Hati chafu manispaa ya Kigoma/Ujiji walistahili pia wanastahili

Haludzedzele

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,468
528
Manispaa ya Kigoma/Ujiji ni moja ya Manispaa ambayo utendaji wake wa kazi ni wa kushangaza sana kwani mambo yake yote ni ya kiholelaholela tuu ukianzia vyanzo vya mapato, stahiki za watumishi pia miundombinu ni balaa tupu. Barabara za katikati ya mji baadhi ni mashimo ya hatari ambazo zinaharibu sana magari pia husababisha hadi ajali mfano barabara ya Katonga ni shida tupu tena hadi Meya kwao huko. Ukusanyaji wa ushuru bado changamoto kubwa sana hasa kwa Wafanyabiashara kumekuwa na ongezeko la mara kwa mara la kodi utadhani sio Tanzania hii ni shida sana. Ukiacha hayo yote kwenye stahiki za Watumishi hawa jamaa hapana kwakweli wapo tofauti sana na Halmashauri/Manispaa zingine kabisa yani tatizo bado naendelea kulifanyia kazi kama ni sababu ya wenyeji wengi kuwamo kwenye maofisi ama laa! Nitakuja na majibu ya tafiti yangu. Watu wameomba likizo ya malipo tangia 2015 mpaka sasa wanalipa wa 2016 mwezi wa 6 napo kwa mafungu sasa kama pesa hakuna kuna haja gani ya kuwajazisha watu likizo za malipo ilihali mnafahamu kuna ugumu katika ulipaji mie naomba wizara husika iliangalie hili, Upandishaji wa madaraja kwa watumishi umekoma tangia 2011 mpaka leo hivi kweli morali ya watumishi itatoka wapi kufanya kazi kwa moyo ilihali stahili zao hawapati za kimsingi kabisa mbona halmashauri/manispaa zingine watumishi wao wanapandishwa kunani Kigoma? Mie ningeshauri Mamlaka husika ije ifanyie kazi haya mambo mapema kabla mambo hayajaharibika kabisa kwani tuendako naona kabisa giza totoro! Nawasilisha iwafikie wahusika
 
Back
Top Bottom