Hatari: Nimeacha kutumia Nyama

Hatari: Nimeacha kutumia Nyama

kabichi/kabeji nayo kuna mtu kaniambia ni hatari sana kwa afya. Akasema ni mojawapo ya vitu wadudu wanapenda sana,sasa ili isishambuliwe na wadudu inapigwa dawa za kutosha na watu ambao hawana ujuzi wa kutumia viwatilifu. Na kwa asili yake jinsi inavyokuwa kwa kujikunja inajikusanya na kujifunga na zile dawa zinabaki mle ndani. Kwa hiyo ukila kabeji a.k.a kabichi una kula full chemicals ,na jinsi nilivyo mtu akielezea vitu vya kitaalam namwamini sana nimeacha kula hiyo kitu
Osha na vinega kabla hujaipika then you're good to go
 
Sababu za kiroho sizipi uzito hata kidogo maana mimi sio mfia dini. Nikizisoma lau juujuu ni kama binadamu walikuwa na nguvu/maamuzi kuliko Mungu ndio maana akawaacha wale nyama umuri wa kuishi upungue wawe wakifa mapema kama njia ya Mungu kulipa kisasi utukutu wao wa kula nyama bila ruhusa yake.
Yani Mungu aliwawekea nyama kama kuwatega ili awahukumu!!? Yani kazi ya mikono yake yaani uumbaji wake anaujaribu yeye mwenyewe?
Kiafya 50/50 ila swali lipo ktk kizazi chetu. Babu yangu mzaa babu yangu alifariki 1996 na miaka zaidi 118, wajukuu, vitukuu na vilembwe tulikuwa zaidi ya mia 3. Babu zangu ambao ni watoto wa huyu babu ninaemzungumzia hakuna aliefariki chini ya miaka mia na, mmoja alifariki mwaka huu na miaka 110, babu yangu hasa mzaa baba yanyu yupo anamiaka 96. Hii familia ilikuwa na uwezo wa kutosha enzi hizo ktk nyanja ya ufugaji na ukulima, mboga kuu ktk hizi familia hadi leo kwa mgawanyiko wake ni nyama. Walikuwa wakila nyama mpaka kisusio na maziwa.
Sasa basi, ktk waliokufa na walio hai hakuna alieugua ugonjwa wa kansa, hapa ndipo ninaposhindwa kukuelewa.
Vipi kuhusu wamasai amba nyama ndio chakula kikuu cha familia? Kama nyama ingekuwa sababu kuu ya ugonjwa wa kansa siniwao tu wangekuwa wamejaa Oshen road hospitali?
Chanzo cha kansa kwa uelewa wangu mdogo ni sumu tunazokula ktk mbogamboga za majani, baadhi ya matunda tunayoita ya kisasa muda mfupi, kuku wa wiki 3 na mayai yake, madawa ya hospitali, vinywaji vilivyosindikwa, sigara, pombe kali na haramu n.k.
 
we jamaa utakuwa ni rasta man si bure

umeacha kula nyama kweli nyama hii hii kabisa duuh hongera

ila fafanua vizuri usijekuta ulikuwa unakula nyama za binadamu na ndio umeamua kuacha sasa?
 
Wazee wa kimasai kuna ma mizizi wanagonga sana baada ya kula nyama na hata wana utaalamu wa kuandaa nyama.
Kama kuna wabobezi wa lishe watusaidie maana wenyewe kwa wenyewe tunachanganyana sana. nilikuwa nimeanza kupata kakitambi kuna mjamaa akaniambia punguza haka katambi maana na kenyewe ni ugonjwa kwa mujibu wa wizara ya afya. nikauliza napunguzaje? nikaambiwa punguza wanga hamia kwenye protein(nyama, mayai, matunda...........) kumbe nyama nayo ndo hivyo haisagiki haraka- Tufuate lipi sasa?
Hahahahaha unaweza kulia haki tena
 
TATIZO LA UBISHI WA WABONGO WANAPOAMBIWA MADHARA AU FAIDA YA KITU FLANI HAWATAKI HATA KUFANYA UTAFITI KWANZA WA FAIDA NA HASARA YA KITU WANACHOELEZWA ZAIDI YA KUJIKITA KATIKA UTETEZI KWA HOJA ZAO FEKI, INGAWA MTOA MADA YUKO SAHIHI ILA ANGESISITIZIA "NYAMA NYEKUNDU".
KWELI DUNIANI KUNA WATU, VIATU, VIJITU, MIJITU, MAJITU NA MAWATU.
HAPA JAMII FORUM KUNA MAWATU SABABU YA KUWA NA UBISHI WA KIWANGO CHA JUU KWA KILA KITU. NYAMA NYEKUNDU KILA SIKU INAKATAZWA NA MADAKTARI SABABU YA KULETA MADHARA CHUNGUNZIMA MWILINI LAKINI MTU ANAJITETEA ETI:
1. TUMEANZA KULA SIKU NYINGI MBONA HATUUMWI KAMA VILE KILA UGONJWA HUPATIKANA PAPO KWA HAPO NAKATI HAKUNA MAGONJWA HATARI SANA NA MAGUMU KUTIBIKA KIRAHISI YATOKANAYO NA UTENGENEZWAJI WA ATHARI MIILINI POLE POLE SIKU HADI SIKU.
MFANO:
KISUKARI, KANSA, TB, BP.
2. UNAWEZA KUACHA KULA NYAMA NYEKUNDU LAKINI KUFA UTAKUFA TU, UTAKWEPA KULA NYAMA LAKINI UTAKUFA KWA KULA PAPUCHI(UKIMWI), KUVUTA SIGARA(KANSA YA MAPAFU), KUNYWA POMBE KWA SANA(KISUKARI) AU HATA KUPATA AJALI KWA KUGONGWA NA VYOMBO VYA MOTO & KUZAMA MAJINI KWA MELI, BOTI AU MITUMBWI NA KUANGUKA HATA KWA NDEGE.
JE KWANINI HATULALI NA MILANGO WAZI MAJUMBANI IKIWA TWATEGEMEA ULINZI WAKE MUNGU KWA 100%?
KUCHUKUA TAADHARI SI KWAMBA NDIYO SABABU YA KITU KUTOKEA JAPO INAWEZA KUWA SABABU YA KUPUNGUZA KITU AU KUSABABISHA KISITOKEE KABISA NA NDIYOMAANA HATA MUNGU ALITUPATIA AKILI YA KUJUA MEMA NA MABAYA ILI TUWEZE KUWA NA TAADHARI KABLA YA TUKIO.
MFANO:
MAGARI HUWEKEWA MIKANDA YA KUFUNGA UNAPOSAFIRI KUZUIA ATHARI ZA KUDHURIKA SANA INGAWA WALIOWEKA HAWAOMBEI AJALI ITOOEE NA HAWAWEZI KUIZUIA LAKINI HULETA FAIDA MARADUFU KULIKO KUTOFUNGA MIKANDA WAKATI WA KUSAFIRI.
3. KUFA NI LAZIMA LAKINI MUNGU HAJATUELEZA TUKALALE KWENYE BARABARA ZA MAGARI TUGONGWE TUFE, TUKAINGIE KWENYE VINA VYA MAJI MAREFU TUFE AU TUJINYONGE ILI TUFE BALI TUFE KATIKA MPANGO WAKE MUNGU.
SO KUFA ISIWE SABABU YA MTU KUTOCHUKUA TAADHARI LA SIVYO WATU TUSINGETHUBUTU KABISA KWENDA HOSPITALINI KUTIBIWA NA MADAKTARI TUKIUMWA SABABU KUFA NI LAZIMA.
4. KWANINI HAMTAJI AINA YA MITISHAMBA NA MIZIZI AMBAYO HAO WAMASAI & WAADZABE HUTUMIA KUJIKINGA NAYO NA KUONDOA SUMU MIILINI ZAIDI YA KUWATAJA TU KUWA WANAKULA NYAMA MARA NYINGI TU BILA YA KUUMWA AU KUFA?
HIVI KUTATAJWA MAKABILA YALIYO VIZURI KTK MATIBABU NA KUJIKINGA MWILINI VIZURI UKAACHA HAO WAMASAI TOFAUTI NA HAWA WA MJINI MATAPELI?
TUWE TUNAKUBALI KUELIMIKA TUNAPOELIMISHWA.
5. PROTINI HUHITAJIKA KTK MIILI YETU KWA FAIDA MBALI MBALI KAMA VILE KUIMARISHA HOMONI ZETU BUNADAMU LAINI SI LAZIMA HIZO PROTINI ZITOKANE NA NYAMA TU BALI ZINAWEZATOKANA NA SAMAKI, VYAKULA VYA MBEGU MBEGU KAMA VILE SOYA, KOROSHO, KARANGA NA MAHARAGE, MATUNDA(PARACHICHI) & NAZI, MAZIWA NA MBOGA MBOGA KAMA VILE SUKUMA WIKI NA MAJANI YA KUNDE.
6. NYAMA ZA ENZI ZA MABABU ZETU ZILIKUWA HAZICHOMWI SINDANO MARA KWA MARA KAMA HAWA NG'OMBE WA KISASA NA HATA HIVYO WAZEE WETU WALIKUWA WANAFANYA KAZI NGUMU SANA KWA KUTEMBEA UMBALI MREFU, KULIMA MASHAMBA NA KUPALILIA KWA MIKONO TOFAUTI NA KIZAZI CHETU CHA LEO KINACHOTAKA KUFANYA KAZI KIDOGO TU NA KUKAA SIKU NZIMA BIPA YA KUTOKWA HATA NA JASHO.
IKUMBUKWE KUWA SUMU KTK MIILI YETU HUTOKA KWA HAJA KUBWA, MIKOJO NA JASHO, SO MIMENG'ENYO YA BABU ZETU ILIKUWA MIKUBWA SANA KWA SABABU YA KUJISHUGHULISHA KWA KAZI NGUMU AMBAPO LEO HII TWAPASWA KUFANYA MAZOEZI YA KUTOSHA ILI KUONDOA SUMU KTK MIILI YETU KWA WALE TUNAOISHI MIJINI.
7. UKISHINDWA KULA KABISA NYAMA BASI JITAHIDI ULE HATA MARA 1 TU KWA MWEZI NA HAKIKISHA UMEIBANIKA MOTONI KWA WAVU IMEKAUKA VIZURI NA IPIKE ILAINIKE SANA NDIPO UTAWEZA KUPUNGUZA AU KUZUIA KABISA ATHARI ZA AFYA MWILINI.
Afadhali we nimekuelewa
 
Kuna jamaa ameanzisha uzi humu akiomba ushauri wa kuwa Vegetarian.
Kwa vile uzi huu unagusa kila mtu nimeona niandike hapa ili kila mtu afaidike na historia yangu ya kula nyama.

Mwaka 1993 ndo ulikuwa mwaka wangu wa kufanya maamuzi ya kuacha kutumia nyama yaani nyama zote za kuchinja kuku na wanyama wote. Sababu za kuacha nyama nimezigawanyisha katika makundi mawili.

1. Kiroho (spiritually) na 2. Kimwili (biologically?

Nitaanza na sababu za kiroho
Mungu ndo ametuumba sisi binadamu, chakula ambazo alikusudia mwanzo kabisa ni matunda tu ndo iwe chakula chake. Baada ya uovu, akaruhusu na mboga mboga.

Alikuja kuruhusu nyama baada ya gharika la Nuhu, lengo lake Mungu kuruhusu nyama ni hizi zifuatazo.

1. Kupunguza life span ya wanadamu maana matokeo ya ulaji wake ni magonjwa, na matokeo yake umri wa kuishi ukapungua kutoka mamia ya miaka hadi miaka mia hapa mwanzoni.

2. Aliwaruhusu kula nyama ili kukidhi tu haja yao ya tamaa, maana waliisha anza kutumia nyama kabla hawajaruhusiwa.

Ndio maana pia sehemu zote watu makini wa Mungu kama Daniel hawakutumia nyama.
Mungu alivyowatoa wana wa Israel alikusudia kutowapa nyama badala yake aliwapa Mana. Lakini walimlazimisha akawapa ndege kwale. Tukio lile lilimsononesha Mungu la kulazimisha kupewa nyama, ama la warudishwe Misri walipotoka. Biblia nzima ruhusa ya kula nyama ilitolewa kama tukia la sadaka, maana kula nyama halikuwafurahisha hata walaji kuchinja mnyama asiye na hatia kwa ajili tu ya dhambi zako.

Sababu za kimwili.

Miili yetu ilivyotengenezwa haihitaji nyama. Kwa kuwa mwili hauna storage ya protini, kwa kuwa nyama zote zina protein ya grade A. Recommended Daily Allowance ya protein kwa siku inayohitajika kwa matumizi mwilini kwa mtu mzima ni 30grams per day, yaani sawa sawa na uzito wa sarafu tatu za shilingi 10.

Protein ni muhimu kwa watoto ambao wanakua kila siku, kwa mtu mzima umuhimu wa protein ni kwa ajili ya ukuaji wa nywele na kucha tu hakuna kingine. Hivyo protein kwa mtu mzima ni negligible au haihitajiki sana. Zaidi ya hapo ni koungeza uchafu mwilini.

Uchafu kwa maana ya waste zinazozalishwa wakati wa kuiondoa protin mwilini.
Chemical zinazozalishwa wakati wa mchakato ni Amino acid kisha inabadilishwa kwa kuchanganya na madini mengine kama calcium ili kufanikisha kupata Urea na inatoka nje kama mkojo.
Mtengenezaji wa chemicali hizo ni Ini.

Hivyo protini kwa wingi mwilini hufanya Ini lipate load kubwa ya kutengeneza chemical za kuneutralize madhara ya protein. Ndio maana siku hizi kuna ugonjwa wa homa ya Ini kwa sababu ya matumizi makubwa ya protein, na pia ugonjwa wa UTI umekuwa common sana kwa sababu kipimo kinaonyesha particles nyingi za protein ambazo ni dalili kuwa hata figo zinazidiwa sana na chemicals zinazosababishwa na Ini.

Kwenye Amino acid kuna substance, ya Nitrogen ambazo ni kichocheo kikubwa cha uzalishaji wa seli za mwili. Uwepo wa Nitrogen kwa wingi mwilini ambao husababishwa na Amino acid ambayo ni zao la protini, huongeza uwezekano wa kupata kansa kwa vile kansa ni kuzaliana kwa seli nyingi kupitiliza.

Kwa vile zama hizi consumption ya protini ni kubwa hivyo maradhi yanayohusiana na ulaji huu ni yafuatayo.

Homa ya Ini:
Hii husababishwa na Ini kuzidiwa, yaani ini lingekuwa linaongea lingesema, jamani sasa hivi siwezi kutengeneza dawa za kurekebisha taka zenu mnazoingiza mwilini. Ini likizidiwa, yaani lina homa, linashindwa kuzalisha chemicali ya Insulini hivyo mtu hupata ugonjwa wa kisukari.

Wakati huo huo na figo nazo zinateseka, kongosho nk. Pia kama ini bado ni ngangali basi cancer zinaanza kukuotea sehemu mbali mbali, kama mauvimbe mwilini au lipoma ma MD wanaita. Na magonjwa mengine kama arthritis husababishwa na utumiaji mkubwa wa protein. Nyama pia huongeza acid nyingi mwilini. Na kwa vile miili yetu inataka vyakula vya alkaline, ni vyakula vyote alivyoumba Mungu vya mimea vina alkaline.

Vimelea wengi hustawi kwenye mazingira ya acids hivyo too much blood acid ni too much diseases.
Damu ikiwa ni alkaline hakuna kimelea kinachoweza kuishi mwilini. Ulaji wa nyama ni ukatili tu unaosababishwa na uchu wa binadamu hakuna kingine. HUWEZI KUWA NA AFYA NJEMA KWA KULA NYAMA.

Hizo tunaita old school tie, yaani ujinga tuliokalilishwa shuleni kwamba nyama ni chakula bora.
UNAPOCHUKUA HATUA KUACHA NYAMA hakikisha unakula vyakula mchanganyiko vilivyo na balanced diet pamoja na matunda mengi sana pamoja na maji. Utaenjoy afya njema ya mwili na roho.

Wakati naacha nyama kipindi hicho mwaka 1993 nilikuwa nahofu kuwa afya yangu itazorota. Lakini ipo vizuri sana sana magonjwa yamenikimbia, maana sijaumwa tangu mwaka 1999 hadi leo 2018 ni miaka 19 na sina mpango wa kuumwa, nang'atwa na mbu kila siku na kunywa maji salama yasiyokuwa treated na chemicals na siumwi.

Sio Mungu ananilinda, ila Mungu amenipa mwanga wa kuacha kutumia vitu visivyo na manufaa kwa afya ya binadamu sasa na enjoy life, labda kitu ambachosii enjoy ni kutokuwa na pesa na kutosha kula starehe za dunia.

Sasa MD's njooni mharibu uzi huu kwa kuleta mbwebwe zenu mkijifanya mna akili sana kuliko wote, mnashindwa kung'amua between right and wrong kutoka huko medical school.

Mimi sio MD hata biology sijasoma, nimesoma PCM tu ya O- Level, najua matkuja kutoa mapovu tu hapa, mnashindwa kuwaelekeza wagonjwa matatizo yanayowakabili, ninyi mnawashindilia madawa, wanakunywa wanaharibu organ muhimu mwilini, wanakufa. Au kwa vile jamii ni wajinga, na nyie mtasema tulikuwa tunaokoa maisha yake.
Hili bandiko linanifanya nianze kuwaza kuacha nyama...
 
Ingia kwenye tovuti ya shirika la afya duniani, mpaka leo hakuna tafiti zilizothibitisha ubaya wa nyama nyekundu katika tafiti zaidi ya mianane zilizofanyika ila tafiti chache zimeonesha ubaya wa processed meat katika kuleta kansa
Kuwa na akili si kusoma kila kitu na kukiamini, bali ukipewa wazo zuri au habari njema basi dadavua kwa kutumia akili yako ya kuzaliwa.
Hivi unawaamini wazungu kuwa wanakupenda kwa 100% bila kujua wengi wao hawakupendi kabisa bila ya kuwapa faida yeyote?
Wakupende wangekutengenezea UKIMWI ktk maabara ili uathirike na wakuuzie dawa ya kurefushia maisha "ARV" ukiishi kwa matumaini nakati wanaijua dawa halisi lkn sababu wanataka kuendelea kutajirika wakutawale vzr kiuchumi kwa kununua hizo dawa kwa gharama ya juu hadi serikali yako ndiyo iingilie kati kuzinunua?
Wangeweza kukupumbaza na ushoga nakati wanaelewa vzr kabisa athari zake kwa kutoongezeka idadi ya Watu kwa kuzaliana?
Wangeweza kukuletea makuku ya kisasa(mataira yasiyokuwa na baba wala mama) bali yameundwa tu kwa kemikali na kukuzwa kwa mwanga wa umeme?
Hivi ulishawahi kujua hata madhara ya vitu wanavyokuletea yakiwemo hayo mayai feki ya kizungu? Jaribu kuliweka siku 7 yai la kuku wa kizungu afu lipasue ndani uone kama utakachokikuta kitendana na afya yako.
Pia fanya vivyo hivyo kwa mayai ya kuku wa kienyeji ndipo utajua jinsi gani unapaswa uwe mtu wa kujifunza siyo kujua kila kitu ktk dunia ya leo.
Wangekuwa wanakupenda hao wazungu wangekutengenezea vitu vyenye mionzi mikali ya kukusababishia kansa, ukosefu wa nguvu za kiume na matatizo ya kufa kwa kizazi(ukosekanaji wa homoni za kiume kuweza kirutubisha yai la kike ili kiumbe kitungwe tumboni)?
Usiwe na mahaba kupita kiasi kijana kwani afya yako ni muhimu sana kwa nguvu kazi ya Taifa lako la leo na kesho.
 
Nyama, kitaalamu yapaswa kuliwa kwa kiasi na sio kutokula kabisa kwani ni chanzo cha protini ya daraja la kwanza. Kwashiorkor kwa watoto ni kwa sababu ya ukosefu wa protini hiyo. Umri unapoongezeka, kiwango kidogo cha protini huhitajika kwani kasi ya usagaji hupungua. Kwa ukosefu wa elimu tunakula nyama kwa wingi kila siku, matokeo yasababishayo mkusanyiko mkubwa wa uric acid kwenye damu, isababishayo gout ( aina ya arthritis yenye maumivu makali). Nyama za kuku, samaki, hasa wa baharini, ng'ombe na mbuzi, zapaswa kuliwa kwa kiasi kwa watu wazima (sparingly) na matunda, mboga za majani na maji mengi vitumike kwa wingi ( generously), na sio kuzuia nyama moja kwa moja
 
Back
Top Bottom