Hatari ya CCM kukosa majimbo yote Dar

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
15,300
23,022
Mpaka sasa sioni dalili ya CCM kuchukua jimbo hata moja katika jiji la Dar labda la Kigamboni kutokana na mgogoro wa CHADEMA na CUF lakini majimbo yote UKAWA wana nondo za kutosha.

Mfano, Kibamba yule mama hata UKAWA wangesimamisha jiwe, jiwe lingeshinga.

Ubungo mpaka sasa sijui atashindia wapi kwani mkutano wake tuu haina watu, kubenea hana mpinzani

Segerea ndo kabisaa, Mtatiro anashinda kweupeee

Temeke huyu Mtemvu watu walisha mchoka tangu zamani

Ukonga, Silaa sidhani kama ataweza shindana na Waitara kutokana na nguvu ya upinzani katika jimbo hilo

Ilala huyu Hassanal ndio anakubalika na wamachinga na vijana wengi, zungu washamchoka.

Mbagala ndio hivyo CCM hakuna chao pale

Kinondoni ambapo ni makao makuu ya CHADEMA, CCM pale hawana jipya tena.

Kawe, Halima Mdee ndio hivyo tena anasubiri kuapishwaa
 
Bahati mbaya kinondoni hakuna mgombea waukawa. Mgombea wa cuf alienguliwa
 
Ukawa wahakikishe wanaondoka Na majimbo zaidi ya 150. Iwe mijini au vijijini!
 
Wamachinga wamemchoka zungu? Ilala Wamachinga wanakuja na kuondoka sio wakazi wala hawajajiandikisha Ilala msidanganywe na kelele zao
 
Sio dar tu huku mikoani ccm hawaitaki kabisa nilienda songea sidhani kama mgombea wa ccm atapata nusu ya kura dhiidi cdm na hata wakishindwa nani asiyejua wabunge wa ccm ni mizigo bora kutokuwa na mbunge kuliko ndiyoooooooo
 
Kidogo nilikuwa na wasiwasi na jimbo la ilala maana namuona Zungu kama ana nguvu vile, ila kikweli kwa hayo mengine njia ni nyeupe kabisa kwa UKAWA.
 
shost

Kwa Ilala mmmmh! Wamachinga si wapiga kura Ilala, wanakuja kufanya biashara tu jioni wanarudi Mbagala...
 
Last edited by a moderator:
Kidogo nilikuwa na wasiwasi na jimbo la ilala maana namuona Zungu kama ana nguvu vile, ila kikweli kwa hayo mengine njia ni nyeupe kabisa kwa UKAWA.

Majimbo ya Ilala,Kigamboni,Ukonga na Temeke hayo yanarudi CCM,Chadema wana uhakika majimbo ya Kibamba na Ubungo while Kawe,Segerea hayo ni 50/50.Sina uhakika na Mbagala,Kinondoni
 
Majimbo ya Ilala,Kigamboni,Ukonga na Temeke hayo yanarudi CCM,Chadema wana uhakika majimbo ya Kibamba na Ubungo while Kawe,Segerea hayo ni 50/50.Sina uhakika na Mbagala,Kinondoni

Kwa mimi ninavyoona Ilala, kigamboni, kinondoni, Ukonga na Temeke itayachukua CCM..., Ubungo, Segerea, kibamba, mbagala na kawe yanakwenda Ukawa
 
Kwa mimi ninavyoona Ilala, kigamboni, kinondoni, Ukonga na Temeke itayachukua CCM..., Ubungo, Segerea, kibamba, mbagala na kawe yanakwenda Ukawa

Jimbo la Kawe yeyote anaweza akashinda hali sio nzuri kwa Mdee kwani hakufanya la maana jimboni na CCM wana mgombea strong (Kippi Warioba)
 
wakazi wa ilala sio machinga, ni watumishi wa serikali na wafanyabiashara wa kiasia. wote ni waasia, watachagua wa kumpa
 
Back
Top Bottom