BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 328
- 414
Wiki hii palizuka taarifa ya upotoshaji iliyodai Serikali imewarudisha kazini watumishi wa umma zaidi ya 4,000 walioondolewa kazini mwaka 2017 kwa sababu ya kughushi vyeti na watumishi hewa.
Msemaji Mkuu wa Serikali Ndugu Gerson Msigwa leo Jumamosi Agosti 28, 2021 wakati anazungumza na Wanahabari ametolea ufafanuzi taarifa hiyo kwa kusema:-
Watumishi waliorejeshwa kazini na kurudishwa kwenye orodha ya malipo ya mshahara ni wale ambao walioondolewa kazini mwaka 2017 kwa maagizo ya kuwataka wakatafute sifa ya kuwa na cheti cha kidato cha nne. Watumishi hawa ni wale wote ambao waliajiriwa kabla ya mwaka 2004 kwa sifa ya elimu ya darasa la 7.
Kwahiyo Serikali imewarudisha kazini na kuwarejeshea malipo yao ya mshahara watumishi hao 4,380 ambao baada ya kuondolewa kazini kwa sababu hawakuwa na sifa ya kidato cha 4, walikwenda kutafuta sifa ya elimu ya kidato cha 4 na sasa wameipata na ndiyo pekee ambao Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa kwa niaba ya Serikali ameagiza warudishwe kazini lakini sio wale walioondolewa kazini kwasababu ya kughushi vyeti na wale watumishi hewa, hao hawatarejeshwa tena kazini.
Kwahiyo taarifa ya kwamba Serikali imewarejesha kazini watumishi walioondolewa kwasababu ya vyeti feki na watumishi hewa ni ya uongo na ya upotoshaji mtupu.
#KaziInaendelea