Mwangosi. Mimi sidhani kama mhusika wa mauaji ni yule askari aliyekamatwa.

Kwa kifupi Mwombeji amepanda cheo sasahivi yupo mkoani, na anafanyia kazi yake hapa Arusha!
 
Mwombeji sio Ocd tena,kapandishwa cheo siku nyingi sana.
 
Anaendelea vizuri na majukumu yake ya kujenga taifa kupitia jeshi letu tukufu la polisi,na hivi sasa ameongezewa madaraka zaid ya kushughulikia watu wanaondamana hovyo barabaran bila kaz!!!!!!wakiongoza na padri wao aliyekimbia madhabau kwa dhambi zake!!!!
 
Vyeo kwa hisani ya Dhaifu kwa watu dhIfu...unapata udhaifu squired.
 
Amekuwa kwenye misuguano ya mara kwa mara na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo tangu 2010, kikidai kuwa amekuwa akitumia wadhifa wake kukikandamiza katika harakati zake za kisiasa jijini Arusha huku OCD mwombeki akikanusha na kudai kuwa yeye anatekeleza wajibu wake kwa mjibu wa sheria za jeshi nlapolisi na nchi kwa ujumla wake.

Mgogoro wa mwisho ulikuwa ni ule wa kuwaita wafuasi wa CDM'PANYA' pale mahakama kuu Arusha kwenye kesi ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo G.Lema,hili ililalamikiwa sana na uongozi wa cdm pamoja na wafuasi wao na kuitaka serikali imwajibishe au ahamishwe Arusha,CDM walitishia hata kuitisha maandamano ya amani iwapo maombi yao hayatatekelezwa.Nakumbuka Jeshi La Polisi lilituma maofisa wake toka makao makuu akiwamo Changonja kwenda Arusha kuchunguza tuhuma mbalimbali dhidi ya OCD huyo na kuahidi kuchukua hatua.

Naomba mwenye taarifa ya nini ilikuwa hatima ya OCD Mwombeki baada ya uchunguzi kukamilika atumwagie hapa jamvini, maana ni muda kitambo umepita hasikiki kabisa huyu kamanda licha ya cdm kuendelea na harakati zao za kisiasa jijini Arusha,ikizingatiwa kuwa ndiye aliyechangia G.Lema aamue kukaa mahabusu kwa madai ya kuchoshwa na unyanyaswaji wa Jeshi La Polisi wilayani Arusha chini ya uongozi wake.

Idimulwa huna cha kufikiria mpaka Unamkumbuka mwombeji! Kweli humu hakuna great thinkers. Kwa taarifa yako watu wanaomjua huyu jamaa anapiga kazi kinoma, yaani ni jembe. Askari wote wangekuwa hivi jeshi lingekuwa la kimataifa.
 
mkuu do you mean kuminya demokrasia na kupelekea mauaji kama ya mwangosi ni kigezo cha jeshi lapolisi kuwa la kimataifa?
 
Mkuu siyo Mwombeki, anaitwa Zuberi Mwombeji. Kwa kifupi huyu OCD alikuwa anatekeleza majukumu yake kwa maelekezo. Mfano mauaji ya Mwangosi. Mimi sidhani kama mhusika wa mauaji ni yule askari aliyekamatwa.

Kwa kifupi Mwombeji amepanda cheo sasahivi yupo mkoani, na anafanyia kazi yake hapa Arusha!

Kweli tz ni zaidi ya tuijuavyo
 
mwombeji juzi alipokea msafara wa maalim seif na lipumba akiongozana na viongozi waandamizi wa majeshi ya ulinzi na usalama katika uzinduzi wa kuiua chadema arusha.
 
Hivi sasa amepandishwa cheo na kuwa staff one. Yaani msemaji mkuu wa jeshi la polisi mkoani Arusha. Ana uhusiano wa karibu sana na Chagonja. Usitegemee maajabu hapo.
 
NEED WE SAY MORE? ila kwa kuongeza tu ni kuwa jamaa walimkata makali ya kuongea neno "CHADEMA" kwenye vyombo vya habari! Next time usitake kujua habari za wauaji walioko uraiani. They can attack you and KILL you anytime just like others. BEWARE!
 
Thubutu kwangu hawezi mkuu, mie msukuma wa shy bwana 'NASHIMIGIJE NKOI'
 
Wakuu Crashwise,LiverpoolFC na wengineo mlioko ARUSHA tunaomba taarifa,kama huyo kamanda bado anaonekana A-Town au la!

Huyu Zuberi baada ya pindua pindua ndani ya polisisisiem alikaba nafasi ya Staff Officer na hakika huyu ndg laana ya Watanzania aliowaweka pabaya kimaisha itamfuata popote pale alipo!
 
Huyu jamaa ni KADA wa magamba na ni mtiifu sana kwao kwani wakati wa uchaguzi mkuu alishiriki hila nyingi sana za kumkwamisha Lema hata kumdhuru lakini Mungu alisaidia ikashindikana akaamia kutumia njia butu zikawazinamsaidia Lema badala ya Magamba HATIMAYE CHEO ALICHOPEWA KINAMSTAILI Maana amesaidia kuimaliza ccm Hapa Arusha.
 
Back
Top Bottom