Hatari! Mtoto aunguzwa na mama wa kambo...!!

Nimesikitishwa sana na hii habari,Baadhi ya watu wana roho za ajabu sana
MTOTO.PNG

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida na kinyama mama mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Amina,
Mkazi wa Kigamboni Dar es Salaam amedaiwa kumuunguza mtoto Hawa Maulid Mbonde.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana zinasema kuwa baba wa mtoto huyo anaishi na mwanamke mwingine huku mama mzazi wa mtoto huyo yuko mkoani Mtwara akiwa ameolewa na mwanaume mwingine.

Aidha habari zaidi zinadai kuwa Maulid Mbonde aliachana na mama wa mtoto huyo muda mrefu na kuamua kuishi na mwanamke mwingine.

Siku ya tukio hilo inadaiwa kuwa mama wa kambo huyo alichukua maji ya moto huku mtoto huyo akiwa amelala akamwagiwa mwilini na kumsababishia majeraha makubwa.Imedaiwa kuwa baada ya mama huyo kufanya tukio hilo alitoroka hadi sasa hajulikani alipo.

source;gumzo la jiji
​

​
Inasikitisha sana! hii si chengine bali ni wivu, huyu mama wa kambo itakua amevumilia kumlea huyu mtoto akitegemea kwamba na yeye angepata wa kwake karibuni! huenda ameshakaa sana kwenye huo uhusiano lakini hajapata mtoto! Ni psychological trauma!!!!
 
Sasa anatoroka nini? Si akae hapo hapo! Kumbe anajua ni vibaya. Mkono wa sheria utampata tu!!!
Nimesikitishwa sana na hii habari,Baadhi ya watu wana roho za ajabu sana
MTOTO.PNG

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida na kinyama mama mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Amina,
Mkazi wa Kigamboni Dar es Salaam amedaiwa kumuunguza mtoto Hawa Maulid Mbonde.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana zinasema kuwa baba wa mtoto huyo anaishi na mwanamke mwingine huku mama mzazi wa mtoto huyo yuko mkoani Mtwara akiwa ameolewa na mwanaume mwingine.

Aidha habari zaidi zinadai kuwa Maulid Mbonde aliachana na mama wa mtoto huyo muda mrefu na kuamua kuishi na mwanamke mwingine.

Siku ya tukio hilo inadaiwa kuwa mama wa kambo huyo alichukua maji ya moto huku mtoto huyo akiwa amelala akamwagiwa mwilini na kumsababishia majeraha makubwa.Imedaiwa kuwa baada ya mama huyo kufanya tukio hilo alitoroka hadi sasa hajulikani alipo.

source;gumzo la jiji
​

​
 
Kweli nyie wanawake walio wengi ni nooma tena nooma sana mnaroho mbaya sana kwa hawa viumbe hasa wakiwa sio wenu
 
Wanawake wanajua uchungu wa mwana alafu ndo wanakuwa vinara wa unyanyasaji kwa watoto, Mungu amtangulie mtoto huyu apate kupona na kurudi ktk afya yake ya kawaida
 
Wewe ndo kama mimi.

hakuna mtu atakaeweza kulea mtoto wako kama utakavyomlea mwenyewe!! mtoto anataka kubembelezwa hata kwenye kula lakini nani atakae kaa ambembeleze wakati we hupo unaangahika na ya dunia
 
Mungu amrehem mwanamke huyo, Mungu amponye mtoto huyo naàmpe uwezo wa àjabu
 
Huyo ni kumuombea laana tu. Nayeye apate mtu amchome moto ivoivo aone raha. Yani binadam kama hujawa na huruma kwa watoto hufai hata kuishi
 
hakuna mtu atakaeweza kulea mtoto wako kama utakavyomlea mwenyewe!! mtoto anataka kubembelezwa hata kwenye kula lakini nani atakae kaa ambembeleze wakati we hupo unaangahika na ya dunia

Waswahili wamesema 'msi mama kaumili hakuna mama wawili'
 
Kweli nyie wanawake walio wengi ni nooma tena nooma sana mnaroho mbaya sana kwa hawa viumbe hasa wakiwa sio wenu

Wengine wanayafanya hayo hata kwa watoto wao. Ilimradi kuna mtu kaahidi ndoa wakiti akiwa home kwa wazazi han dili na mtangaza ndoa hamtaki mtotot
 
Back
Top Bottom