Dzerzhinsky
Member
- Jun 11, 2015
- 32
- 40
Nadhani ni mwandishi wa kimarekani Cristoper Dikens kama sijakosea jina, wakati Marekani ikijiandaa kuishambulia Iraq ili kumuondoa Sadam madarakani mandishi huyu aliandika makala "The perils of victory" Kwa Kiswahili unaweza kusema "hatari za ushindi". Kwenye makala hii alitahadharisha mambo ambayo yangetokea baada ya ushindi wa kijeshi wa marekani dhidi ya Sadam. Alitabiri karibu kila kilichotokea baadaye kuanzia the cilivil war hadi kugeuka kwa Iraq kuwa a save heaven kwa magaidi.
Si lengo langu kuijadili makala ile, nimechukua kichwa cha makala ile vile kinawiana sana na yanayoelekea kutokea kwenye siasa za Tanzania kwa sasa. Kuna fununu kwamba kada wa CCM Mh Edward Lowassa anaelekea ku hama chama chake na kujiunga na chama kikuu cha upinzani (CDM) na labda akapitishwa kugombea uraisi kupitia UKAWA.
Uchambuzi wangu finyu unaniambia uwezekano wa Lowassa kushinda uraisi kupitia UKAWA ni mkubwa. Kwa nini! Wengi wanafikiria juu wa watu walioko nyuma yake lakini sidhani kama hilo ndilo lenye umuhimi wa kwanza. Kuna mambo kadhaa yanayompa Lowassa na UKAWA nafasi nzuri ya kuiangusha CCM.
CONNECTIONS ZA LOWASSA NDANI YA SYSTEM NA CHAMA Kushinda uchaguzi ni zaidi ya kuungwa mkono na watu, ni zaidi ya kupigiwa kura za kutosha. Uchaguzi ni kama vita na unapojipenyeza kwenye ngome ya adui yako na kujua anachopanga kufanya hakika una nafasi nzuri zaidi ya kushinda. Lowassa ana watu ndani ya system na CCM. Kuna watakaotoka naye iwapo atatoka (wana CCM) na kuna watakaobaki na kuendelea kumtumikia kichini chini wakiwa CCM, kuihujumu CCM toka ndani. Watu wake ndani ya system watasaidia sana kukabili juhudi wa system kuuhujumu upinzani. CCM na system iliyoko nyuma yake italazimika kupigana vita mbili kwa wakati mmoja, vita na upinzani wa wan je upande mmoja na upande wa pili itakuwa vita dhidi ya upinzani wa ndani. War on two fronts is the last thing strategist would wish for.
RASILIMALI FEDHA Ni wazi kuwa nyuma ya Lowassa kuna massive financial resources kulinganisha na kile ambacho CDM/UKAWA inaweza ku mobilize bila Lowasa. Rasilimali fedha ni muhimu sana kushinda uchaguzi, huu ni mchakato ghali sana ambapo uwezo wa kifedha una nafasi yake katika kuleta matokeo.
ORGANISATION Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni, 4u movement ilikuwa the best organised campaign within CCM, ilikuwa movement iliyoazima mbinu nyingi za kibiashara kufanya siasa, kosa kubwa lilikuwa ni kutokuweka msisitizo wa kutosha kwenye siasa yenyewe, siku nikiwa na nafasi nitalieleza hili kwa kina. Sasa organisation hii ikijumlishwa naya UKAWA itakuwa ni kikosi mahiri kabisa na tutaona mambo mapya kwenye kampeni za kisiasa. Sioni namna gani CCM inaweza kutengeneza timu ya kushindana na hii hapa.
WATU Hili wa watu nimelipa kipaumbele cha mwisho, Yes Lowasa ana watu wa kutosha (watu wa kawaida) japo si wengi kama anavyotaka kutuaminisha, jambo kubwa hapa watu hawa wengi wao si undecided voter bali ni wapiga kura wa CCM, watu wa Lowasa wana double effect iwapo wataipigia kura UKAWA, kwanza watoongeza kura za UKAWA na pili watapunguza kura ambazo kwa kawaida CCM inakuwaga imeshajihakikishia.
JE LOWASA NA CHADEMA/UKAWA WANA AGENDA MOJA?
Lowasa anautaka uraisi kwa gharama yeyote na UKAWA wanataka kuchukua dola. Hapa they both have something in common ila ukienda mbele zaidi utagundua wanaachana. Siamini kama Lowasa anataka madaraki ili kuleta mabadiliko chanya kwa Tanzania na Watanzania, kama ni hivyo basi hilo ni la mwisho katika vipaumbele vyake. Namuona kama mtu anayeendeshwa zaidi na ego yake na maslahi yake binafsi yale ya marafiki zake. Upande wa pili kuna element ndani ya UKAWA/CDM strong enough elements zilizodhamiria kuleta mabadiliko chanya kwa Tanzania/watanzani. Ni wazi kuwa pande hizi mbili kila moja inamjua mwenzia fika, ndoa hii iwapo itafungwa haiongozwi na mapenzi bali maslahi fulani fulani ya pande hizi mbili, mengine yenye manufaa kwa Tanzania na mengine yasiyo na manufaa kwa Tanzania. Of course siasa ni mchezo wa mahesabu makali na average brains zinaweza zisielewe most of the policial moves, siasa haziongozwi na hisia za mapenzi au chuki, zinaongozwa na maslahi ya mudu mrefu.
NINI HATARI YA USHINDI WA UKAWA? CDM/UKAWA wanaamini wataweza kudhibiti Lowassa baada ya kumtumia kuchuka dola, hili si jambo rahisi sana kwa kaliba yake Lowasa ninayemfahamu. Uwezo wake wa kujua bei za watu na staili yake ya kufanya siasa isiyo na jambo la kuonea aibu kufanya iwe baya kiasi gani inatoa picha tofauti. Naona hatari ya Lowasa kuununua uongozi wa juu wa CDM/UKAWA na akaishia yeye kuwaendesha badala ya wao kumuendesha. Hili likitokea tutaona muendelezo wa uozo ule ule tuliouona ndani ya serekali ya CCM na watu watajiuliza ilikuwa ni kwa manufaa gani waliiondoa CCM madarakani? Mbona majizi yale yale yaliyotamalaki chini ya utawala wa CCM bado yanaendelea kubaka rasilimali zetu chini ya utawala wa UKAWA? Huo utakuwa mwisho wa kisiasa wa baadhi ya vyama ndani ya UKAWA, nadhani muathirika namba moja atakuwa CHADEMA.
Hatari hii ikiwa kweli tutasema "not all is lost": kwanza itakuwa ngumu sana kupitisha mambo bungeni kwa msimamo wa chama, for sure no matter what happens UKAWA ikishinda hatutaona chama kimoja kikiwa na udhibiti wa bunge kama ule iliokuwa nao CCM. Hii ni habari njema sana kwa wapenda mabadiliko. Pili: Baada ya kuiondo CCM madarakani, itakuwa kazi nyepesi sana kuving'o vyama vitakavyofuatia, CCM ni chama dola, chama kilichotuletea uhuru, chama chenye mizizi iliyojikita chini sana, hao wengine watakuwa wepesi sana kuwaondoa na tutaendelea kubadilisha vyama hadi tupate watawala sahihi. Hakutakuwa na chama kimoja kinachohodhi madaraka kama ilivyo CCM sasa!
HITIMISHO Kama hitimisho, iwapo Lowassa atahamia UKAWA kuna uwezekano mkubwa wa kuong'oa CCM madarakani japo kuna hatari kubwa ya uozo wa CCM kujirudia chini ya utawala huo mpya. Hata hivyo bado naona "it is a risk worth taking! Kuiondoa CCM madarakani itakuwa hatua ya kwanza, tutakuwa tumeondoa kikwazo kikubwa kabisa cha kwanza hivyo vingine tutaendele navyo hatu kwa hatua.