Wizara ya Ardhi
Govt Institution
- May 14, 2024
- 299
- 160
Tukielekea ukingoni mwa mafunzo ya mfumo mpya wa Ardhi kidijiti mkoani Kagera, wataalamu wa sekta ya ardhi wameanza kuonesha matokeo ya ujuzi walioupata kwa vitendo, ambapo hadi sasa hati nne za umiliki wa ardhi zimetolewa kupitia mfumo huo na wananchi husika wametaarifiwa kuzifata hati hizo.
Aidha, zaidi ya viwanja 500 vimeingizwa kwenye mfumo, hatua inayoweka msingi wa kuwawezesha wananchi kuendelea na taratibu za kupata hati zao kwa njia ya kidijiti.
Katika eneo la Mipango Miji, wataalamu wamefanikiwa kupandisha jumla ya michoro 27 kwenye mfumo wa e-ardhi hatua inayorahisisha upatikanaji wa taarifa za matumizi ya maeneo na kumwezesha mwananchi kutambua matumizi yaliyopangwa kwa eneo husika kabla ya kuendelea na taratibu za umiliki na uendelezaji wa ardhi.
Mafunzo haya ya wiki Moja yameanza mapema Tarehe 14 Septemba,2026 katika ukumbi wa ELCT Bukoba na yanatarajiwa kuisha mapema wiki ijayo tayari kuendana na kasi ya mfumo mpya wa Ardhi