Hatari: Nimenusurika kifo

Hatari: Nimenusurika kifo

Habari wakuu...
Jana mwanajamii mwenzenu ilibaki kidogo tu ni rest in peace kutoka kwa wananchi wenye hasira Kali. Ilikuwa kwenye daladala...kama mnavyojua wana JF usafiri wa umma tabu zake hasa nyakati za asubuhi.

Basi baada ya daladala kuingia kituoni watu tukaanza kugombania..hatimaye nikafanikiwa kuingia..lakini sikufanikiwa kupata siti....nilisimama na mdada Fulani hivi pembeni yangu huku akiwa amening'iniza mkoba wake upande Wangu..wakati tunaendelea na safari na hizi barabara zetu zilizo kwenye marekebisho. Ule mkoba ukawa unaning'inia kuniegemea mimi.

Sasa kuna mtu alikuwa anashuka kituo kinachofuata ikanilazimu kusogea mbele kidogo ili kumpisha mshukaji..kwa bahati mbaya wakati nampisha Yule mshukaji mabega yetu yakawa kama yanauvuta ule mkoba wa yule dada.

Kasheshe likaanzia hapo baada kunihisi mimi ndiye niliyekuwa nauvuta ule mkoba kwa makusudio ya kuiba..akaanza kunipigia makelele ya wizi. Jambo ambalo liliwapa hamaki abiria wengine wakaanza kunishambulia hadi konda alipoanza kunitetea kwa kuwa alilishuhudia. Na ukijumlisha na personality ...abiria wakaanza kunielewa kwamba sikuwa mwizi.

Ikanibidi nishukie kituo kinachofuata ili kuondoa nuksi...duh..kweli si kila anayekufa kwa wizi basi kaiba kweli..wengine wanasingiziwa tu...tuweni tunaposhambulia wezi....

Kikulacho ki-nguoni mwako.
 
Mkuu sasa ndio umewapa wabishi ndani ya bus nafasi ya kusema "NDIO MIJIZI YENYEWE, TUMEMSTUKIA KASHUKA"....Pole sana
 
Da pole sana kaka mi ilinitokea Sinza siku moja kwenye lodge moja hivi. Nilikuwa na Shem wenu ndani ya chumba tukagombana coz ma gal alikuwa anawivu sana.

Baada ya kugombana nikabidi mi nisepe zangu nikaona hamna dalili ya kupata mzigo hapa but kipindi naondoka Shem wenu alikuwa yupo anaoga.. Mi nipo njiani nakaribia pale meeda nikaona kundi kubwa la watu km 10 hivi wananifata na kuita mwizi mwizi mi nikashangaa vp. Ghafla namuona mlinzi wa lodge anasema kuna demu mmoja Anasema umemwibia pochi yenye laki 2..watu baada ya kusikia hivyo wakaanza kunipiga mdogo mdogo kwamba lazima tukuchome wewe, watu wakawa wanaongezeka na kipondo kinaongezeka yani sipati hata muda wa kujitetea.

Mara gafla akatokea jamaa mmoja tulipiga naye mzumbe chuo amani Mimi mtu huyu namjua twendeni turudi lodge Kwa huyo binti aliyeibiwa, basi tukarudi watu kama 20 ivi hapo nishapigwa sana jamani.. Tukafika guest house pale, Dada wa reception akasema yule msichana kaondoka sasa hivi kafatwa na mwanaume akiwa na gari..kuhusu pochi kumbe kaiona ilikuwa chini ya mto. Sitoisahau that day

Hapo ukaumia mara mbili.....1- kipigo cha wananchi wanaojiita wenye hasira kali......2- kunyimwa mzigo halafu unasikia kuwa alifuatwa na kidume mwingine tena ana gari
 
Ila outlook yako pia inakufanya uwe safe. Mfano ninavojipigiliaga napotoka nyumbani,siriazness napikua public transports, mapozi nini asee ukiniitia mwizi nahisi watu wote watakuhamaki.
 
Ni wiki sasa imepita kuna kijana wa miaka 17 kauawa huku kimara mwisho njia ya bonyokwa millenium. Huyu kijana alijiingiza kwenye ufundi wa bodaboda baada ya wazazi wake kushindwa kumlipia ada.

Siku ya idd tar 29/7/2014 marehemu aitwae lawrance alishinda nyumbani kwao tu maeneo ya mavurunza kimara, ilipofika saa kumi kuna kijana aitwae john alifika nyumbani kwa akina lawrance kwa lengo la kumuomba akamtebgenezee bodaboda. ilipofika saa moja jioni wakaanza safari kuelekea mahali bodaboda ilipo, kufika kule kijana lawrance akafanikiwa kutengeneza ile pikipiki sasa ile aijaribu akiwa amempakia john na kijana mwingine ambaye hakufahamika hatua chache mbele wakasikia mwizi mwizi, john na yule kijana mwingine wakafanikiwa kuruka na kutokomea, lawrance kwa vile alikuwa hajui chochote akabaki ameduwaa ndipo walipoanza kumshambulia

Akafanikiwa kuwachomoka akaingia kwenye nyumba moja bodaboda wakaizunguka ile nyumba kwa vitisho kuwa mwenye nyumba asipomtoa watachoma nyumba, wakaanza kuvuta mafuta toka kwa bodaboda zao, mwenye nyumba akaingia woga ikabidi lawrance atolewe wa bodaboda wakamtia mikononi kila alimshambulia anavyotaka mpaka mauti yalipomfika kila mtu akakimbia zake.

Baada ya uchunguzi ikagundulika kuwa john ndie aliyeiba bodaboda na wamemuua lawrance asiekuwa na hatia
 
Pole sana,
wakati mwingine angalieni na haya majina mnayotumia jamani KikulachoChako
kwetu wanasema jina linakufuata;
 
Last edited by a moderator:
Ni wiki sasa imepita kuna kijana wa miaka 17 kauawa huku kimara mwisho njia ya bonyokwa millenium. Huyu kijana alijiingiza kwenye ufundi wa bodaboda baada ya wazazi wake kushindwa kumlipia ada. Siku ya idd tar 29/7/2014 marehemu aitwae lawrance alishinda nyumbani kwao tu maeneo ya mavurunza kimara, ilipofika saa kumi kuna kijana aitwae john alifika nyumbani kwa akina lawrance kwa lengo la kumuomba akamtebgenezee bodaboda. ilipofika saa moja jioni wakaanza safari kuelekea mahali bodaboda ilipo, kufika kule kijana lawrance akafanikiwa kutengeneza ile pikipiki sasa ile aijaribu akiwa amempakia john na kijana mwingine ambaye hakufahamika hatua chache mbele wakasikia mwizi mwizi, john na yule kijana mwingine wakafanikiwa kuruka na kutokomea, lawrance kwa vile alikuwa hajui chochote akabaki ameduwaa ndipo walipoanza kumshambulia, akafanikiwa kuwachomoka akaingia kwenye nyumba moja bodaboda wakaizunguka ile nyumba kwa vitisho kuwa mwenye nyumba asipomtoa watachoma nyumba, wakaanza kuvuta mafuta toka kwa bodaboda zao, mwenye nyumba akaingia woga ikabidi lawrance atolewe wa bodaboda wakamtia mikononi kila alimshambulia anavyotaka mpaka mauti yalipomfika kila mtu akakimbia zake, baada ya uchunguzi ikagundulika kuwa john ndie aliyeiba bodaboda na wamemuua lawrance asiekuwa na hatia

Dah...! So sad.
 
Kwa reference zote hizi TAFAKARI KISHA CHUKUA HATUA, OKOA MAISHA KWA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI tunaposhuhudia hali hii, si kila aitiwaye mwizi ndiye.
 
Ila outlook yako pia inakufanya uwe safe. Mfano ninavojipigiliaga napotoka nyumbani,siriazness napikua public transports, mapozi nini asee ukiniitia mwizi nahisi watu wote watakuhamaki.

aaah wapi! kwa taarifa tu, wezi wa siku hizi wanavaa kama wanaenda maofisini posta mpya na maeneo mengine ya heshima
mkuu usiamini mtu kirahisi rahisi, kuna jamaa mmoja hivi ambaye sikudhani kabisa angeweza kuwa kibaka wa kutupwa,

jamaa alikuwa amevaa vizuri sana na kuonekana super smart, utadhani anaenda mkutanoni AICC, kumbe waapi ni kibaka mzoefu tu!

Basi bwana, kuna jamaa yangu alikuwa na sim mpya, miaka mitatu hivi iliyopita, ilikuwa ni nokia X2-01 enzi hizo zinatoka..

jamaa kakaa pembeni na simu yake anapata soft soft baridi huku ameweka simu pembeni na stori za hapa na pale.. huku pembeni naona jamaa halitulii, jicho lake liko kwenye simu tuu! najiluliza kimoyo moyo, vp jamani mbona hivi? au kibaka?

nikaamua tu kuichukua ile simu ya rafiki yangu nikawa nimesihikilia mkononi makusudi tu nione jamaa atafanya nini.. baadae jamaa akaondoka! kwa kweli hakuwa na kazi yoyote ya msingi eneo lile..

Baadae kuja kupeleleza, nikaambiwa huyo ni kibaka mzoefu!...

so, mavazi hayawezi kuniaminisha kwamba wewe ni msafi sana moyoni mwako!

Halafu pia kuna ule ukbaka unaokujaga kutokana na ushaiwshi tu wa ghafla wakati wewe si kbaka, hapo pia waweza iba!
 
Dah! Jamii forum baba lao. Nasoma experiences za watu najifunza mambo mengi sana. Poleni wote mliokutwa na hii mikasa.
 
Ila outlook yako pia inakufanya uwe safe. Mfano ninavojipigiliaga napotoka nyumbani,siriazness napikua public transports, mapozi nini asee ukiniitia mwizi nahisi watu wote watakuhamaki.

siku hizi hakuna kitu kamahiko, nakumbuka 1999 nikiwa kwenye kipanya kwajirani zetu wa +254, hukoo Kitale, nilivyoingia nikabahatika kukaa siti moja na jamaa mmoja ambaye kwa umri alionekana ni mdogo kwangu, lakini na mwili kunizidi na kitambi kimefutuka, kavaa vizuri suti yake ya dark blue, kanyoa vizuri amependeza ukimwangalia wala hauwezi kumtilia shaka, mimi nilikuwa kawaida tu kisafari na kijibegi changu cha mkononi nilivokaa kwenye siti nikaweka kibegi mapajani.

Tumeenda katikati ya safari nikawa nahisi kitu kinakwaruza kwenye bei upane wa huyo jamaa, akili ikafanyakazi haraka sana nikasema nisimshtue nisijekuwa namsingizia nikaumbuka mimi, nikawa kimya kama kausingizi kananipitia, akaungua zipu ya begi akaingiza mkono, alivyozamisha mkono tu nikaukamata, hakukurupuka wala kufanya purukushani yoyote, tukamshuka kwenye checkpoint tukaendelea na safari.

Katika story na abiria kumbe wanamjua ni wa eldoret na mimi jana yake tu nilikuwa Unga Limited Eldoret, nikajua atakuwa alinifuatilia akijua natembea na pesa kwenye begi kumbe sina kitu!

Wezi wa siku hizi wakomakini sana wanajitahidi kublend-in, ni ngumu kumshtukia ndiyo maana watu wasio na hatia wanauwawa!
 
Stering hauwawi ila chamoto atakipta

Lol! Ka movies za Van Damme, AWOL, sterring alikula kichapo kitakatifu, mwisho wa siku alishinda kwa kuchechemea. Kweli tujifunze kutokana na experiences za wenzetu.
 
Da pole sana kaka mi ilinitokea Sinza siku moja kwenye lodge moja hivi. Nilikuwa na Shem wenu ndani ya chumba tukagombana coz ma gal alikuwa anawivu sana.

Baada ya kugombana nikabidi mi nisepe zangu nikaona hamna dalili ya kupata mzigo hapa but kipindi naondoka Shem wenu alikuwa yupo anaoga.. Mi nipo njiani nakaribia pale meeda nikaona kundi kubwa la watu km 10 hivi wananifata na kuita mwizi mwizi mi nikashangaa vp. Ghafla namuona mlinzi wa lodge anasema kuna demu mmoja Anasema umemwibia pochi yenye laki 2..watu baada ya kusikia hivyo wakaanza kunipiga mdogo mdogo kwamba lazima tukuchome wewe, watu wakawa wanaongezeka na kipondo kinaongezeka yani sipati hata muda wa kujitetea.

Mara gafla akatokea jamaa mmoja tulipiga naye mzumbe chuo amani Mimi mtu huyu namjua twendeni turudi lodge Kwa huyo binti aliyeibiwa, basi tukarudi watu kama 20 ivi hapo nishapigwa sana jamani.. Tukafika guest house pale, Dada wa reception akasema yule msichana kaondoka sasa hivi kafatwa na mwanaume akiwa na gari..kuhusu pochi kumbe kaiona ilikuwa chini ya mto. Sitoisahau that day

yaani changudoa unataka tumwite shemeji?!!..tutake radhi!
pole sana lakini, siku nyingine ukichukua changu mpe maslahi mliyoelewana.
 
Back
Top Bottom