G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,592
- 36,008
Naam muda utafika na haya yanayozungumzwa leo yatatekelezwa tu.
Sisi wote ni wazalendo, tena wazalendo tuliopiga kelele kwa muda kwelikweli. Tatizo letu kubwa huwa hatuachi kusema ukweli tena ukweli mchungu. Tulifungia makontena ya ACACIA pale bandarini kwa muda sasa huku tukiunda tume kuyachunguza. Sasa tuchague moja, kuwalipa fidia pale watakapodai ama kuishi kama watu ndani ya handaki, hakuna kutoka nje ama kutoa chochote. Hapo nimetumia mfano ila ni kuwa tutakapoamua kwenda kinyume na mikataba CCM waliyosaini basi tutaumia wote.
ACACIA hawakufanya biashara hewani, wamefanya biashara Tanzania na wamekaguliwa na vyombo huru tulivyojiundia sisi wenyewe, wao kama wao hawajawahi kutoka nje ya vyombo lukuki mliojiwekea enyi serikali ya CCM. Mna TMAA, mna CAG, mna ofisi ya AG, mna mahakama ya kibiashara na mbaya zaidi wanapitia kwenye njia zenu kupeleka mali zao huko ughaibuni.
Leo mnakurupuka kuwafungia kwa muda lakini tutalazimika kubuni vyanzo vingine vya mapato kuwaifidia kwa haya tunayofanya leo pale watakapoamua kufanya hivyo.
Uzalendo ukiambatana na mambo ya kujifariji na kuishi kwa matumaini ndani ya muda mfupi, huo sio uzalendo. Uzalendo huambatana na ukweli na suluhisho ambalo ukiliangalia tu unajua kuwa hili ni suluhisho. Badala yake sasa tunapiga tu blah blah na mbaya zaidi wanaotuchezesha zumari hili la blah blah wanaujua ukweli. Ole kwa wale wasiojua ukweli huo.
Jana rais Magufuli alichofanya ni kuwakumbusha tu watanzania kuwa Mkapa katuingiza cha kike. Akakumbushia machungu wee huku tukiuma meno kwa hasira. Lakini ni bora angesema pia hata haya makontena niliyozuia nitalazimika kulipa fidia pale itakapodaiwa. Huo ndiyo ukweli.
Narudia tena kuwa, ACACIA aki-step forward tu nitashangaa sana kama AG atatuma mawakili kwenda kutetea serikali! Kushinda kesi itakuwa ni ndoto ya mchana. Ni kweli tumepigwa kwa muda sana na sasa madini ni kama yanaishiaishia lakini kwa sasa tunayo maamuzi mawili tu (Haramu)
1) Kukubali kuendelea kupigwa kutokana na mkataba tuliosaini wenyewe.
2) Tuamue kufanya kama Mugabe (Huyu ni mwenzetu. Kamwe tusijilinganishe na kina Cuba, Ana Venezuela maana hawa wanajiweza sana kiuchumi). Na tukiamua kuishi kama Mugabe basi watakaoanza kuumia ni wale mafukara wa kutupwa. Kuumia kutaenda ngazi kwa ngazi hilo lipo wazi. Nje ya hapo tutakuwa tunapiga tu porojo.
Bahati mbaya sana yapo mavuvuzela humu ambayo tukiongea ukweli huu yanaleta kejeli na kuona kama tumenunuliwa! Lah! Acha tu muone hivyo lakini ukweli ndio huo! Hawa wamefanya biashara wakisimamiwa na vyombo lukuki vya serikali ya CCM, leo hawapaswi kamwe kulaumiwa. Na kinara anayelaumu naye alikuwa kwenye vikao halali vya baraza la mawaziri tangia mwaka 1998 hajawahi kuwa nje hata mara moja mpaka anakuwa rais. Bora hata Muhongo yeye aliyakuta ila siyo Magufuli.
Naona UVCCM wamepongeza, tofauti ni kuwa wakati Mkapa anasaini hii mikataba UVCCM ya wakati huo ilipongeza pia na kuuita uzalendo. UVCCM hiyohiyo ya enzi za Kikwete ilipongeza pia. Hawa huwa ni kazi yao kupongeza kila tukio la mkuu wao wa wakati huo. Ukweli ni kazi yetu sisi kuusema na ndiyo maana tunausema. Sisi ni wazalendo kweli ila pia ni wasema ukweli kweli.