Hati za Jeetu Patel zatiliwa shaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hati za Jeetu Patel zatiliwa shaka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Dec 24, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,487
  Likes Received: 81,782
  Trophy Points: 280
  Hati za Jeetu Patel zatiliwa shaka
  Timothy Boniface
  Daily News; Tuesday,December 23, 2008 @21:15

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, jana ilitoa agizo la kufanyiwa uthamini upya moja ya mali zilizotumika katika moja ya hati ya dhamana ya washitakiwa Jeetu Patel na wenzake kutokana na kubainika kuwa ina makosa.

  Hakimu Mkazi Richard Kabate alisema hati hiyo ambayo ni ya shamba lililoko Bagamoyo mkoani Pwani, iliyotumika hapo awali kwa ajili ya kuwadhamini washitakiwa Jeetu Patel, Devendra Vinodbhai Patel na Amit Nandy ilikuwa na makosa ambayo yanahitaji kufanyiwa uthamini upya.

  Washitakiwa hao wanatuhumiwa katika wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania. Hakimu Kabate aliuagiza upande wa utetezi kufanya uthamini wa hati hiyo ili kurekebisha makosa yaliyopo.

  Katika kesi hiyo, washitakiwa kwa pamoja wanashitakiwa kwa tuhuma za kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo, kuiba na kujipatia Sh bilioni 2.6 kwa kutumia kampuni yao ya Bencon ya Dar es Salaam. Inadaiwa kuwa waliiba fedha hizo baada ya kudanganya kuwa Kampuni ya Matsushita Electric Trading Company iliwapa jukumu la kulipwa fedha hizo kupitia kampuni yao ya Bencon International Ltd.

  Washitakiwa hao pia kwa pamoja wanashitakiwa kula njama, kughushi, kuiba na kujipatia Sh bilioni 7.9 kwa kutumia kampuni hiyo ya Bencon International Ltd. Washitakiwa hao ni miongoni mwa washitakiwa 21 ambao wamefikishwa mahakamani tangu kuanza kwa kesi hiyo ya wizi wa mabilioni ya fedha za Benki Kuu ya Tanzania katika Akaunti ya Madeni ya Nje. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 30, mwaka huu.
   
 2. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2008
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Uandishi wa Tanzania, unaweza kuchana gazeti. Hati ina makosa gani? Hayasemwi. Hata kuripoti tu, ni shida na hili ndio Daily News au Mkuu BAK ndo umetafsiri from original? No wonder RA na EL waliwanunua wote kama kuku wa kitoweo
   
 3. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ha hahaahahaaaaaaaaaaaa!

  Mwalimu Zawadi, ngoja nikuudhi zaidi, angalia hii headline kwenye press leo:


  Ha hahaahahahahaaaaaa!

  Dada Happy muongo ile mbaya unaambiwa. Hata yeye mwenyewe anatucheka!
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Dec 24, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Ulitaka anune kama yule mnuka samaki wako? ebo....maisha mafupi wewe...ununenune ili iweje sasa....
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,487
  Likes Received: 81,782
  Trophy Points: 280
  Sijatafsiri chochote hapo. Kwa maoni yangu huyu mwandishi labda hakuhangaika kutafuta sababu za hizi hati kutiliwa mashaka labda kwa kutaka kutoa article yake haraka au wahusika wenye undani wa habari hii hawakutaka kutoa info zaidi kulikoni hata hati hizo zikawa na walakini. Tusubiri kama habari hii ina ukweli basi tutajua ni sababu zipi hati hizo zimetiliwa mashaka. Subira yavuta heri.
   
 6. Arsenal

  Arsenal Senior Member

  #6
  Dec 24, 2008
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 191
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  uyu Happiness Katabazi si ndo FM Academia wamemwimba kwenye nyimbo ya inayoitwa "Heshima ya mwanamke" so mnatarajia nini kutoka kwake?????wizi mtupuuu...
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,487
  Likes Received: 81,782
  Trophy Points: 280
  Date::12/23/2008
  Jeetu Patel, wenzake wataka tathmini mpya ya mali zao
  Nora Damian
  Mwananchi

  MFANYABIASHARA Jayantkumar Chandubhai Patel (Jeetu Patel) na wenzake ambao wanakabiliwa na kesi ya tuhuma za wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Malimbikizo ya Madeni ya Nje (EPA), wametakiwa kuwasilisha upya mahakamani ripoti ya tathmini za mali walizoweka kama dhamana baada ya kuonekana mapungufu.

  Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi, Richard Kabate wa Kisutu baada ya upande wa utetezi kuwasilisha maombi mahakamani hapo wakiomba ripoti ya tathmini ya mali waliyoweka kama dhamana ifanyiwe tathmini upya baada ya kubadilishwa jina la kampuni.

  Wakili wa washtakiwa hao, Martin Matunda alidai mahakamani hapo kuwa Julai 2 mwaka 1995 washtakiwa walibadilisha jina la Kampuni ya Azania Investment Ltd na kuwa Noble Azania Investment Ltd, lakini hawakuomba kubadilisha hati ya kampuni.

  "Baada ya washtakiwa kufikishwa mahakamani Novemba 5 mwaka huu na moja ya masharti ya dhamana kuwataka walete fedha au hati, tulilazimika kwenda Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kubadilisha hati ya kampuni na ripoti ya tathmini," alisema Matunda.

  Alieleza kuwa ripoti hiyo ilitolewa Novemba 7 mwaka huu ikiwa na jina la Azania na Novemba 14 mwaka huu ilitolewa hati ya kampuni ikionyesha kuwa kampuni hiyo imebadilishwa jina na kuwa Noble Azania Investment Ltd.

  Alieleza kuwa waligundua kuna mapungufu kwani hati ya kampuni ndiyo ilitakiwa itolewe kwanza kabla ya ripoti ya uthamini.

  Hakimu Kabate aliahirisha shauri hilo hadi Desemba 30 mwaka huu upande wa utetezi utakapowasilisha ripoti hiyo.

  Jeetu Patel na wenzake Kentan Chohan na Amit Nandi wanashtakiwa kwamba,mwaka 2005 walikula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka bandia na kuiibiaBoT Sh3,323,974,942.30 kupitia kampuni yao ya Navy Cut Tobacco (T) Ltd kwamadai kuwa imerithishwa deni la kiasi hicho cha pesa kutoka kampuni yaMatsushita Electric Trading Company ya Japan.

  Katika kesi hiyo Jeetu na wenzake walipata dhamana baada ya kuwasilisha hati za mali zisizohamishika zenye thamani ya zaidi ya Sh 3.5 bilioni.
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,229
  Likes Received: 5,619
  Trophy Points: 280
  pumbafuuuuuuuuuuuuuuuuu zao wooooooooote mahakamani na majaji zao
  unatoa dhamana ndio unadai ......oohhhhhhhhhhhhh shit hawana maana kabisa
   
Loading...