Kuna utata mkubwa umeghubika tukio la kuwepo kwa yule jamaa mtafsiri wa lugha za alama jana wakati wa mkusanyiko wa msiba wa mzee Mandela pale katika uwanja wa FNB kwa kuwa inadaiwa hakupewa kazi hiyo na serikali ya Afrika Kusini na hadi leo haijajulikana alifanya kazi ile kwa ridhaa ya nani, ingawa inadaiwa mtu huyo hukodiwa mara moja moja katika mikusanyiko ya chama tawala cha nchi hiyo ANC. Baadhi ya vyombo vya habari vimeibua inayowezekana kuwa ni kashfa nzito ya kiusalama kwa serikali ya Rais Zuma ambapo ingekuwa hatari kubwa kama mtu huyo angejitwisha 'milipuko'! Mtu huyo alikuwa kushoto kwa wazungumzaji wakuu, akiwemo Rais Barack Obama (wakati akitoa hotuba yake).
Source: CNN News leo!
Source: CNN News leo!