Hatari iliyopo kuhusu Waendesha Bodaboda na vijana wa mtaani

kilimajoy

Senior Member
Oct 31, 2010
132
7
Hello Wadau,

Kwa siku za hivi karibuni kumekua na ongezeko kubwa la waendesha pikipiki aka bodaboda. Hatukatai ni ajira ambayo imewawezesha vijana wengi kujiajiri. Ila tutambue ya kwamba kitu chochote kisipokua na control ya kutosha kinaweza kikawa ni tatizo kubwa. Siku za hivi karibuni, kumeibuka mtindo ambao ni hatari sana, mfano pale ajali inapohusisha boda boda,... bila kujali aliyekua na makosa ni nani.. hawa jamaa wamekua wakikusanyika kwa umoja wao na mara nyingi wamekua wanafanya fujo na kama ni ajali inayohusisha gari basi mwenye gari anaweza kupata madhara.

Ila cha kutisha zaidi, hizi boda boda zimekua ndiyo zinatumika kwenye uhalifu wa aina zote, kuanzia kupora watu vitu mikononi, kwenye kutekeleza tukio la ujambazi, mauaji n.k. Wengi wao wamekua ni wale vijana ambao walikua hawana ajira na wengine walitoka kwenye wimbi la uhalifu wakahamia kwenye boda boda. Ila hatari nyingine ni kwamba, hawa jamaa wanaweza wakajiunga kwa pamoja na kuunda vikundi vya kihalifu ambavyo nijuavyo mie kwa uwezo wa jeshi letu tunaweza kushindwa kukabiliana nao.

Wengine wanaotisha amani ya nchi hii ni hao vijana wadogo waliozagaa kila pembe ya mji wa Dar es Salaam. Hawa vijana ni wadogo sana, na ni rahisi kutumiwa na wanaotaka kufanya uhalifu wa namna yoyote ile.

Ushauri wangu kwa kila mmojawetu, tutoe mawazo yetu njia sahihi ya kukabiliana na hatari hii ambayo imeshatokea na inayoweza ikahatarisha kabisa usalama wa nchi yetu tusipokua makini. Hapa kwenye Jamvi watu tunafurahi kuchangia ila hawa jamaa wakichachamaa hata muda wa kuchangia tunaweza kukuta hatuna. Kwa wale wenye mawazo chanzo na wenye kuona hatari iliyombele yetu tujadiliane hili.
 
Back
Top Bottom