Lamkyeku
JF-Expert Member
- Apr 18, 2014
- 494
- 661
Hapa kwenye hii ofisi nina mwaka mmoja tu, nilivyoajiriwa hapa niliwakuta wenzangu wengi wakiwa wanafanya kazi na wanaendelea na masomo, wengi walikuwa wanasoma diploma na degree. Mimi nilikuwa tayari nina degree ingawa hapa sifanyi kazi ya proffesional yangu. Kwakuwa nilikuwa na lengo la kusoma mwaka huu nika apply masters na nikapata na ni evening class. Tatizo linakuja nimeenda kwa boss kuomba ruhusa ya kusoma ili awe ananiruhusu niingie kazini asubuhi kwakuwa hapa kuna shift ya jioni, ili niweze kuingia darasani amekataa. Amedai masters yangu haisaidii chochote kwenye kampuni na pia kwake hata mtu wa cerficate tu anatosha. Ada nimeshalipa na nimeanza kusoma maboss wa humu naombeni kazi au nisaidieni ushauri niache kazi au ni postpone chuo? Ni kampuni binafsi.