Hatari! Dada aibukia kwa RC Makonda na kudai ametelekezwa na baba yake ambaye ni Mzee Edward Lowassa

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Mdada mmoja ameitikia wito wa Mkuu wa Mkoa Dar, Paul Makonda kuhusu wanawake waliotelekezewa watoto kufika ofisini kwake ili kupata msaada wa kisheria. Dada huyo amejitokeza na kudai yeye ni mtoto wa Mzee Edward Lowassa.

Amesema..
''Nimetokea Kigamboni, nimekuja hapa, nimekuja kusikiliza wito wa mkuu wa mkoa, Makonda kwamba watu ambao wametelekezwa. Sasa mimi ni mmoja wa mtoto ambaye niliyetelekezwa, ambaye baba yangu ni Edward Lowassa. Nimeanza kumtafuta toka nikiwa darasa la sita na mama ananambia ni kweli baba yako ndio huyo huyo. Sasa nimefuatilia kila sehemu lakini sioni mafanikio kwa hiyo nimekuja hapa kwa mkuu wa mkoa Makonda anisaidie kwa hali na mali kwa vyovyote vile itakavyokuwa kama nipo tayari nipimwe DNA na huyo mzee Lowassa ili nisaidiwe nijue nakaa wapi. Kwasababu mama yangu mzazi yupo hata akija atatoa ushahidi na atasema kwamba itakuwaje kama DNA nipimwe basi.''


Lowassa.jpeg

Habari zaidi, soma=>Aliyedai kuwa mtoto wa Lowassa akamatwa na Polisi, ni baada ya kuomba radhi
 
Kwa mujibu wa tangazo la RC, aliyetakiwa kuja ni mama yake au ni huyu mtoto? Kama ni kweli lakini.

Kwa kuwa huyu binti hajamtaja huyo mama yake wala kutaja jina lake, lakini tayari wameshamchafua baba wa watu, na huyo mama anaweza asipatikane kama alivyokuwa yule kada wa ccm aliyemuokoa na kumsaidia Nondo, naanza kuingiwa na mashaka na hili zoezi zima.
 
Saga on move..
Naona lengo linatimia,hivi kweli una akili timamu unachoma nauli kwenda kujidhalilisha,wangekuwa wanaenda pewa hela za matumizi sawa,wangetupa mrejesho wa Vijana wasio na ajira waliowajaza leaders mwaka Jana vipi wamefikia wapi kuhusu kuwapatia ajira,awajamaliza moja wanarukia mengine, ili wamake headlines, cheap politics.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom