Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,685
- 119,325
Wanabodi
Nimeangalia ITV kumepambazuka mubashara ya asubuhi hii ambapo mgeni rasmi ni CAG Mstaafu Ludovick Utouh aliyekuwa akichambua Ripoti ya CAG kwa mwaka huu.
Utouh ametahadharisha Tanzania kukabiliwa na hatari kukua kwa kasi kwa Deni la Taifa kusiko kwenda sambamba na ukusanyaji wa kodi hivyo taifa kukabiliwa na hatari ya kuwa na deni la taifa lisilo lisilo lipika!.
Hii maana yake Tanzania tunakopa zaidi kuliko uwezo wetu wa kulipa kwa kukusanya kodi kidogo, hivyo makusanyo yote ya kodi yote inayokusanywa haiwezi kuli service deni la taifa.
Hii maana yake tunakopa kuliko uwezo wetu wa kulipa na tunatumia kuliko uwezo wetu wa kukusanya mapato. Tanzania bado inakusanya kodi kidogo kuliko shughuli za uzalishaji ambazo zingepaswa kutozwa kodi. Ni wachache wanaolipa kodi ukilinganisha na idadi yetu ya watu.
Hali hii ya kukopa kuliko uwezo wa kulipa ikiendelea hivi kuna hatari ya Tanzania kuwa haikopesheki.
Utouh ameshauri ili taifa lisielemewe na mzigo wa madeni,
Serikali inegotiate na wadeni wetu, ili watuongezee muda wa kulipa madeni yetu bila kuongeza riba na wakati huo huo kuongeza ukusanyaji wa kodi.
Amesema Ripoti ya CAG bado inakabiliwa na changamoto ya utekelezaji mapendekezo ya CAG na kutolea mfano kati ya mapendekezo zaidi ya 200 ya CAG kwenye ripoti ya mwaka jana, ni mapendekezo 38 tuu ndio yametekelezwa.
Amempongeza CAG aliyepo Prof. Mussa Assad kwa ripoti nzuri na kumpongeza rais Magufuli kwa ahadi ya kuitisha mikutano ya kila sekta kuijadili ripoti hiyo.
Utouh amesema katika kulisaidia taifa kwa uzoefu wake, ameanzisha taasisi ya uwajibikaji ili kuisaidia serikali yetu kuwawezesha watendaji wake kuwajibika.
Jumatatu Njema.
Paskali