Hatari cheti feki wanarudishwa kazini

Hatari cheti feki wanarudishwa kazini

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,940
Reaction score
7,847
Binafsi nimeshituka kusikia waziri anasema kati ya cheti feki kiasi cha alfu kumi na tano hivi 4000 wamerudishwa. Kiasi hiki ni kikubwa sana. Hii inatia shaka kama zoezi la kuwatambua lilifanyika vizuri. Vinginevyo tuamini cheti feki wanatumia ujanja na rushwa kurudishwa kazini. La msingi kutambua cheti feki ni fisadi wenye hila kubwa na ni hatari sana kwa mstakabali wa weledi nchini. Ni watu waovu kupindukia. Wapo wasomi na wataalam wahitimu wa kweli wengi wamedhulumiwa na hawa vibaka ambao wameweza kuwadhibiti wasomi wakweli sehemu zao za kazi hivyo kudhuru ufanisi wa kazi sehemu nyingi. Yafaa umma kufuatilia na kupewa taarifa kuona kama kweli vyeti feki wanaorudi wanavyo vyeti halali.
 
Umaskini huu. Mbona wapo wengi tu wameshasahau hata kama waliachishwa kazi na wengine weshafungua hadi biashara na wameajiri wenye hizo degree? We endelea kudhani kuna Mtu amekalia riziki ya mwingine wenzio wanatafuta maisha.
 
Mchakato wa kuwabaini wenye vyeti feki ulikosa weredi na kujaa woga wa utekelezaji. Wapo walionewa kweli.
 
Umaskini huu. Mbona wapo wengi tu wameshasahau hata kama waliachishwa kazi na wengine weshafungua hadi biashara na wameajiri wenye hizo degree? We endelea kudhani kuna Mtu amekalia riski ya mwingine wenzio wanatafuta maisha.
riski=riziki
 
Binafsi nimeshituka kusikia waziri anasema kati ya cheti feki kiasi cha alfu kumi na tano hivi 4000 wamerudishwa. Kiasi hiki ni kikubwa sana. Hii inatia shaka kama zoezi la kuwatambua lilifanyika vizuri. Vinginevyo tuamini cheti feki wanatumia ujanja na rushwa kurudishwa kazini. La msingi kutambua cheti feki ni fisadi wenye hila kubwa na ni hatari sana kwa mstakabali wa weledi nchini. Ni watu waovu kupindukia. Wapo wasomi na wataalam wahitimu wa kweli wengi wamedhulumiwa na hawa vibaka ambao wameweza kuwadhibiti wasomi wakweli sehemu zao za kazi hivyo kudhuru ufanisi wa kazi sehemu nyingi. Yafaa umma kufuatilia na kupewa taarifa kuona kama kweli vyeti feki wanaorudi wanavyo vyeti halali.

Si kweli hata kama wametumia vyeti si vyao Lkn wamekaa darasani Na Huwezi ufeki utaalamu.Huwezi ufeki ualimu,udaktari,uinjinia,udereva nk cheti ni makaratasi.Nchi zilizoendelea huwa awahangaiki Na vyeti Bali output ya MTU.
 
Umaskini huu. Mbona wapo wengi tu wameshasahau hata kama waliachishwa kazi na wengine weshafungua hadi biashara na wameajiri wenye hizo degree? We endelea kudhani kuna Mtu amekalia riziki ya mwingine wenzio wanatafuta maisha.

True Na wapo waliofanikiwa Na wanajuta walipoteza mda wao .Pia wapo walioajiriwa sekta binafsi wengine nje ya nchi Kwa package kubwa Na umshukuru Mungu Kwa kuachishwa Na watazama vyeti makaratasi badala ya output ya MTU.mfano si umeona madereva vyeti wanavosababisha ajali za watendaji kila mara tofauti Na wale madereva waliofukuzwa.
 
Si kweli hata kama wametumia vyeti si vyao Lkn wamekaa darasani Na Huwezi ufeki utaalamu.Huwezi ufeki ualimu,udaktari,uinjinia,udereva nk cheti ni makaratasi.Nchi zilizoendelea huwa awahangaiki Na vyeti Bali output ya MTU.
Ndiyo maana nimesema hili ni jambo la kijinga lililofanyika kijinga.

Yaani Juma Kampa Cheti cha kidato cha nne daraja la tatu Moses, Moses Kaenda kidato cha tano, juma kaamua kuwa mfanyabiashara. Moses Kafaulu mtihani wa Kidato cha sita na kujiunga na Chuo Kikuu cha tiba Muhimbili.

Moses Kasoma na kumaliza masomo na baadhi ya wenzake waliokuwa na vyeti vyao halisi walifeli yeye akafaulu. Kwa miaka zaidi ya saba ni Moses aliyekuwa anasoma na si Juma aliyeamua kuwa Mfanyabiashara.

Sasa Elimu ya Udaktari anayo Moses ama Juma? Na amegushi udaktari ama nini? Maana na yeye alisoma hadi kidato cha nne ila hakufaulu mtihani.

Halafu mfumo wetu wa kusahihisha mitihani ya sekondari una tija na usawa kwa kiasi gani? Jee karatasi ya Kwanza kusahihishwa kwake na mtu mmoja inafanana na karatasi ya 200 inaposahihishwa na mtu huyo huyo?
 
True pia mitihani sio kipimo sahihi cha kumtest mtahiniwa.MTU anakaa darasani miaka minne unampima Kwa Masaa mawili kumbuka kuna factor changizi zingine mfano stress,njaa,kushindwa kukadilia mda,kulielewa swali kumbuka watungaji utumia lugha ngumu,nk hivo mtihani sio kipimo sahihi.
 
Halafu Timiza mfumo wa kusahihisha mitihani kwenye kituo kimoja unaleta shida sana maana wasahihishaji hupewa mzigo mkubwa sana kwa kurundikiwa mitihani mingi.

Usahihisha huu ulifaa zama zile tuna shule chache za sekondari na wasahihishaji walikuwa wana uwezo wa kupitia kila karatasi ya mtihani kwa muda mrefu. Siku hizi wasahihishaji wanalipwa kwa kila karatasi wanayosahihisha.

Kwa mantiki hiyo kila msahihishaji anakimbikizana na kuongeza wingi wa karatasi ili apate posho nyingi zaidi.
 
Binafsi nimeshituka kusikia waziri anasema kati ya cheti feki kiasi cha alfu kumi na tano hivi 4000 wamerudishwa. Kiasi hiki ni kikubwa sana. Hii inatia shaka kama zoezi la kuwatambua lilifanyika vizuri. Vinginevyo tuamini cheti feki wanatumia ujanja na rushwa kurudishwa kazini. La msingi kutambua cheti feki ni fisadi wenye hila kubwa na ni hatari sana kwa mstakabali wa weledi nchini. Ni watu waovu kupindukia. Wapo wasomi na wataalam wahitimu wa kweli wengi wamedhulumiwa na hawa vibaka ambao wameweza kuwadhibiti wasomi wakweli sehemu zao za kazi hivyo kudhuru ufanisi wa kazi sehemu nyingi. Yafaa umma kufuatilia na kupewa taarifa kuona kama kweli vyeti feki wanaorudi wanavyo vyeti halali.

Nadhani hujamsikiliza vizuri Mh Naibu Waziri, ni hivi katika lile zoezi,kuna watu walikata rufaa hivyo serikali ilipitia rufaa zao wakabaini kuna watu 4,160 walionewa hivyo kurudishwa kazini acha kupotosha watu ndugu jiangalie na upotoshaji wako sio mzuri sana na sijui unafanya hivi kwa lengo gani?
 
Si kweli hata kama wametumia vyeti si vyao Lkn wamekaa darasani Na Huwezi ufeki utaalamu.Huwezi ufeki ualimu,udaktari,uinjinia,udereva nk cheti ni makaratasi.Nchi zilizoendelea huwa awahangaiki Na vyeti Bali output ya MTU.
Mwaka jana tarehe 3/9/2018 mzee wa kanisa fulani alipoteza (fiwa) mtoto kwa sababu ya nesi asiye na uzoefu aliyemhudumia kwenye hospitali moja ya wilaya.
Iko hivi:
Baada ya kutumbuliwa vyeti feki na wenye elimu ya drs la 7, waliajiriwa manesi wapya wasio na uzoefu. Marehemu alikuwa na upungufu mkubwa wa damu (2%), kitabibu inasemekana ukiwa na damu kiasi kidogo namna hiyo, unapoongezewa damu inatakiwa iwekwe kwa rate (speed) ndogo sana. Sasa yule nesi mwenye cheti halali hakuzingatia hilo, matokeo yake ilisababisha umauti kwa mtoto.
Uzoefu na cheti ni vitu viwili tofauti sana, ni kama zilivyo mbali mbingu na nchi!
Viongozi wetu wanahitaji sana hekima ya Mungu iwaongoze wanapofanya maamuzi yanayogusa maisha ya watu!
 
Wenzetu walishatoka kuamini vyeti,cheti hata stationary unakipata skills ni lzm ukae darasani
 
Si kweli hata kama wametumia vyeti si vyao Lkn wamekaa darasani Na Huwezi ufeki utaalamu.Huwezi ufeki ualimu,udaktari,uinjinia,udereva nk cheti ni makaratasi.Nchi zilizoendelea huwa awahangaiki Na vyeti Bali output ya MTU.
Ebu fikiria yule Dr. aliyesoma hadi akapelekwa Urusi na serikali akafaulu miaka 7 akaja kufanya kazi hadi kufikia kuwa RMO moro halafu akaondolewa eti cheti cha form iv hakikuwa chake. Hata kama ni kweli maana udaktari hafanyii cheti cha form iv anafanyia ujuzi mwingi alioupata ndani na nje ya nchi. Watu hawa watafutiwe utaratibu mwingine au hata faini. Ila Daudi kwa vile hafanyi kazi yenye ujuzi anapeta tuu.
 
Kulikuwa hakuna tija kumfukuza Kazi mtaalamu aliyefanya Kazi miaka mingi kisha cheti cha form four tena cha miaka 20 nyuma MTU kasoma hadi urusi.Ilitakiwa waondoe Watumishi hewa Na sio wenye shida za vyeti,
 
Kwa mtazamo wangu mtu aliyeghushi cheti na aliyeghushi taaluma ni lazima watofautishwe. Kuna mtu hajasomea taaluma husika ila kachukua cheti cha mwingine na kujifanya ni mwanataalamu wa fani fulani, huyu ni mtu hatari na anastahili hata kushitakiwa.

Kuna mwalimu alifundisha kwa miaka 28 mwezi mmoja kabla ya kustaafu ikasemwa alighushi cheti. Akafukuzwa kazi na mafao yake akanyimwa.
 
Umaskini huu. Mbona wapo wengi tu wameshasahau hata kama waliachishwa kazi na wengine weshafungua hadi biashara na wameajiri wenye hizo degree? We endelea kudhani kuna Mtu amekalia riziki ya mwingine wenzio wanatafuta maisha.
Hujamwelewa. Ikiwa ni hivyo, hata hapo ulipo unaweza tendewa sivyo, hutalalamika? Utahamia shughuli nyingine kienyeji tuu? Kubwa tuheshimu haki za wengine, haya ni mapito. Kuna watu wamefanyiwa vetting mbalimbali, mabosi vihiyo wamewaangusha!
 
Back
Top Bottom