Hatima ya OCD Zuberi Mwombeki wa Arusha

Amekuwa kwenye misuguano ya mara kwa mara na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo tangu 2010, kikidai kuwa amekuwa akitumia wadhifa wake kukikandamiza katika harakati zake za kisiasa jijini Arusha huku OCD mwombeki akikanusha na kudai kuwa yeye anatekeleza wajibu wake kwa mjibu wa sheria za jeshi nlapolisi na nchi kwa ujumla wake.

Mgogoro wa mwisho ulikuwa ni ule wa kuwaita wafuasi wa CDM'PANYA' pale mahakama kuu Arusha kwenye kesi ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo G.Lema,hili ililalamikiwa sana na uongozi wa cdm pamoja na wafuasi wao na kuitaka serikali imwajibishe au ahamishwe Arusha,CDM walitishia hata kuitisha maandamano ya amani iwapo maombi yao hayatatekelezwa.Nakumbuka Jeshi La Polisi lilituma maofisa wake toka makao makuu akiwamo Changonja kwenda Arusha kuchunguza tuhuma mbalimbali dhidi ya OCD huyo na kuahidi kuchukua hatua.

Naomba mwenye taarifa ya nini ilikuwa hatima ya OCD Mwombeki baada ya uchunguzi kukamilika atumwagie hapa jamvini, maana ni muda kitambo umepita hasikiki kabisa huyu kamanda licha ya cdm kuendelea na harakati zao za kisiasa jijini Arusha,ikizingatiwa kuwa ndiye aliyechangia G.Lema aamue kukaa mahabusu kwa madai ya kuchoshwa na unyanyaswaji wa Jeshi La Polisi wilayani Arusha chini ya uongozi wake.

Huyu kiboko cha Lema akishirikiana na Mkuu wake Akili Mpwapwa.

nasikia Akili Mpwapwa amepandishwa cheo kuwa RPC manyara. Na huyu pasi na shaka atakuwa RCO.
 
Hivi sasa amepandishwa cheo na kuwa staff one. Yaani msemaji mkuu wa jeshi la polisi mkoani Arusha. Ana uhusiano wa karibu sana na Chagonja. Usitegemee maajabu hapo.
hajapanda cheo ila amepandishwa madaraka amekuwa afisa mnadhimu wa mkoa wa arusha yaan staff officer,si kwamba ndiye msemaji wa polisi kimkoa,msemaji ni KAMANDA WA POLISI MKOA
 
Huyu jamaa ni KADA wa magamba na ni mtiifu sana kwao kwani wakati wa uchaguzi mkuu alishiriki hila nyingi sana za kumkwamisha Lema hata kumdhuru lakini Mungu alisaidia ikashindikana akaamia kutumia njia butu zikawazinamsaidia Lema badala ya Magamba
HATIMAYE CHEO ALICHOPEWA KINAMSTAILI
Maana amesaidia kuimaliza ccm Hapa Arusha.


Hapo kwenye red Kamanda!

Kha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha haaaa!!
Ameikandimiza kabisaaaa!!
 
Back
Top Bottom