Hataki nimchukue mwanangu, sijui anataka nini kwangu?

Hataki nimchukue mwanangu, sijui anataka nini kwangu?

Nakushauri utumie busara zaidi kuliko ubabe. Zungumza vizuri na kwa heshima na mzazi mwenzio mama Maureen. Huyo ni mtoto WENU...sio wa kwako (peke yako kama inavyotafsirika kwenye andishi lako). Jadilianeni. Nashauri priority iwe ni mafanikio na furaha ya mtoto zaidi ya kutanguliza egos na fantasies zenu. Kila la kheri mkuu
Asante kwa ushauri kaka
 
Mama siku zote ndio mlezi,labda awe na matatizo ambayo yeye mwenyewe ya kiakili au ulemavu.huwezi kumtoa mtoto kwa mama kwa kukimbia gharama! Tena una bahati kuna kitu kinaitwa 'child support'hii nataka sana ije bongo watu watie akili.
Hiyo kitu imekaaje mkuu explanation plz
 
Hiyo kitu imekaaje mkuu explanation plz
'Child support/maintenance' ni pesa ambayo kisheria inabidi alipwe mzazi ambaye anaishi,kumlea na kumwangalia mtoto.Hii ipo nchi nyingi za ulaya magharibi na America(usa&canada).
Ni suala la kisheria hivyo watu inabidi walipe au wanapelekana mahakamani,na huwa pesa hukatwa moja kwa moja kutoka kwenye mshahara hivyo ni vigumu kuikwepa.
 
'Child support/maintenance' ni pesa ambayo kisheria inabidi alipwe mzazi ambaye anaishi,kumlea na kumwangalia mtoto.Hii ipo nchi nyingi za ulaya magharibi na America(usa&canada).
Ni suala la kisheria hivyo watu inabidi walipe au wanapelekana mahakamani,na huwa pesa hukatwa moja kwa moja kutoka kwenye mshahara hivyo ni vigumu kuikwepa.
Thanks for explanation mkuu,imekaa bomba sana daah ije na tz tu vijana wawe na adabu wapunguze kuzalisha hovyo na kutelekeza watoto.
 
Kama mjuavyo kwamba ninao watoto watatu wa mama tofauti,SEAN,TRAVIS na MOUREEN,.sasa hao wa kiume wote wawili nilishawachukua na wapo pale kwa mama yangu mzazi na nimewatafutia house girl.wote wapo nursery shule moja maarufu hapa dsm na wana miaka minne wote ila wamepishana miezi tu.sasa nataka na Moureen nimchukue nimpeleke kwa mama pia ila mama Mama moureen hataki kunipa mwanangu kabisa.na huyu ndie mkubwa maana ana miaka 6.yupo darasa la kwanza.nataka nimchukue akae kwa mama yangu na wale wenzake maana naona naingia hasara sana kuhudumia huku na kule.ni bora niwe natuma pesa sehemu moja ieleweke moja.sasa mwenzangu kila nikiongelea kumchukua mtoto anakuja juu sana.nashindwa kuelewa lengo lake.tafadhari mama moureen najua upo humu na unasoma sana nyuzi zangu nakuomba unipe mwanangu ..
kisheria mtoto akizaliwa nje ya ndoa ni mali ya mama,na akizaliwa ndani ya ndoa ndio mwanao,kama hataki muachie kazalishe mwingine mbele ya safari na pia mwambie amtafutie baba yake huyo MOUREEN,ila nna uhakika atakuja kukutafuta babake,yashanikuta kama yako,binti aliwachenjia huko kwa mama yake na saiv ninae bure kabisa bila malipo yeyote,ni suala la muda tu mkuu!
 
Baadhi ya wanaume mnajifanyaga wazazi bora kuliko wamama wakati sio kweli. Hakuna anayeweza kulea na kujali mtoto vile ipasavyo kama Mama. Huyo aliyembeba miezi 9 na uchungu aliuupitia bila ya wewe kujua ana haki kubwa ya kukakaa na mwanae. Akupe huyo mtoto halafu mama wa kambo akammtese . Aendelee tuu kukaa na mwanae na hataki chochote kutoka kwako
 
Back
Top Bottom