Hatari ya deni la Taifa lisilolilipika!. Tunakopa kuliko uwezo wa kulipa!.-Ex CAG, Ludovick Utouh

Kuna mizigo serikali hii imejibebesha bila ya ulazima wowote na hivyo kuongeza matumizi makubwa kwa serikali.

Kwa mfano kulikuwa na haja gani ya kuanzisha Mahakama ya Mafisadi??

This is bringing very unnecessary expenditures to the government.

Hii Mahakama imeleta ufanisi gani so far??

Shida kama Taifa we don't have priorities. Ni hobela hobela tu mtu anaamua ananunua midege kama vile mahitaji ya watanzania ni mindege kwa sasa. Mindege haikuwa hata kwenye bajeti as a result masuala mengine ya msingi yanakwama kwasababu ya matumizi haya ya ovyo ambayo hayakuwa kwenye bajeti.

That's why tunakopa sana na tunakoelekea status yetu itakuwa hatukopesheki.
bila kusahau ujenzi wa kiwanja cha ndege cha chato kwa manufaa ya nani??kwa bujeti ipi kweli kuna mizigo mingine tunajitakia wenyewe
 
Labda tuainishe aina ya wadai,kuna wadai wa ndani ambao benki hazitakubali kusubiri kwa wale waliokopa,na wengine biashara zao zitakufa kwa kuwa mitano yao imeshikiliwa serikalini,hawajalipwa,kuna watumishi wa umma,wakisubiri watawekewa riba?

Hao wa nje sijui
Dani la ndani haliisumbui serikali hata kidogo. Kwani hata miaka mingapi kama riba yake ikiwa inalipwa, ukuwaji wake hauwezi kuwa wa kutisha.
Dani la nje ndio wa kulipwa kwanza kwani kuendelea kuwa na hela yao kunalikuza deni. Hata usipokopa deni jipya, shiling ikishuka thamani tu,deni huongezeka.
Ndio maana ya kujadiliana. Hoja za serikali zikieleweka kwa madeni ya ndani sawa. Haya ni yale madeni ya kibiashara kwenye mabenki. Si madeni ya wazabuni,na wafanyakazi.
 
Ukusanyaji Kodi hapa Tanzania ndio umeshafika mwisho wake, zaidi ya hapa ni kuwaonea Wananchi na kuwakamua kwenye vitu visivyo na maana

Bila uwekezaji mkubwa hakuna kitakachofanyika hapa Tanzania, kwa sasa sector ya Biashara inaelekea kufa, sector ya Mahotel imeshakufa
 
Ukusanyaji Kodi hapa Tanzania ndio umeshafika mwisho wake, zaidi ya hapa ni kuwaonea Wananchi na kuwakamua kwenye vitu visivyo na maana

Bila uwekezaji mkubwa hakuna kitakachofanyika hapa Tanzania, kwa sasa sector ya Biashara inaelekea kufa, sector ya Mahotel imeshakufa
Wamehamia kwenye simu,nataraji bando zitakuwa muhanga wa bajeti hii,
 
Tatizo jamaa bado hajapata mtu wa kumshauri na hataki kuoneonekana mjinga baada ya kufata ushaur wa ndani anamfata yule jamaa anaemiliki mkoa mmoja wa tanzania.

But also bashite ndio mshaur mwengine hebu niambieni hzi ndege alizitamka katika sera yake ya ccm???

Viwanda hakuna kazi kupiga domo tz ya viwanda but nothing we gotta.

Ujinga juu ya ujinga kazi kuwaandama wasanii na wanasiasa.

Dah natamani hata kulia pumbav zao

Sitorudia kunywa pombe [HASHTAG]#2020[/HASHTAG]
 
Ni kweli taifa haluwezi kujinasua kwenye mafedi km halina uwezo wa kukusanya kodi.

Ni dhahiri pia kuwa TRA umeshindwa kusimamia vyema ukusanyaji wa kodi. Hapa Tanzania watu pekee wanaolipa kodi kihalali ni wafanya kazi. Wengine wooote halalipi kodi inavyostahili.

Kwahiyo namna pekee ya kujinasua toka kwenye madeni ni kuboresha mfumo wa ukusanyaji kodi.

Ukienda sasa hivi kariakoo. Ukinunua kitu muuzaji anakuuliza nikupe risiti bei ibaki 100,000 au nsikupe ili bei iwe 70,000? Kwa akili ya kawaida option ,B ndo rahisi kwa mlaji.

Pia ukinnua kitu kwenye efd mashine item haiandikwi km ipasavyo na mwisho badala ya kuingiza 300,000 inaandika 30,000. Tutafika kweli kwa utaratibu huu??

Niishauri serikali na TRA. Itumie mfumo wa Barcoding. Yaan bidhaa iwe unakuwa scanned tu na details zake zote incl. Bei iwe inaingia automatically kwenye system. Mfumo huu utumike kwenye big stores/shops kwa kuanzia. Inaweza boresha mapato yetu hata Mara 10 zaidi ya sasa.

Kwa utaratibu huu tunaoendelea nao wa mambo kufanyika manually. Hatuwez kukusanya kodi accordingly na deni litakua hadi kuwakuta vining'ina wetu.
mchango wako mzuri sana mdau ila wengi huwa tunasahau hapa na kuparuka,hili swali gumu kwanini huwa hatujiulizi kwanini wafanyabiashara wanaskip kulipa kodi?kwanini watafute mbinu za kukwepa kulipa kodi halisi,je hizi complain za wafanyabiashara kuwa kodi nikubwa kuliko uhalisia wa wanachokiuza na kuzaliasha tunazichukulia serious sisi wananchi na taasisi husika za ukusanyaji mapato,hivi mazingira ya biashara Tanzania ni kweli yanaridhisha kuwekeza au rate ya harasa iko juu zaidi ya faida?TRA lazima waje na mkakati mpya wa ukusanyaji mapato na elimu pana ya ulipaji kodi kwa umma na pia wajadili changamoto mbalimbali katika sekta ya biashara nchini
 
Kuhusu ndege ungewaachia sekta binafsi tuu ww kusanya kodi mpk utakapo fikia baadhi ya hatua ndo uanze kutuchukulia pangaboi lakin now hatuna madawa,elimu inakufa huajiri dah kwaherini naumia sana.
 
Kodi ni nyingi mpk inaboa mzigo mmoja unaweza ukagharimu 10000 tena mdogo hebu niambie why nisitumie njia ya magendo
 
IMG-20170424-WA0004.jpg
 
Nadhani madarasani tunasomeshwa hard and complex terms za uchumi plus its principles ambazo kimsingi ni non applicable.

Uchumi ni uzalishaji/production na matumizi/expenditures mengine yoooote ni ulipumba tu

Trust me guys!
simple economics
1. Rate ya ukuaji wa deni hautakiwi kuzidi ukuaji uchumi

2. Widen tax base vinginevyo ukusanyaji usiozingatia optimal taxing hunyong'onyesha vyanzo vya mapato na future ni kupungua/kukosa cha kukusanya
 
Hivi hawa wawekezaji lukuki tulio nao kwenye gesi, madini na kwingineko kwa nini wasilipe hili deni?!
 
Hakuna nchi yoyote duniani iliyoendelea kirahisirahisi lazima kuumia. Magufuli yuko sahihi siku mkianza kuona matunda ya anachokifanya ndo mtaonekana wajinga

Mkuu wengine tunachoshangaa ni kwamba mkuu alisema tunakopaje wakati tuna kila kitu, pia alituahidi tutakuwa donor country, alienda mbali na kumbeza mtangulizi wake lakini tunachoona kinafanyika tunarudi kulekule,.

Kwa taarifa yako hakuna nchi changa duniani iliyowahi kuendelea kwa kukopa kopa zaidi ya kufirisika na kuwa mtumwa wa hao wanaokukopesha.
 
Hili deni la taifa litatutesa sana!

Ili ulipe deni lazima uzalishe,uzalishaji huleta kodi kwa TRA,kodi hulipa deni,kuna taarifa kwamba sekta ya hoteli inakula hasara kwa asilimia 60,japo mimi si mchumi,maana yake karibu nusu au robo tatu ya hoteli nchini hazitalipa kodi,TRA wataambulia patupu

Mzunguko wa hela hakuna,Ile hoteli ya bwana Slim ya Bagamoyo imeuzwa mara tano na Mara hizo tano amekosekana mtu wa kuinunua kwa bilioni tano,imagine Dar es salaam bilioni tano ni ishu! Hata kama mtu anazo,hazitoi kwa kuwa zinaweza kufia huko

Apartment za msasani exim bank walitangaza mnada,taarifa zinasema apartment zimekosa mnunuzi.

Kama ndivyo,hizi benki zilizokopesha zinaelekea wapi? Kama zikiwa na wadaiwa wa aina hiyo 100 kwa kila benki,maana yake benki zinaelekea kufa kwa kuwa haziwezi ku-dispose/kuuzaassets zilizowekwa dhamana,benki zikifa maana yake haziwezi kukopesha,biashara pia zitaanguka,hasa zinazotegemea mikopo ya benki,na ajira zitapungua,hii yote inajitafsiri katika kodi,yote hayo yakiyumba na kodi zinapungua,na uwezo wa kulipa deni unapungua,kama nchi tunakuwa hatukopesheki.

Kuna kasi kubwa ya kufunga biashara maeneo mbalimbali,hatupewi majibu ya kitaalamu na wataalamu,wanaotoa majibu ni wanasiasa wanasema hao ni wapiga dili,walikuwa wanampigia dili nani? Ina maana watanzania wote milioni zaidi ya arobaini walikuwa wanashinda bandarini,wizarani,halmashauri wakiiba? Tukichukua takwimu,ni watanzania wangapi wanafanya transaction na serikali na za thamani gani? Na je thamani hiyo inalingana na hali mbaya iliyopo? CAG ndio mkaguzi wa hesabu,hajaonyesha upiga dili wa kiasi hicho kikubwa na kama kaonyesha basi ni isolated cases,

Na kwa nini itokee ndani ya mwaka mmoja?

Export kubwa ya nchi hii hasa ni Kilimo,lakini katika vipaumbele vya bajeti,Kilimo hakimo,Kilimo kinagusa asilimia 80 ya watanzania,ukisema Kilimo si kipaumbele maana yake asilimia 80 ya watanzania si kipaumbele chako,na unatengeneza masikini 80 katika kila watu 100,maana yake,kodi watalipa watu 20,themanini wanabaki tegemezi,na pia uwezo wa ku-export unapungua.

Sekta ya umma iko dormant,zamani ilikuwa unasikia halmashauri walau zinauza Viwanja huku na kule,tunaenda mwaka wa pili hakuna hata moja yenye mradi mpya wa Viwanja,wanaouza sasa ni wale waliokuwa na miradi ya enzi za JK,maana yake hakuna mapato,maafisa ndani ya serikali wanaogopa kubuni miradi ya kuongoza pesa,wanaogopa kuitwa wapiga dili na mwishowe kudhalilishwa majukwaani,nadhani wanachofanya maofisini ni kuingia,kusaini,fanya SHUGHULI ZA KAWAIDA,jiendee nyumbani ukalale

Bila kubadilika na kuwaona wafanyabiashara wa ndani wapiga dili,tumekwisha

Kuna jambo moja lilipita kimya kimya,inaonekana wazi sekta binafsi hawashirikishwi katika kuiangalia bajeti(kwa muono wa wapiga dili).JK alikuwa anawaita katika hatua za awali watoe maoni yao,lakini baada ya bunge la bajeti kuanzia ndio nikaona Private Sector Foundation ndio wanaitwa Dodoma,yaani baada ya bajeti kuanza kujadiliwa,hii maana yake ni mwendelezo wa bajeti zisizo rafiki,na muono kwamba "kodi huwa zipo tu" bila kujua kodi hutengenezwa kwa kuboresha mazingira ya biashara.

Mwishowe tunaanza kusema tuombewe,kuongoza nchi kuna sheria na kanuni zake,maombi hayajawahi kuwa sehemu ya kanuni,kuongoza uchumi kuna sheria na kanuni zake na waliozisomea wapo,maombi hayajawahi kuwa sehemu ya kanuni za uchumi,

Sisi watanzania tulishamkabidhi kitabu chetu cha sala, kinaitwa KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO,humo ndio kuna mkusanyiko wa maombi yetu yote kama taifa,pamoja na waraka (sheria)zilizoundwa chini yake,na makasisi(wataalam mbalimbali,wakiwemo wa uchumi),hakuna kingine cha kumpa kwa kuwa hatuna access tena katika decision making mpaka 2020
Mkuu umemaliza... Kama hawatakuelewa basi achana nao..
 
Back
Top Bottom