Mimi yalishawahi kunikuta mwaka 2008, natoka kwenye tamasha la kampuni flani ya simu mida ya saa moja jioni(ilikua ufukwe mmoja maarufu dsm) nashangaa kundi la vijana kama kumi hivi wanakuja mbio huku wakiniuliza " simu uliyoiba iko wapi" .
Kabla sijapata hata muda wa kujitetea tayari nilishapigwa ngumi mfululizo za tumbo na uso mpaka macho yamevimba kiasi cha kutokuona vizuri,
Walipoanza kunisachi nikawa kama nazuia kwa kuweka mikono mfukoni, nilipigwa visu vya mikono, uso, mgongoni na mkononi mpaka leo nina makovu makubwa ya kutosha.
Kisha wakachukua kila kitu huku wakiendelea kunishambulia kwa kelele za mwiziiiiii mwiziiii, hapo sasa raia wenye hasira zao wakamalizia hasira zao kwangu(ninachoshukuru ilikua beach hakukua na mawe wala tofali, hivyo kilikua kipigo cha ngumi, mateke na makuti,) nakumbuka mpaka nililishwa mchanga kama adhabu,
Kwa kweli Mungu ni mkubwa, kilichoniokoa hata siamini mpaka leo.
Nikipata muda nitarudi kuwapa mkasa mzima ni wa kuumiza sana.
Asubuhi njema wakuu.