Heaven on Earth
Platinum Member
- Mar 21, 2013
- 37,234
- 26,754
Nimesikitishwa sana na hii habari,Baadhi ya watu wana roho za ajabu sana
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida na kinyama mama mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Amina,
Mkazi wa Kigamboni Dar es Salaam amedaiwa kumuunguza mtoto Hawa Maulid Mbonde.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana zinasema kuwa baba wa mtoto huyo anaishi na mwanamke mwingine huku mama mzazi wa mtoto huyo yuko mkoani Mtwara akiwa ameolewa na mwanaume mwingine.
Aidha habari zaidi zinadai kuwa Maulid Mbonde aliachana na mama wa mtoto huyo muda mrefu na kuamua kuishi na mwanamke mwingine.
Siku ya tukio hilo inadaiwa kuwa mama wa kambo huyo alichukua maji ya moto huku mtoto huyo akiwa amelala akamwagiwa mwilini na kumsababishia majeraha makubwa.Imedaiwa kuwa baada ya mama huyo kufanya tukio hilo alitoroka hadi sasa hajulikani alipo.

source;gumzo la jiji