Hata wanaume pia wapo makahaba……!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,334
Kama imetokea, ni mara chache sana wanaume wanaonunua miili ya wanawake kuzongwa na jamii. Kama ikitokea ni pale tu mwanaume fulani anaposhindwa kujilinda ipasavyo hadi siri yake ya kwenda kwa makahaba ikatoka.

Kwa kawaida wanawake ndio ambao wanalaumiwa, kutukanwa, kukashifiwa na kupata kila aina ya mzigo unaohusiana na ukahaba. Ni kama vile mwanamke anajiuza na kujinunua mwenyewe au kununuliwa na wanawake wenzake. Mwanaume ambaye bila yeye kwenda kununua mwili wa mwanamke, biashara ya ukahaba haiwezi kuwepo, huwa hatajwi kabisa linapokuja suala la kujadili ukahaba.

Bila shaka ni hali kama hii ambayo inawafanya watu wengi kudhani kwamba wanaume hawahusiki kwenye ukahaba, yaani wanashawishiwa na wanawake ambao kujiuza ndio shughuli yao. Kuvaa nguo fupi na mikao ya kihasara pamoja na vitimbwi vingine vimehesabiwa kwamba, ndivyo vyenye kumshawishi mwanaume kuingia kwenye kununua mwili wa mwanamke.

Inaonekana kama vile mwanaume anasamehewa kwa udhaifu wake wa kushindwa kujizuia anapoona maungo ya siri ya mwanamke, hivyo kosa ni la mwanamke ambaye amemshawishi. Lakini taarifa za kitaalamu zinazohusiana na ukahaba zinaonesha kwamba, hata kama wanawake wangekuwa wanavaa nguo ndefu zinazoburuza chini, ikishabainika kwamba ni makahaba, wanaume watamiminika kuwanunua.

Suala hapa siyo kushawishiwa na wanawake wanaojiuza. Wanawake wanaojiuza hujipitisha na kujinadi mbele ya wanaume kwa kuwahi tu kupata wateja, lakini hata wao wanajua kwamba, hawahitaji kujinadi kwa wanaume……………………….
 

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
32,771
23,031
unaponunua penzi tu ww ni kahaba mnunuzi, na anayeuza penzi kahaba muuza.

Achilia mbali kujiuza, Kuna wanaume wengine makahaba wa kichini chini, wanajilengesha kwa wanawake wenye fedha
 

Cantalisia

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
5,223
2,903
Asante baba kwa huu uzi coz wanawake tunaonewa sana ile hali bila hao wanaume huo uzinzi hautimii,kibaya zaidi na jamii nayo inawakingia kifua kwa kuwaona eti wao wanashawishiwa wakati wanaume wenyewe wanawafuata hao makahaba vijiweni mwao na kuwanunua,hebu nyie wanaume makahaba achen kwenda kuwanunua tuone watauzia miti?yani mjue kbs nyie wanaume makahaba kwa ninyi ndio wazamini wakuu wa ukahaba hapa dunian!
 

mjasiria

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
4,160
1,822
Asante baba kwa huu uzi coz wanawake tunaonewa sana ile hali bila hao wanaume huo uzinzi hautimii,kibaya zaidi na jamii nayo inawakingia kifua kwa kuwaona eti wao wanashawishiwa wakati wanaume wenyewe wanawafuata hao makahaba vijiweni mwao na kuwanunua,hebu nyie wanaume makahaba achen kwenda kuwanunua tuone watauzia miti?yani mjue kbs nyie wanaume makahaba kwa ninyi ndio wazamini wakuu wa ukahaba hapa dunian!
No offence lakini nawe kahaba?
 

Straddler

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
722
188
unaponunua penzi tu ww ni kahaba mnunuzi, na anayeuza penzi kahaba muuza.

Achilia mbali kujiuza, Kuna wanaume wengine makahaba wa kichini chini, wanajilengesha kwa wanawake wenye fedha

Kichini chini? Aaah Wapi..!!! Nenda beach za Zanzibar na Mombasa. Huko wanaitwa "Beach-boys". Kazi yao ni kujiuza kwa vi-bibi kizee tajiri vya kizungu.
 

lidoda

JF-Expert Member
Apr 27, 2008
641
573
Bana ehe, biologically mwanaume kaumbika kuwa awe na wanawake wengi. Mboan tunapofuga kuku au mbuzi tunakuweka majike mengi na dume moja?
 

charndams

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
437
126
bora kama na hili mmeliona wenyewe!
binafsi neno kahaba halijawahi kunitoka kinywani kwa ajili ya kumsuta mwanamke. wakulaumiwa kwa ongezeko la ukahaba duniani ni mwanaume. iwapo sisi wanaume tutakuwa responsible manyumbani kwetu na kuacha kupachika mahousegirl na wasichana wa watu mimba ovyo ovyo kisha watelekeza au hata wake zetu then hii issue tungeizika katika kaburi la sahau.
 

charndams

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
437
126
mkuu mtambuzi, ungeileta hii elimu mwaka juzi leo hii ukahaba ungekuwa umepungua kwa 50%. pia kuna kitu nimegundua, mada nzuri kama hii utapata haina wachangiaji wengi lakini mada kuhusu tigo, sijui nini..tena za kihuni ndo haswa watu wanajaa huko. hebu tuone leo niwangapi watatia sahii kwenye huu mjadala.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom