Hatima ya jimbo la Sumbawanga mjini mashakani

Ptz

JF-Expert Member
Aug 23, 2011
541
384
Wakuu shalom! Jana tar 30 Novemba 2012 katika mahakama kuu kanda ya Sumbawanga, ilitolewa ruling kuhusu hoja ya bw Aeshi aliyevuliwa ubunge kwa kukutwa na kasoro katika mchakato mzima wa uchaguzi mkuu mwaka 2010 uliompatia ubunge, kasoro hizo ilikuwa ni kwa bw Aeshi kujihusha na rushwa na uchochezi wa uvunjifu wa amani katika mikutano kadhaa ya mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema mzee Yamsebo. Ikumbukwe kuwa mara baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2010 mgombea wa Chadema mzee Yamsebo alifungua kesi kulalamikia uvunjifu wa sheria ya uchaguzi uliofanywa wakati wa uchaguzi mkuu uliomuweka bw Aeshi kuwa mbunge, hukumu ya kesi hiyo ilitolewa Mwezi April mwaka huu kwa kutengua ubunge wa bw Aeshi, kilichofuata ni kwa bw Aeshi kukata rufaa mahakama kuu, walipangiwa majaji watatu ruling iliyotolewa ni kuwa rufaa ilikuwa batili na hivyo kutupwa chini kwa kukosa sifa za kusikilizwa.

Lakini baadaye Bw Aeshi alitoa kitu inatwa Certificate of Agency kwa uelewa wangu baada kufuatilia kwa ukaribu nikaambiwa kinachokusudiwa ni kuwa hoja hiyo inataka kesi ianze upya kwa kutupiliwa mbali hukumu ya kuvuliwa ubunge.

Sasa jana 30/11/2012 ruling ilitolewa na kuwa bw Aeshi kapewa siku 14 kukabidhi vielelezo vyake ilikusudi hoja yake ianze kufanyiwa kazi na mahakama. Na zaidi nachojua ni kuwa huyu bw Aeshi ni corrupted sana, huwa yuko radhi hata kuua ili anachotaka kitimie. Naomba sasa kuuliza ni nini hatima ya jimbo la Sumbawanga mjini, je, hii hoja kisheria inamaanisha nini, ni mahakama ipi itasikiliza hoja hii, je, mahakama kuu au ya rufaa? kwa mwenye kuelwa please.
 
Back
Top Bottom