juvenile davis
JF-Expert Member
- Apr 13, 2015
- 4,752
- 4,467
Kama mjuavyo kwamba ninao watoto watatu wa mama tofauti,SEAN,TRAVIS na MOUREEN,.sasa hao wa kiume wote wawili nilishawachukua na wapo pale kwa mama yangu mzazi na nimewatafutia house girl.wote wapo nursery shule moja maarufu hapa dsm na wana miaka minne wote ila wamepishana miezi tu.sasa nataka na Moureen nimchukue nimpeleke kwa mama pia ila mama Mama moureen hataki kunipa mwanangu kabisa.na huyu ndie mkubwa maana ana miaka 6.yupo darasa la kwanza.nataka nimchukue akae kwa mama yangu na wale wenzake maana naona naingia hasara sana kuhudumia huku na kule.ni bora niwe natuma pesa sehemu moja ieleweke moja.sasa mwenzangu kila nikiongelea kumchukua mtoto anakuja juu sana.nashindwa kuelewa lengo lake.tafadhari mama moureen najua upo humu na unasoma sana nyuzi zangu nakuomba unipe mwanangu ..