Hataki nitazame simu yake

Seto

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
953
53
Kuna msichana nipo nae kwa uhusiano for about 4 years now, mi nafanya kazi flani hapa Dar na yeye yupo chuo flani Dodoma. Tulianza uhusiaano 2007 ye alikuwa Form 4 na mi nilikuwa Chuo. Ila shida napata naye siku zote ni kuwa yeye hupenda sana kuchunguza simu yangu ataanza maswali kuhusu contacts zote za majina ya kike asoyajua, message zote ila yeye ananikatalia yake. Alivyoona namsumbua kaamua kuweka SECURITY CODE. Kuna nini hapo?
 
Kuna ambacho hataki ukione kwenye simu yake,heshimu hilo.....:suspicious::suspicious:

If you do not trust her and she is not helping you to trust her ,then let her go.......:car:
 
Msalimie sana na mtakie maisha mema yeye na simu yake...Hapo wewe ni kondakta tuu..basi lina mwenyewe kaka.
Ogopa hiyo ni kama :A S-fire1:.
 
icon1.png
Re: Hataki nitazame simu yake

Msalimie sana na mtakie maisha mema yeye na simu yake...Hapo wewe ni kondakta tuu..basi lina mwenyewe kaka.
Ogopa hiyo ni kama
A%20S-fire1.gif
 
Huko peke yako.
Kuna mtu/watu mnasaidiana.
Hivyo uchague kuendelea kuwa nae kwa zamu ama kama huwezi basi usiumize roho bure.
Pole sana ndio ukubwa, mkuu;:)
 
mwizi siku zote hudhani mwenzie nae mwizi.anachunguza simu yako ili kuonakama una tabia kama zake za kuchanganya wanawake,huyu ni kumwacha fasta huko chuoni anachakachuliwa sana kuna wa kumfundisha,kuna wa kumchuna,kuna wa kumpa mambozzz na ww .pole
 
Si una yako? ya mwenzio unaitakia nini? Utaugua vidonda vya tumbo wewe kwa wivu!
 
Unataka nn kwenye simu yake? Yako huwa unamwachia acheki? Fanya yako mambo yaende ukichunguza sana Bata haliki.
 
Kaka angu hizo ni tabia za msichana mwenye mahusiano zaidi ya mtu mmoja. mimi mwenyewe yalinikuta hayohayo unahangaika na simu mpaka sometime unatamani kwenda kuoga nayo. ukishindwa yote hayo ndio unaweka security code?Nikaona sio dili nikaacha.Mtu unakuwa na wasiwasi saa zote utafikiri unaoga nje!

Jiulize kwa nini anaangalia ya kwako halafu ya kwake anaikatalia? hapo unaliwa babu! ndio yalee ya mmasai mchaga na wengineo. mwangalie sana huyo huko dom kuna mizee mibunge ina ngoma kama nini
 
Unataka nn kwenye simu yake? Yako huwa unamwachia acheki? Fanya yako mambo yaende ukichunguza sana Bata haliki.

well said, kifupi kuna mambo ambayo yapo kwenye simu yake ambayo hataki ww uyaone. Kwa hiyo ni uamuzi wako, kama utaona hali hiyo inakukwaza mweleze ukiona imeshindikana endelea kutafuta mwingine ili kuheshimu private zake.
 
imekula kwako la sivyo nawe weka password uone atakalofanya ndio ujue huna chako hapo.
 
Jamani siku zote mie nawaambia kuwa simu ya mkononi ni yako peke yako
Unatafuta nini kwenye simu mwenzio???? Kama si ugonjwa wa moyo??
 
SIMPLE. Nawewe piga mi pasword kila mahala, akikuuliza mwambie umemuiga yeye si kwa ubaya. Kwaro safi tu, then piga kimya uone atakavyo hangaika. Itamuuma kishenzi na atakoma then hapo ndo unamwambia hakuna mtu kugusa sim ya mwenzie. Mtaishi kwa amani sana, be a man and do it hakuna kuumia hapa.
 
Jamani siku zote mie nawaambia kuwa simu ya mkononi ni yako peke yako
Unatafuta nini kwenye simu mwenzio???? Kama si ugonjwa wa moyo??

Ndo hapoo, ukitaka usizeeke haraka kaa mbali na sim ya mwenzio.
 
Kuna msichana nipo nae kwa uhusiano for about 4 years now, mi nafanya kazi flani hapa Dar na yeye yupo chuo flani Dodoma. Tulianza uhusiaano 2007 ye alikuwa Form 4 na mi nilikuwa Chuo. Ila shida napata naye siku zote ni kuwa yeye hupenda sana kuchunguza simu yangu ataanza maswali kuhusu contacts zote za majina ya kike asoyajua, message zote ila yeye ananikatalia yake. Alivyoona namsumbua kaamua kuweka SECURITY CODE. Kuna nini hapo?
Hizo ni ishara kuwa miaka mi4 imefika mwisho.... siku zote mwizi huwa mwoga sana kuibiwa!!!:laugh:
 
acha kuchunguza simu ya mwenzako, nadhani ulichokuwa unakitafuta umekipata uchunguzi na wivu wako umeishia kuwekewa password sasa roho inakuuma unaona unaibiwa. Achana na simu za wanawake na pia mwambie mwenzako akae na simu yake aachane na yako. Kila siku simu zinaharibu mahusiano na nyie ni victims wa hali hiyo.

Halafu mmekaa ktk mahusiano miaka minne na mtu bila ya kuanza kufanya taratibu za uchumba na kuoa? ndio maana msichana amekuona huna maana zaidi ya kuona unampotezea muda na kwa taarifa yako wenzio wanakuchapia ndio maana umewekewa password ili usione kinachoendelea na umetafuta mwenyewe kuyajua na sasa yamekuzidia unakuja huku tukushauri.

Kingine mwanaume unatakiwa kuwa na msimamo na pia kama unahisi kuna tatizo wasiliana na mwenzio na umuulize kwa nn anaweka password kwenye simu yake, nadhani kama anakupenda na kukujali ataitoa hiyo password ila ukiona haijatolewa ujuwe hakupendi na hakuthamini

Mwisho videmu vya CBE Dodoma ni vicheche mno kama ndio yuko hapo kapime ngoma haraka kisha piga chini
 
Back
Top Bottom