Hataki kuzaa kabla ya ndoa

Daah yani hata sielewi mkuu kuna hali napitia ngumu sana nimeona sehemu umeandika kwamba kama hatakuwa na uwezo kuzaa watatumia hyo nikajikuta natamani kujua kila kitu kuhusu hicho kitu.
Sijajua wanavyopatikana, ila ninachojua surrogate mother ni mwanamke ambaye anabeba mimba na kuzaa kwa ajili ya mwanamke mwingine ambaye hana uwezo wa kuzaa kwa sababu mbalimbali.

Mara nyingi huyo surrogate mother anakuwa anapandikizwa yai na mbegu kutoka kwa hiyo couple ambayo imemuomba awasaidie kubeba mimba kwa makubaliano, akishajifungua anawapa mtoto anapewa chake.
 
Hakuamini maana umekaa kujihami sana, pili yawezekana pia mimba aliyotoa haikuwa hata yako. Kajipime kwanza hospitali kbala ya kujihakikishia kuwa wew huwez kuwa na tatizo.
 
Wewe hebu usitake kumchanganya mtoto wa watu. Huyo binti anachokifanya ni kitu cha kipekee sana, anajaribu kujenga msingi mzuri katika maisha yake na kuondoa desturi mbovu ya familia yao ya kupata watoto nje ya ndoa na kuzaa zaa na wanaume hovyo bila adabu. Kwa kifupi anajaribu kubreak generational curse ya familia yake....

Msaidie kuliweza hilo. Huyo binti atakuwa mama mzuri kwa watoto wako kama utampa sapoti anayostahili. Kuoa wala si jambo la kufanya kwa gharama kama uwezo hauruhusu, fanya kitu very simple tena ikibidi kafungie mkoani kwao kama unataka kupunguza gharama zisizo za lazima, unaalika ndugu zako na rafiki wa karibu wachache, mnaenda kusheherekea habari kwisha, ukianza kuchanganya madawa muda huu utakuja kufeli......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mada ndeefu halafu kaandika upupu.
Binti alitoa mimba kwa sababu maisha yake hayaeleweki na hataki historia ya familia yake ijirudie kwake. Na anataka kuzaa ndani ya ndoa Leo unamwambia azae ndiyo umwoe. Unawaza vizuri kweli?

Na asiposhika mimba? Mapenzi yanaisha? Kama mimi ni huyo binti mpaka sasa hivi ningeshakuacha.
Miaka mitano kwenye uchumba mnatafuta degree ya udaktari?
Kweli kabisa nakuunga mkono, una akili sana..... Kama upo single njoo inbox

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha ujinga we jamaa. Binti yuko sahihi sana. She just needs assurance from you. We muhakikishie uone kama atakataa.

Kama umejipanga vizuri, kaeni chini mpange kupeana mimba. Ikishaingia tuu fanyeni mipango ya harusi chap chap within 3 months muwe mmeshafunga ndoa.

Ukipita huo muda hujamuoa basi awe huru kuitoa.

Mpe hiyo ahadi kama atakataa.
Unforgetable
 
Sijajua wanavyopatikana, ila ninachojua surrogate mother ni mwanamke ambaye anabeba mimba na kuzaa kwa ajili ya mwanamke mwingine ambaye hana uwezo wa kuzaa kwa sababu mbalimbali.

Mara nyingi huyo surrogate mother anakuwa anapandikizwa yai na mbegu kutoka kwa hiyo couple ambayo imemuomba awasaidie kubeba mimba kwa makubaliano, akishajifungua anawapa mtoto anapewa chake.
Nashukuru sana mkuu, kuna siku nitakupa mrejesho katika hili. Ubarikiwe sana.
 
Kwani kuzaa kabla ya ndoa ndo pete ya uchumba😂😂😂😂😂😂😂
 
Kabla ya yote, Karibu sana jamii foram, naona umejiunga leo asubuhi.

Mleta Mada chukua huu uchauri,na cha zaidi basi mnaweza kwenda hospital kupima nani ana tatizo au ukampime Yeye kama ana huo ugumba au la, ila cha luzingatia Watoto ni majaliwa japo amefanya kosa kitoa mimba hongera umemsamehe lakini, huyo binti ameonja uchungu wa single mother so hapendi kurudia mwelewe na me namsurpport huyo binti na usimuuzi au kumlazimisha ana uchungu na hapendi kufanya makosa Kama ya familia yake.

Kontoro@
pujo
financial services

Karibuni jamani Wapendwa mseme machache.
Niko upande wa huyo binti
 
Habari wana jf, mimi ni kijana wa miaka 32. Nipo kwenye mahusiono ya miaka 5 na binti wa watu mmoja. Nimekuja hapa jf kuomba ushauri kwa wakubwa zangu wenye uzoefu wa hili jambo maana linanitatiza.

Kipindi tuna miaka 3 kwenye mahusiano, mpenzi wangu alipata mimba ila bila kunipa taarifa aliitoa na taarifa akanipa baada ya kuitoa na nilidhibitisha kama alikuwa nayo na akaitoa. Nilimmind sana na tukakaa kama mwezi bila mawasiliano. Wasiwasi wangu ulikuwa ni kwamba atakuwa ameitoa mimba bila kunishirikisha kwa sababu hataki kuzaa na mimi.

Baadaye aliniomba msamaha na kunieleza historia yake fupi ya ukweli ya maisha aliyokulia. Kalelewa na single mummy, familia yao wamezaliwa watoto wa kike 3 ambao kila mmoja ana baba yake na baba yake hamjui hadi sasa.

Dada zake wote wamezalishwa tuu na hawajaolewa, dada yake mmoja kazalishwa na wanaume 3 tofauti na analea watoto wote mwenyewe na haishi na mume. Na dada mwingine ana watoto 2 naye anawalea bila mume.

Justification ya abortion aliyoifanya ni kutokana na historia ya maisha yake kuwa magumu kwahiyo asingependa mwanae naye akue bila baba kama yeye alivyokua. Na pia historia ya dada zake ambao wote wamezalia kwao kwa hiyo asingependa nayeye awe kama wao. Ilibidi nimwelewe na tukaendelea kudate hadi sasa tuna miaka 5 kwenye mahusiano.

Tangu naanza kudate naye nimemfuatiria sana kujua mienendo yake maana kwenye simu yake nilimwekea program ambayo nimeitengeneza mwenyewe ambayo naweza kusikiliza simu zote anazopiga na kupigiwa, naweza soma message zote anazotuma na kutumiwa, naweza angalia picha zote ambazo zipo kwenye simu yake, naweza soma message za whatsup, fb n.k pia naweza mrekodi sehemu yoyote aliyopo bila yeye kujua. Katika kumfuatiria kote issue ninazokutana nazo ni za kawaida ila sijawahi kuona akiwasiliana na mwanaume mwingine as if anadate naye. In short ni mwaminifu kwangu.

Nimekuja na pendekezo moja kwake na kumwambia kwamba kabla sijakuoa nataka nikupe mimba na uzae kwanza kwa sababu madhara ya kutoa mimba kwa mabinti wengi ni ugumba, au kupata mimba zikatoka. Kwahiyo mimi siwezi kukuoa na ukawa na matatizo hayo ambayo najua ulitoa mimba na hayo matatizo unaweza kuwa nayo so inabidi nikutest nijue kama nikikuoa ntaweza endeleza kizazi changu. Sio nakuoa tunaanza kwenda kwa waganga kutafuta mchawi nani kwanini hushiki mimba au tumalize mahospitali tukitakuta dawa ya uzazi.

Baada ya kumwambia hivyo kakataa katakata, kwamba yeye anataka azae akiwa kwenye ndoa.

Mimi sina wazo baya, wala sitaki kumfanyia uhuni wa kumzalisha na kumkimbia, mimi sina mwanamke mwingine zaidi yake ila wasiwasi wangu ni uzazi.

Mabinti wengi wanamatatizo ya kushika mimba kwa sababu walishatoa mimba kabla ya ndoa. Mimi sitaki kufanya hilo kosa.

Naombeni ushauri ndugu zanguni, je mimi nakosea au niko sahihi au nifanyeje ili mahusiano yaendelee vizuri?
hao Dada zake walikuwa na vizaz vya majaribio au ni mawazo yang tu
 
Unawajua wanadamu wewe? Kuna mtu anasaliti bila kutumia cm. Ushukukuru katoa mimba sio yako hiyo. Halafu mkuu hiyo ni laana kamwe haiwezi kuwatoka hiyo familia. Na wewe miaka mitano na mtoto wa watu kwanini usimuoe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom